Hukumu ya mwenye kuacha Kufunga Ramadhani.

HUKUMU YA MWENYE KUACHA KUFUNGA MWEZI WA RAMADHANI Kuacha Swawm kwa makusudi ni aina mbili: 1. Kuchukulia Swawm si nguzo ya Uislamu: ...

HUKUMU YA MWENYE KUACHA KUFUNGA MWEZI WA RAMADHANI

Kuacha Swawm kwa makusudi ni aina mbili:

1. Kuchukulia Swawm si nguzo ya Uislamu:

Ikiwa ni hivyo jambo hilo litamtoa mtu katika Uislamu na kuwa kafiri.

2. Kwa sababu ya udhaifu wake mwenyewe (kwa kutambua kuwa hiyo ni nguzo):

Kufanya hivyo ni dhambi kwake. Hapa duniani hapana adhabu maalumu atakayopatiwa isipokuwa ikiwa ipo dola ya Kiislamu naye anakula hadharani Qadhi atamtia adabu anayoona inafaa ili na wengine wasiwe ni wenye kumuiga katika maasiya hayo. Lakini Siku ya Qiyaamah ataadhibiwa vilivyo na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).  

Jambo linalotakiwa ni ni mtu au watu kuzungumza naye na kumueleza katika njia nzuri na ya sawa ili arudi katika misimamo ya kidini.

KiShariy’ah huyu mtu anatakiwa alipe kila siku aliyokula. Pia anatakiwa atubie, atake maghfirah kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  tawbah ya kikweli kweli pamoja na kujuta na awe na azma ya kutorudia tena kosa hilo. Na anatakiwa ajitahidi kufanya amali za kheri nyingi ili mabaya yake yabadilishwe kuwa mema. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Anasema:

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يُبَدِّلُ اللَّـهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٧٠﴾

Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda ‘amali njema; basi hao Allaah Atawabadilishia maovu yao kuwa mema.  Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu.  

وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللَّـهِ مَتَابًا ﴿٧١﴾
Na atakayetubu na akatenda mema, basi hakika yeye anatubia kwa Allaah tawbah ya kweli.  [Al-Fuqaan: 70-71]


Lakini kwa yule ambaye hatatubia mpaka inafika wakati wa kukata roho basi hapo haitamsaidia kurudi na kutaka maghfirah. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema: وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّىٰ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّي تُبْتُ الْآنَ وَلَا الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا أَلِيمًا ﴿١٨﴾ 
Lakini tawbah si kwa wale wanaofanya maovu mpaka mauti yanapohudhuria kwa mmoja wao husema: “Hakika mimi sasa nimetubu.” Na wala wale wanaokufa na hali wao ni makafiri. Hao Tumewaandalia adhabu iumizayo. [An-Nisaa: 18]

Na Allaah Anajua zaidiImenakiliwa na bunduki.com
kutoka katika vyanzo vinavyoaminika.


COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: Hukumu ya mwenye kuacha Kufunga Ramadhani.
Hukumu ya mwenye kuacha Kufunga Ramadhani.
https://3.bp.blogspot.com/-cMby8UWaDdY/WwQlK4kCuvI/AAAAAAAAChQ/U2vvnXUhlIAz5zNnjIAyl703JpFn4WrEwCLcBGAs/s400/91302b89b622be45213a65f1d51a3310.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-cMby8UWaDdY/WwQlK4kCuvI/AAAAAAAAChQ/U2vvnXUhlIAz5zNnjIAyl703JpFn4WrEwCLcBGAs/s72-c/91302b89b622be45213a65f1d51a3310.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/05/blog-post_22.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/05/blog-post_22.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content