MKALAMO (PART 1)

Mkalamo yavutia, kwa kadhaa vivutio
Vichache takutajia, litege lako sikio
Kwanza mji umekua, wamepita wapitao
Naipenda Mkalamo, Mungu ameibariki


Mandari za kubarizi, kusepa hutotamani
Kama mto MSANGAZI, kigong’ondo Ufingoni
Japo kwenye kiangazi, maji hakuna mtoni
Naipenda Mkalamo, Mungu ameibariki

Maji yaliyotuwaa, mabwawa maji baridi
Kama vile muangaa, Kwembosha kwa musabedi
Watu hunywa na kufua, kunywesha hawana budi
Naipenda Mkalamo, Mungu ameibariki

Imepita kati reli, usafirishaji mwema
Kwa treni na toroli, Tanga to Darisalama
Huzisafirisha mali, salmini na salama
Naipenda Mkalamo, Mungu ameibariki

Mashamba ya kupendeza, ya miembe na minazi
Muhunguru hadi boza, tizama neema hizi
Macho yako huliwaza, uendapo matembezi
Naipenda Mkalamo, Mungu ameibariki

Umeme ni wera wera, mataa kila sehemu
Sehemu za biashara, zinapendeza kaumu
Mtihani bara bara, ndo kidogo nalaumu
Naipenda Mkalamo, Mungu ameibariki

Mitaa yake minono, kwa tamu zake lahaja
Tongani hadi chamwino, sisahau Mtakuja
Sokoni hasa ndo mno, kwa bwana Mitumba ROJA
Naipenda Mkalamo, Mungu ameibariki

Kuna kabila kadhaa, zilizopo kwenye chati
Wazigua ndio taa, ndo wenyeji wenye hati
Wagogo na wasambaa, sasa wapo wamang’ati
Kijiji kinavutia, ukifika utapenda

Viko vingi vidokezo, viwanja vya kujidai
Kwenye game na michezo, ni mtini na kindii
Watu huonesha uwezo, BUSHI dafu hawafui
Kijiji kinavutia, ukifika utapenda

Usafiri abiria, wa kudumu si mapito
Mkata ukitokea, utakuja na KIDATO
Pangani kielekea, utauvuka na mto
Kijiji kinavutia, ukifika utapenda

Karibu wangu JIRANI, nyumbani karibu sana
Ndugu zangu wa Sadani, Kwamsisi nawaona
Karibu wa Mikocheni, Mkwaja mpaka Bweni
Karibuni karibuni, sisi watu wakarimu

Ya mwisho kadi tamati, yanatosha nilosema
Naivaa yangu shati, hapa ndo mwisho nakoma
Pongezi zangu za dhati, kwako wewe ulo soma
Siku iwe njema kwako, iache yako coment.

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MKALAMO (PART 1)
MKALAMO (PART 1)
https://1.bp.blogspot.com/-mllH4aKmg7Q/XvSDpAAon8I/AAAAAAAAVCA/NhZVUTTugTYg8K06nErygtwR2vv7XsjwQCK4BGAsYHg/w256-h181/SHAIRI%2B2.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-mllH4aKmg7Q/XvSDpAAon8I/AAAAAAAAVCA/NhZVUTTugTYg8K06nErygtwR2vv7XsjwQCK4BGAsYHg/s72-w256-c-h181/SHAIRI%2B2.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/05/mkalamo-mkalamo-yavutia-kwa-kadhaa.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/05/mkalamo-mkalamo-yavutia-kwa-kadhaa.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content