Hivi raha
iko wapi?, nambieni wana kundi
mtunzi
Saidi R Bunduki
Maisha haya
mafupi, nadhani hayana fundi
Si orijino
si kopi, si fureshi si mtindi
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Fukara alia
pesa, huamini ndipo sawa
Akipata atatesa,
kila mtu tamjuwa
Tangu zama
hadi sasa, bado hajafanikiwa
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Fukara
mawazo tele, usiku mang’amu ng’amu
Hata ugali
tembele, kupata ni kazi ngumu
Watoto
wasoma shule, hana pesa ya mwalimu
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Mke watoto
ni shida, nguo mipasuo hiha
Unaoitwa
uroda, yeye kwake ni karaha
Anawaza
kila muda, lini apate staha
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Anayeitwa
tajiri, sisi twamuona bomba
Mamia
ameajiri, fukara na omba omba,
Kumbe yuna
kisukari, kula yake ni jaramba
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Huitwa FOGO
mtata, ana magari lukuki
Mkosee ule
MBATA, popote humpeleki
Du! Tarifa
nlopata, Hasimami hasimiki
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Mwenye mali
hana heri, bora ulalae RAGO
Wengine
mali za siri, ajuae bi mdogo
Kutwa
anatafakari, Hata akikata GOGO
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Alimpenda
fulani, awe kwake ni faraja
Kumbe ye
kamtamani, azikidhi zake haja
Amebaki
mataani, kabaki na ngoja ngoja
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Aso ndowa mashakani, amechoka ubachela
Mwenza ana
mtamani, apunguze kuzurula
Leo nanga
zi angani, ndoa chungu tele hila
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Hana mwana
hana SUDI, mpweke anajiliza
Hospito
nenda rudi, na waganga kamaliza
Bado adaiwa
kodi, nyumba watamfukuza
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Haya ni
maoni yangu, msije nipatiliza
SIDE BOI
jina langu, BUNDUKI la kubatiza
Pia penye
lugha chungu, ushauri nasikiza
HII RAHA YA
MAISHA, IKO WAPI WAJAMENI?
Saidi R Bunduki
COMMENTS