-
JAMBO LANYEWE SI GENI, NGOJENI NIWAAMBIEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- NANENA TOKA MOYONI, WAHUSIKA MUSIKIE
- NAANDIKA KITABUNI, NA ASOME ASOMAE
- YULE ANOKUTHAMINI, HAKIKA TULIA NAEUSIMTIE KAPUNI, KUMUONA WA BADAEHEBU MUWEKE MOYONI, MAISHANI MKOMAEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- JE WENGINE HAWAONI?, SHANGAA USISHANGAEANGEMTAKA FULANI, ANGESHATEMBEA NAEKAKUFANYA WEWE HONEY, MAZURI MUONYESHEEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- ALIYEKUPA THAMANI, MSHIKE MSHIKILIEHUJUI KAPENDA NINI, KWAKO HADI AKUJIEHWENDA ALIPENDA DINI, YEYE NDIYE AJUAEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- NAWEWE MPE THAMANI, MOYO WAKE UTULIEAPATE RAHA MOYONI, DUNIA AFURAHIEUSIMPE MITIHANI, MAPENZI AYACHUKIEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- PENZI SIRI YA MOYONI, ANAJUA APENDAEUKIM BEZA MWENDANI, WAMFANYA APUNGUEMUULIZE ATAKANI?, KWAKO AJIRINGISHIEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- HILI JAMBO SIO GENI, FAHAMU NA UTAMBUEKAMA SI WEWE FULANI, MWAMBIE NAE AJUEHWENDA UKAWA KUNDINI, HATA KAMA KWA BADAEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- PENZI NI RAHA JAMANI, UPENDWAPO UPAJUEWALOBAKI HAYAWANI, MBELE MBELE WATEMBEEPOPOTE WAJIAMINI, NA HASA UKIWA NAEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- MTUKUZE WAKO HONEY, PUMZI AJISHUSHIEMPE NA CHA UVUNGUNI, UPEPO UMPEPEEMSHIKE JUU NA CHINI, ANGALAU MSIFIEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- NI MADHAMBI KUMHINI, ALOPENDA UWE NAETAMTIA MAWAZONI, MAAMUZI AJUTIENA HATA PINGU FUNGENI, ZA MAISHA UTAMBUEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- NISEMAYO SI MAGENI, NAYAJUA MFANOENAYAJUA KIUNDANI, SIOMBE YAKUTOKEENI HATARI HATARINI, UTAPOTEA MWISHOEMPENDE AKUPENDAE, LIWAZA HISIA ZAKE
- KUMI MBILI HAPA PINI, SITAKI NIENDELEENENO LANGU CHUKUENI, PUUZA UANGAMIENASEPA ZANGU MITINI, BUNDUKI NIKUAGAESIKU IWE NJEMA KWAKO, NAKUOMBEA MAZURI,
BY: Saidi R. Bunduki
COMMENTS