INSHA MADHARA YA ZINAA KATIKA JAMII Nini maana ya zinaa? Zinaa ni neno lenye asili ya kiarabu lenye maana ya kufanya mapenzi baina...
INSHA
MADHARA YA ZINAA KATIKA JAMII
Nini maana ya zinaa?
Zinaa ni neno lenye asili ya kiarabu lenye
maana ya kufanya mapenzi baina ya mwanaume na mwanamke ambao hawajafunga ndoa
kisheria. kwa Kiswahili chetu tunaweza kuita uzinzi.
Nini sababu za zinaa?
Zipo sababu nyingi ambazo zinaweza kusababisha
kitendo hiki katika jamii inayotuzunguka. Mimi nitataja sababu chache kutokana
na mtazamo wangu tu.
1. Utandawazi
Utandawazi umekuwa ni miongoni mwa vitu ambavo
vimesababisha kukithiri kwa matendo machafu katika jamii hususan zinaa.
Kutokana na kukithiri kwa mitandao ya kijamii isio na maadili, televisheni,
magazeti, radio n.k imekuwa ni miongoni mwa sababu kubwa za kuwafanya watu
wazame sana katika dimbwi hili la hatari.
Hii ni kutokana na elimu za mapenzi
zinazotolewa ovyo bila mipaka katika vyombo hivyo. Hivyo basi watu wengi
wakiwemo vijana wadogo wanazifuatilia elimu hizo na kuzifanyia kazi hali yakuwa
hawajaowa wala kuolewa.
2. Maisha magumu
Umasikini na ufukara umekuwa ni chanzo kikubwa
katika jamii tulizonazo kuweza kuingia katika janga hili la uzinzi. Suala hili
huwaathiri zaidi watoto wa shule, watoto wasio na wazazi au usimamizi wa
kutosha. Wanadanyanywa na watu wenye fedha zao na hatimae wanajikuta
wanatumbukia katika janga hili. Watoto wanashawishika kwa pesa kidogo ili
kukidhi mahitaji yao ya kila siku na hatimaye kuamua kujitia katika mapenzi
kutokana na umasikini walionao na wala si kwa matakwa yao binafsi. Hii sio kwa
watoto wa kike tu, hata vijana wa kiume wanaweza kushawishiwa na wanawake walio
na pesa ingawa kwa upande wa wanaume sio sana lakini pia hiyo ipo. (HUTAKI AU?)
3. Kukosa elimu ya dini
Jamii kutokuwa na elimu ya dini hasa dini ya
kiislamu ni tatizo kubwa sana kwani inafika kipindi mambo ya maasi yanaonekana
kama ni utamaduni na ni fasheni kwa mwenye kuyafanya. Na jambo kama hulijui
ubaya wake unaliona ni la kawaida hata kama lina madhara makubwa. Na kwa bahati
mbaya jamii zetu kwa sasa zimepuulia mbali suala la kusoma elimu ya dini kwa
kuona kuwa haina maana. Hapo imani ya Mungu inakuwa imekosekana na na shetani
anachukua mkondo wake kuweza kuwaongoza watu wa aina hiyo. (MUNGU ATUONGOZE)
4. Vishawishi kutoka katika makundi
Hakuna asiyefahamu madhara ya kufuata makundi
yasio na maadili. Makundi ya vijana mengi hua yanahimizana katika upotofu na
kusifiana katika mambo machafu. Miongoni mwa mambo machafu hayo kwa asilimia
90% ni zinaa. Kwa hiyo vijana wengi wanaoingia katika makundi hayo wanakutana
na story hizo na hatimaye nao kuanza kujaribu na hatimaye ni kuzama kabisa kama
sio kupotea katika jamii iliyo staarabika. Unapisikia makundi unaweza ukajua ni
ya wavulana tu, HAPANA hata wasichana nao wana makundi yao tena mabaya zaidi
ambayo hushawishiana katika mambo ya uzinzi. (MCHUNGE SANA MWANAO)
5. Migogoro katika ndoa
Hapa ni kwa wale wanandoa. Jamani migogoro
katika ndoa ni kitu kibaya sana. Narudia tena migogoro karika ndoa ni jambo
baya sana, haijalishi mgogoro huo umetokana na nini. Ubaya wake ni kwamba
panapokuwa na migogoro hua hakuna tena mapenzi. Na pasipokuwa na mapenzi huwa
hapana tendo la ndoa. Maana kila mtu anakuwa hana mapenzi wala hana hamu na
mwenzake. Matokeo yake ni mwanandoa
kutoka nje na kutafuta kitulizo binafsi ili kukidhi haja yake ya kimaumbile.
