Ushairi ni
kipaji, si kila mtu aweza
Kutoka kwa
muumbaji, wachache amewajuza
Sio kama
kunywa maji, au matonge kumeza
Ushairi ni
kipaji, ijapo unasomewa
Ushairi ni
kipaji, sio kitu cha kubeza
Cha kwanza
ni upangaji, wa vina vya kuliwaza
Na
ufuatiliaji, wa beti kufananiza
Ushairi ni
kipaji, ijapo unasomewa
Ushairi ni
kipaji, japo waweza jifunza
Lakini wapo
magwiji, elimu kwake ni kiza
Kwa tungo
za kufariji, na nyingine za kuliza
Ushairi ni
kipaji, ijapo unasomewa
Ushairi ni
kipaji, mimi nilijiuliza
Mbona kuna
watungaji, shule hawajamaliza?
Unaweza
kumjaji, ukawa umepoteza
Ushairi ni
kipaji, ijapo unasomewa
Ushairi ni
kipaji, masomo kama nyongeza
Kumpamba
mtungaji, viungo kukorombweza
Kumvuta
msomaji, asome na kuteleza
Ushairi ni
kipaji, ijapo unasomewa
Ushairi ni
kipaji, za moyoni naeleza
Na abishe
m’bishaji, mimi nitajituliza
Sio
ubabaishaji, na tungo zilizo viza
Ushairi ni
kipaji, ijapo unasomewa
Ushairi ni
kipaji, hebu rafiki chunguza
Na wala
haihitaji, bongo nyingi kuumiza
Ngawa mi
mropokaji, chunguza kisha nijuza
Ushairi ni
kipaji, ijapo unasomewa
Ushairi ni
kipaji, ila mimi ni kilaza
Mimi
muungaungaji, bado najikaza kaza
Mekusudia
magwiji, kama we nojiuliza
Ushairi ni
kipaji, ijapo unasomewa
Sayyid R Bunduki.
COMMENTS