Fadhila za kusoma QUR AN

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM MWENYE KUSIKILIZA QUR'ANI  Imepokelewa kutoka kwa Mohammad bin bashiir [1] kutoka kwa Ali bi...

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

MWENYE KUSIKILIZA QUR'ANI 
Imepokelewa kutoka kwa Mohammad bin bashiir [1] kutoka kwa Ali bin Hussen (a.s) na ameipokea hadithi hii kutoka kwa Abi Abdillah (a.s) amesema: Mwenye kusikiliza herufi moja ya kitabu cha Mwenyezi Mungu bila ya kusoma, Mwenyezi Mungu humuandikia jema moja na kumfutia kosa moja na kuinuliwa daraja moja, na mwenye kusoma kwa kuangalia bila ya kusali Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi jema moja na kumfutia kosa moja na huinuliwa daraja moja, na mwenye kujifunza herufi moja ya dhahiri ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humuandikia mema kumi na kumfutia makosa kumi na kuinuliwa daraja kumi, akasema:

Sisemi kwa kila aya lakini kwa kila herufi sawa iwe baa au faa au mfano wa hizo, akasema: Na mwenye kusoma herufi moja hali ya kuwa amekaa kwenye sala, Mwenyezi Mungu humuandikia kwa kila herufi hiyo mema khamsini, na kumfutia makosa khamsini, na kumuinua daraja khamsini, na mwenye kusoma herufi moja hali ya kuwa amesimama kwenye sala yake, Mwenyezi Mungu humuandikia mema mia moja na kumfutia makosa mia moja na kumuinua daraja mia moja, na mwenye kuihitimisha, maombi yake ni yenye kukubaliwa, sawa yachelewe au yawahi akasema: Nikasema: Niwe fidia yako mwenye kuihitimisha yote? Akasema: Mwenye kuihitimisha yote.[2]

Na imepokelewa kutoka kwa Is'haq bin Ammar, kutoka kwa Abi Abdillah (a.s) amesema: Mwenye kusoma aya mia moja akisali kwa kisomo hicho kwa usiku mmoja Mwenyezi Mungu humuandikia kwa aya hizo kunuti za usiku na mwenye kusoma aya mia mbili tofauti na kwenye sala ya usiku Mwenyezi Mungu humuandikia kwenye lauhul mahfuudh mema yaliyo sawa na mali nyingi (qintwaar ) na qintwar ni kinaya ya mali nyingi, aukia miamoja, na awqiyah ni kubwa zaidi ya mlima wa Uhudi.[3]

Na imepokelewa kutoka kwa Anas amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w): Mwenye kusoma aya mia moja, hataandikwa miongoni mwa wenye kughafilika, na mwenye kusoma aya mia mbili huandikwa miongoni mwa wenye kunyenyekea na watiifu, na mwenye kusoma aya mia tatu Qur'ani haitamtolea hoja, yaani mwenye kuhifadhi kiwango hicho cha aya za Qur'ani, husemwa: Hakika mtoto amesoma Qur'ani: Kwa maana amehifadhi.[4]imenakiliwa na sayyidbunduki.blogspot.com

kutoka katika vyanzo vinavyoaminika

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: Fadhila za kusoma QUR AN
Fadhila za kusoma QUR AN
https://4.bp.blogspot.com/-DbOJAJmqhQ0/Ww_d8shUn1I/AAAAAAAACjU/AxjNvtumLpg4bHkcJm_uP3goLtDxk1-IgCLcBGAs/s400/quran-image.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-DbOJAJmqhQ0/Ww_d8shUn1I/AAAAAAAACjU/AxjNvtumLpg4bHkcJm_uP3goLtDxk1-IgCLcBGAs/s72-c/quran-image.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/05/fadhila-za-kusoma-qur-an.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/05/fadhila-za-kusoma-qur-an.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content