ADABU ZA KUSOMA QUR AN

Imepokelewa riwaya kutoka kwa Mohammad bin Fudhail kutoka kwa Abil Hassan (a.s) amesema: Nilimuuliza: Ninasoma msahafu (qur'...Imepokelewa riwaya kutoka kwa Mohammad bin Fudhail kutoka kwa Abil Hassan (a.s) amesema: Nilimuuliza: Ninasoma msahafu (qur'ani) kisha ninabanwa na mkojo nikasimama nikakojoa na kustanji na kuosha mikono yangu na kurudi kusoma msahafu huo? Akasema: Hapana mpaka utawadhe kwa ajili ya sala.

Na katika kitabu Al-khiswaal imepokelewa kwa sanadi na upokezi wake kutoka kwa Ali (a.s) -katika hadithi ya mia nne- amesema: Asisome mmoja wenu Qur'ani ikiwa hayuko kwenye twahara mpaka ajitwaharishe.

Na imepkelewa kutoka kwa Ahmad bin Fahd katika kitabu (Uddatud-daiy) amesema: Amesema (a.s): Mwenye kusoma Qur'ani hali ya kuwa amesimama kwenye sala, anayo mema mia moja kwa kila herufi aisomayo, na akiisoma kwa kukaa anayo mema khamsini, na akiisoma hali ya kuwa ni mwenye twahara na akiwa kwenye sala, anayo mema ishirini na tano (25), na ikiwa kama hakuwa ni mwenye twahara atapata mema kumi (10), ama mimi sisemi ya kuwa (Alif laam miim) ni kumi, bali ninasema Alif ni kumi, na laam ni kumi, na miim ni kumi, na Ree ni kumi).

Na imepokelewa kutoka kwa Hassan bin Ali Al-askariy (a.s) katika tafsir yake amesema: Ama kauli yake ambayo alikuitia na kukuhimiza kuitekeleza na akakuamuru kuitekeleza wakati wa kusoma Qur'ani ni, Audhu billahis samiul aliim minash-shaitwanir rajiim, hakika Amirul muuminiin (a.s) amesema ya kwamba: Kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo (Audhu billahi, yaani ninajizuilia na kujikinga kwa Mwenyezi Mungu-hadi akasema- na istiiadha ni kule kuamuru Mwenyezi Mungu waja wake wakati au pindi wanapo taka kusoka Qur'ani pale aliposema:

Na pindi utakapo taka kusoma Qur'ani basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani alie laaniwa), na mwenye kufuata adabu ya Mwenyezi Mungu atampeleka na kumfikisha kwenye mafanikio ya milele na milele, kisha akataja hadithi ndefu kutoka kwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema kwenye hadithi hiyo: Ukitaka usipatwe na sharri yao (mashetani) na usipatwe au kufikwa na vitimbi vyao, basi sema unapo amka asubuhi: Audhu billahi minash-shaytwanir rajiim, hakika Mwenyezi Mungu atakulinda na kukukinga na sharri zao.

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: ADABU ZA KUSOMA QUR AN
ADABU ZA KUSOMA QUR AN
https://1.bp.blogspot.com/-VQuioENbsCc/XSSUzHikJ9I/AAAAAAAAHmU/8Hhd-8fLQpcX75E7D9gdcvDRdNahtO1XwCLcBGAs/s400/quran-b.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-VQuioENbsCc/XSSUzHikJ9I/AAAAAAAAHmU/8Hhd-8fLQpcX75E7D9gdcvDRdNahtO1XwCLcBGAs/s72-c/quran-b.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/05/adabu-za-kusoma-qur-an.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/05/adabu-za-kusoma-qur-an.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content