MKALAMO (PART 2)

Nilitaka kusahau, kuzungumzia hili
Waliniomba wadau, Kina ticha STAMBULI
Nitasema angalau, namimi bila kujali
Nitaeleza kidogo, changamoto Mkalamo

Ngumu njia za riziki, asikudanganye mtu
Piga boda piki piki, ama kakate misitu
Ndo wengi wamediriki, kuhama miji ya watu
Hizi ndizo changamtoto, hapa kijijini kwetu

Si swala la masihara, tunasema liko wazi
Hakuna hapa ajira, wala fursa za kazi
Vijana tunazurura ,wengine wezi wa NAZI
Hizi ndizo changamtoto, hapa kijijini kwetu

Boda boda majiani, wanaipata shughuli
Mara “iweke pembeni”, mbona mebeba wawili
Sikwambii msituni, mejaa maliasili
Hizi ndizo changamtoto, hapa kijijini kwetu

Kitegemea kilimo, mvua shida kwakweli
Zinaishia ngurumo, na kunyesha huko mbali
Mwaka ukipata chumo, njaa yaja kwenye vuli
Hizi ndizo changamtoto, hapa kijijini kwetu

Ya zamani bado yapo, kwa visiki vya mpingo
Yanayoathiri pipo, kushushiana viwango
Yale ya papo kwa hapo, warogaji na mazongo
Hizi ndizo changamtoto, hapa kijijini kwetu

Vijana wanojituma, kutwa kupigwa hasadi
Wanawarudisha nyuma, makusudi makusudi
Wakikwona umekwama, raho zao zafaidi
Hizi ndizo changamoto, hapa kijijini kwetu

Wako wanosema sema, ukipita unaisha
Ukikonda una ngoma, ndio imekukondesha
Wakiona umehama, umekimbia maisha
Hizi ndizo changamtoto, hapa kijijini kwetu

Ishu Maadili mema, ni wachache siku hizi
Wamesema wamesema, bado hawasikilizi
Watoto watu wazima, ushenzi kisha ushenzi
Hizi ndizo changamtoto, hapa kijijini kwetu

Watoto shule kwa fimbo, wanaongoza kufeli
Huiga mambo ya ng'ambo, ya viduku na singeli
Ukimuuliza kimombo, iz iz ni muhali
Hizi ndizo changamtoto, hapa kijijini kwetu

Yanatosha nilosema, yaliyobaki navunga
Mule nilo kwama kwama, jua SIJUI KUTUNGA
Vina na sauti njema, nawaachia wahenga
Mimi bado ni mchanga, ndo mana sina fasihi

 JAMANI NDUGU ZANGU MIMI BADO MUANDISHI MCHANGA SANA
Naomba usiache kukosoa pale ambapo unaona kuna makosa.

Asante sana.

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MKALAMO (PART 2)
MKALAMO (PART 2)
https://1.bp.blogspot.com/-mllH4aKmg7Q/XvSDpAAon8I/AAAAAAAAVCA/NhZVUTTugTYg8K06nErygtwR2vv7XsjwQCK4BGAsYHg/w256-h181/SHAIRI%2B2.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-mllH4aKmg7Q/XvSDpAAon8I/AAAAAAAAVCA/NhZVUTTugTYg8K06nErygtwR2vv7XsjwQCK4BGAsYHg/s72-w256-c-h181/SHAIRI%2B2.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/05/mkalamo-sehemu-ya-2-changamoto-nilitaka.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/05/mkalamo-sehemu-ya-2-changamoto-nilitaka.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content