Kwasababu haki ya kimaumbile ni kwa kila aliyekamilika. Na hakuna njia ya
kuiepuka zaidi ya kutimiza wajibu huo. Je? Uanataraji mwenzawako atatumia njia
gani kama wewe unaleta sokomoko ndani? (TAKE CARE)
6. Kukithiri kwa wanawake wanaovaa nusu uchi
Pointi hii haina tofauti sana na ile ya
utandawazi. Lakini hapa tunaitaja katika upande mmoja tu. Watu wamekuwa wakiiga
tabia za watu wa magharibi (wazungu) ambao kawaida yao ni kupingana sana na
maandiko ya uislamu hususan katika
mavazi, malezi n.k. wanapoiga tabia hizo za uvaaji inakuwa ni zaidi ya nusu
uchi. Hapo ndipo wanakuja kutokea watu wanaojiuza miili yao kwa njia isiyo ya
moja kwa moja. Utamkuta mwanamke anavaa
mavazi ya kutamanisha hatimaye mwanaume hata kama alikuwa hana nia ya kumtongoza
atamtongoza tu ili atembee naye kwa sababu huenda aliona kitu kinachomfurahisha
ambacho laiti angejisitiri kisingeonekana. Pia asilimia nyingi ya wanawake
wanaovaa ovyo hua wakitongozwa hawakatai. (LAKINI USIJE UKAJARIBU MZEE)
7. Tamaa
Kutaka kupata kwa haraka kitu ambacho huna
uwezo nacho, kutaka kujilinganisha na levo ambazo sio zako, hiyo tunaita tamaa.
Kuna msanii mmoja wa bongo fleva
alisema “tamaa
ya moyo inaweza kukuweka mashakani” mashaka aliyoyakusudia hapa miongoni
mwayo ni kuzama katika dimbwi la mapenzi. Msichana unatamani
pesa nawe huna lazima utataka kuzitafuta kwa
njia yoyote. Na njia nyepesi ni kuhongwa na anaekuhonga mwisho wa siku atataka
kufanya mapenzi na wewe. Hapo utajikuta unaangukia katika dimbwi la zinaa. (AU
NADANGANYA?)
MADHARA YA ZINAA KATIKA JAMII
1. Kupoteza fedha
Asiyejuwa kuwa zinaa ni gharama anyooshe kidole
juu. (nadhani wote mnajua). Fedha nyingi hutumika ili kukamilisha zoezi hili
kufanikiwa. Ukizingatia kwanza zoezi hili kwakuwa si halali mara nyingi
washiriki hupenda kujificha ili wasionekane na jamii iliyowazunguuka. Hivyo
hutumia gharama nyingi zikiwemo usafiri
labda kama wanataka kutoka nje ya mji wao, chakula chao ili wapate nguvu
ya kwenda kumuasi Mungu, zana kama kondomu n.k. pia washiriki ili kudumisha
penzi lao baada ya kumaliza ni lazima wapongezane kwa kupeana pesa. Hizi zote ni gharama laiti kama mtu angeamua
kukaa yote hayo yasingali jitokeza na pesa ile angeitumia kwa matumizi mwngine
ya halali kabisa.
2. Maradhi
Ukitaja moja kwa moja maradhi makuu
yanayosababishwa na zinaa ni UKIMWI. Hili halina kificho. Dunia yetu imechafuka
sana, watu wengi sana wameathirika na maradhi haya ya uzinzi. Yapo pia maradhi
mengine kama GONORHEA, KISONONO, U T I na maradhi mengine mengi zaidi.
