TUNAMKUMBUKA (UTENZI)

UMMAR BIN MOHAMED MAHAMBA.


TWAMKUMBUKA DAIMA
SHEKHE WETUALO MWEMA
MZEE MWENYE HEKIMA
UMAR BIN MAHAMBA

NAANDIKA NIKILIA
CHOZI LANIMWAGIKIA
BADO TWAKUFIKIRIA
UMAR BIN MAHAMBA

UNDANI SIKUFAHAMU
NI KUBWA YAKO ELIMU
KWANGU ZAIDI YA MWALIMU
UMAR BIN MAHAMBA


 NILIPOKUWA LA SABA
ALISEMA WANGU BABA
NISOME KWAKO KWA HUBA
UMAR BIN MAHAMBA

NIKAHAMA KWAKO RASMI
KUIPATA YAKO ILMI
NAWE UKAWA NA MIMI
UMAR BIN MAHAMBA


 MADRASA ILIJAA
MPAKA NILISHANGAA
TULIFATA YAKO TWAA
UMAR BIN MAHAMBA

JAPO SIKUDUMU SANA
MAMBO KUINGILIANA
NILIPATA MENGI SANA
UMAR BIN MAHAMBA


 SIKUFIKIA KIKOMO
KWA SABABU YA MASOMO
NA MWAKO NIKAWA NIMO
UMAR BIN MAHAMBA

MASOMO YA SEKONDARI
YALIFANYA NISAFIRI
ILA UKANISUBIRI
UMAR BIN MAHAMBA

LIKIZO IKIWADIA
NARUDI KUJISOMEA
NAWE UNANIPOKEA
UMAR BIN MAHAMBA

KIDATO NILIHITIMU
NIKAREJEA KWA HAMU
NAWE HUKU NILAUMU
UMAR BIN MAHAMBA

NIKARUDI MASOMONI
UKAFURAHI MOYONI
TUKAISOGEZA DINI
UMAR BIN MAHAMBA

ULIPOKUJA RIDHIKA
KUONA NIMESHAFIKA
CHEO UKANIPACHIKA
UMAR BIN MAHAMBA

KUSIMAMIA WENZANGU
UKAWA BENETI KWANGU
DARASA IKAWA YANGU
UMAR BIN MAHAMBA

DARASA ILINAWIRI
WATOTO WALIKITHIRI
KWANGU UKAJIFAKHIRI
UMAR BIN MAHAMBA

SHEKHE HUKUA KIBURI
HUKUCHOKA ZETU SHARI
NA MENGI KUTUSHAURI
UMAR BIN MAHAMBA

MAISHA LIENDELEA
VYOTE SITOELEZEA
NAELEZA BAADHIA
UMAR BIN MAHAMBA

ALIPOTAKA KARIMA
KUTUONDA SISI UMMA
MARADHI KUKUEGAMA
UMAR BIN MAHAMBA

MARADHI YALISHAMIRI
SHEKHE KWELI ULIKIRI
WAKAJA MADAKITARI
UMAR BIN MAHAMBA

UGONJWA UKAKUSHIKA
WATU WALIHANGAIKA
MWISHOWE UKATUTOKA
UMAR BIN MAHAMBA


 UMETUACHA YATIMA
TUNALIA KWA HURUMA
NANI KWAKE TUTASOMA
UMAR BIN MAHAMBA

TAREHE KUMI NA TISA
JANUARI MWEZI HASA
RASMI TULIKUKOSA
UMAR BIN MAHAMBA

TWAWAZA KILA KUKICHA
HUZUNI TWASHINDWA FICHA
MZEE UMETUACHA
UMAR BIN MAHAMBA

MAMA ZETU WANALIA
MACHOZI MEWAISHIA
MAJONZI MEWAACHIA
UMAR BIN MAHAMBA

 UMEMUACHA NA NANI?
SAMARUMBI MLIMANI
PEKE ATAFANYA NINI?
UMAR BIN MAHAMBA


 UMEMUACHA NA NANI?
MKARAMO YA PANGANI
SAMFYOMI MASKINI
UMARI BIN MAHAMBA

RAFIKI ZAKO VIPENZI
WA ENZI TANGU NA ENZI
WAKULILIA MACHOZI
UMAR BIN MAHAMBA

ADAMU IDI BICHUKA
NAE ANAKUKUMBUKA
KILIO KIMEMFIKA
MUNGU AKULAZE PEMA

ALIIMBA KWENYE DUFU
BWANA  HUYU MAARUFU
KIFO HAKINA HARUFU
MUNGU AKULAZE PEMA

NA WALA HAKINUKII
NA SAUTI HUSIKII
WALIKUFA MANABII
MUNGU AKULAZE PEMA

UMETUACHA MZEE
TUTAFANYA NINI SIE
MUNGU ATUTANGULIE
MUNGU AKULAZE PEMA

NALIA NIKIKUWAZA
NINASHINDWA KUJIKAZA
NANI ATANILIWAZA?
MUNGU AKULAZE PEMA

WANAO WANANILIZA
NIWAONAPO HUWAZA
UMEWACHA KWENYE KIZA
MUNGU AKULAZE PEMA

MAJONZI YASO KIKOMO
YAMETANDA MKARAMO
KWELI LEO SHEKHE HUMO?
MUNGU AKULAZE PEMA

MUNGU AKULIPE WEMA
PEPO ILIYO ADHWIMA
HAKIKA WEWE NI MWEMA
MUNGU AKULAZE PEMA

SISEME SANA JAMANI
NI KADARI YA MANANI
TUNAPITA DUNIANI
SOTE TUTAELEKEA

YA ALLA TUPE SUBIRA
ILI TUPATE UJIRA
TUSIJE PATA HASARA
SOTE TUTAELEKEA

HAKUNA ATAEBAKI
HAKIKA HII NI HAKI
SOTE TUTAIDIRIKI
SOTE TUTAELEKEA

MUUNGU UWALAZE PEMA
WALOTUTOKA MAPEMA
NA SISI TULIO NYUMA
SOTE TUTAELEKEA

TUNAMSHUKURU MUNGU
MUUMBA WATU NA MBINGU
MWISHO WA UTENZI WANGU
ATUSAMEHE MAKOSA.



Mtunzi: SAIDI R. BUNDUKI

Tar 31.03.2018 Jumamosi.
Saa 8 -  saa 10 jioni.



Hii ni historia fupi ya MIMI kuingia madrasatil maawa kwa Sheikh Ummar M. Mahamba (Mungu amuweke pema)

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: TUNAMKUMBUKA (UTENZI)
TUNAMKUMBUKA (UTENZI)
UMMAR BIN MOHAMED MAHAMBA.
https://1.bp.blogspot.com/-mllH4aKmg7Q/XvSDpAAon8I/AAAAAAAAVCA/NhZVUTTugTYg8K06nErygtwR2vv7XsjwQCK4BGAsYHg/w256-h181/SHAIRI%2B2.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-mllH4aKmg7Q/XvSDpAAon8I/AAAAAAAAVCA/NhZVUTTugTYg8K06nErygtwR2vv7XsjwQCK4BGAsYHg/s72-w256-c-h181/SHAIRI%2B2.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/04/normal-0-false-false-false-en-us-x-none_13.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/04/normal-0-false-false-false-en-us-x-none_13.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content