Lakini pia na zinaa yenyewe pia ni maradhi kwa
sababu ukiizoea kuacha ni vigumu sana, kama mfano wa sigara au pombe. (EE MUNGU
TUNUSURU)
3. Kupoteza amani ya maisha
Hujawahi kuona mtu anatembea na mke wa mtu na
mwenyewe ameshaanza kumhisi? Je unafikiri yule bwana atakuwa na raha gani
katika maisha? Yeye atakuwa hata akitembea njiani hana amani. Akimuona mtu fulani
au rafiki wa mtu huyo anajificha au kubadili njia. Pia kwa wale wanao fanya
mapenzi na watoto wa watu pindi wazazi wao wanapogundua inakuwa shida sana kwa
watu hao kuishi mtaani kwa amani. Maana anajua muda wowote anaweza kupata janga
lolote kutoka kwa mahasimu wake. Pia kuna wale jamaa zangu wanaorapua watoto wa
shule hao ndio wana hatari zaidi. Anajua muda wowote miaka 30 itamuwajibikia.
(USIOMBE YAKUKUTE)
4. Kifo
Baadhi ya vifo vya binadamu vimetokana na
zinaa. Hii ni pale mtu anaposalitiwa na mpenz wake na kukosa maamuzi sahihi
hatimae kuamua kunywa sumu au kujinyonga. Pia vifo vinaweza kutokana na kuuwana
kwa wivu wa mapenzi mtu kuchukua mke au mume wa mtu. Pia vifo huja pale mtu
anapoamua kutoa mimba ya kiumbe kile, pale inaisabika moja kwa moja kuwa ameuwa
na pia yeye mwenyewe anaweza kupoteza maisha. Hii haina haja ya kuielezea sana
nafikiri inajulikana.
5. Mimba zisizo kusudiwa
Leo ukienda kliniki utawakuta wasichana weeengi
wakiwa wajawazito. Lakini hebu fanya upekuzi wa mimba hizo kwa kina, utagundua
karibu asilimia 50 ya wajawazito hao hawakukusudia kupata mimba hizo na pia sio
mimba za ndani ya ndoa ni mimba zilizo tokana na zinaa. Kwahiyo wanajikuta
katika msukumo ambao hawakuutarajia (yaani kulea mimba & mototo)
6. Ndoa zisizo kusudiwa
Umewahi kusikia ndoa ya mkeka? Basi kama
hujawahi kusikia hii ni ndoa ambayo anaozeshwa mtu kwa nguvu kutokana na
kufumaniwa na mtoto wa mtu. Sasa kibaya zaidi huenda alikuwa mwenyewe
anachakachua tu lakini hakumpenda mwanamke/mwanaume yule, sasa ndo hapo unapata
ndoa zisizotarajiwa. Na mara nyingi ndoa hizi hazidumu na hata zikidumu
haziishi malumbano.
LABDA MUNGU MWENYEWE ALETE MAPENZI BAINA YA WAWILI HAO. (Kwakweli pana
mazingatio sana katika hili)
7. Umasikini
Umasikini ni matokeo ya mwisho mwisho kabisa ya
zinaa, kama ndio unaanza huenda usilione jambo hili. Lakini umasikini unaweza
ukaja ukauona pale ambapo utajiwa na fahamu sasa. Wakati huo umeshapoteza mali
na pesa nyingi kwa ajili ya wanawake na wote walisha kukimbia. Ama ndio
umeshapata maradhi na unaugua peke yako. Michongo yako ya pesa yote
imeshakatika. Ama tena ulipigwa na kujeruhiwa na kupoteza baadhi ya viungo.
Hapo ndo utajua umasikini unaosababishwa na zinaa. (YAA RABBI TUEPUSHE NA JANGA
HILI)
8. Kuvunjika kwa ndoa
Zinaa ndani ya ndoa ni sababu kubwa sana
inayoweza kusababisha kuvunjika kwa ndoa. Mtu hatoweza kuvumilia kumuona
mwenzie anamsaliti kila mara. Na matokeo yake ataamua kumuepuka mume/mke huyo
ili kupisha wengine waendelee na jambo lao. Kwa hiyo si vizuri kumuumiza moyo
mwenzi wako kwa mambo ya kijinga kama hayo.
9. Kukithiri kwa watoto wa mitaani
Tunapozungumzia watoto wa mitaani tunamaanisha
wale watoto ambao wapo mitaani na hawana malezi ya kutosha toka kwa wazazi wao.
Ingawa si wote wametokana na zinaa lakini wengi wao chanzo chao ni zinaa na
hatimaye hawawajui wazazi wao. Kwakweli inasikitisha sana.
10.
Kupoteza
haiba
Haiba ni muonekano mzuri wa mtu kwa watu
wengine. Mtume wetu amesema kuwa mzinifu anakuwa ni mtu ambaye hana aibu hata
kidogo. Kwahiyo mtu wa aina hiyo kutokana na kutokuwa na aibu pia hatokuwa na
staha na watu wengine. Hiyo inaweza kumfanya akawa ni mtu mwenye kuvunja
heshima za watu na pia naye anakuwa ni mtu mwenye kuvunjiwa heshima yake. Pia
kwa kuongezea ni kwamba zinaa inaondoa nuru ya uso. Nuru ya usoni hupewa waja
wema ambao wameshikamana na ibada za Mungu. Lakini kwa mtu mzinifu inakuwa ni
kinyume chake. Automatically anakuwa ni mtu mwenye kudharauliwa. (FANYA
UCHUNGUZI JUU YA HILI UTAAMINI NINACHOKISEMA)
11.
Msongo
wa mawazo
Hapa ni pale ambapo mambo yamekwenda ndivo
sivo. Hapa ndo utajuwa nini maana ya msongo wa mawazo. Ni hii ni pale ambapo
umeshawahi kukutana na baadhi ya madhara ambayo ambayo tumekwisha kuyataja hai
awali.
NJIA ZA KUEPUKA ZINAA
Kwa ufupi. Ili uweze kuepuka kitu ni lazima
kwanza ujue chanzo chake, pia ujue na madhara yake. Ili uweze kujua jinsi ya
kuepuka vitu hivo. Kwahiyo hapa tutapeana kiasi tu lakini kama utafuatilia
vyanzo hapo nyuma wala hautakuwa na haja ya kusoma kipengele hiki.
1. Kushika mafundisho ya dini
Hakuna haja ya kunyumbua sana hoja hii. Nadhani
iko wazi kwa sababu dini imeweka wazi kila kitu. Imekataza jambo na kuamrisha
jambo kwahiyo ni kujitahidi kushika mafundisho ya dini.
2. Kuushinda moyo katika mambo maovu
Mara nyingi moyo wa binadamu huamrisha mambo
mabaya. Na kuukataza kutkufanya ni kazi kubwa sana. Lakini hatuna budi
kupingana na matakwa mabaya ya nafsi zetu. Hili ni jambo zito sana lakini
ukijitahidi unaweza tu kwa uwezo wa Mwenyezimungu. (WANGAPI WALIWEZA BWANA?)
3. Kuwa na subira
Subira ni mlango mpana sana. Lakini yenyewe
imegawanyika katika mambo mawili tu.
a.
Kusubiri katika kufanya mambo mema
Kusubiri katika kufanya mambo mema ni
kuvumialia katika ugumu wake na kudumu nayo mpaka kufa kwako. Pia kufanya kwa
nia thabiti na kutaraji malipo kwa Mungu
b.
Kusubiri katika kuacha maasi
Maasi yamepambwa katika sura nzuri. Lakini
inatakiwa kwa muumizi kujiepusha nayo ijapo kuwa ni mazuri kwa nje. Na
inatakiwa kufanya hivi kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezimungu.
4. Kumuomba Mungu akusaidie katika mambo ya kheri.
Tunatakiwa kudumu na dua. Kumuomba
Mwenyezimungu atudumishe na heri na atuepushe na shari. AAMIN.
MWISHO
COMMENTS