Nasaha kwa vijana

nasaha kwa vijana

Nasaha Kwa Vijana


Vijana wa Kiislamu! Mwezi wa Ramadhani umetuwadia, hatuna wakati mwengine tuutarajiao tena na kuutumaini katika kufuzu kwetu usio huu. Balaa zote za kutuletea maafa hapo kesho (Akhera) tuziepuke na tuwe mbali kabisa nazo.

Katika mwezi huu hakuna masingizio yoyote, ambayo tunaweza kujisingizia nayo kama vile kudai kwamba 'O'..... Shetani ametushika sana! Kwani Mtume (s.a.w.) ametudokezea kwamba, "Mwezi wa Ramadhani unapoingia, milango yote ya rehema huwa wazi (kuwapokea wanaotaka kuingia), milango yote ya Jahannam hufungwa na Mashetani wote hutiwa minyororo ili wasiwahangaishe."

Ajabu kubwa zaidi ni kijana wa Kiislamu kuvaa ushanga, mikufu na bangili namna wafanyavyo wanawake. Ni hadi lini watajisitahi na kuwa na haya juu ya haya wayafanyayo?
Ni aibu kubwa kwa vijana wa Kiislamu kuhalifu sheria za dini yao hasa katika mwezi huu. Kwa kila aliye na uchunguzi, atastaajabu sana kumwona mtu aliyekuwa mnyenyekevu mchana kutwa, msalihina, kubadili hali hiyo na kuufanya usiku kuwa sitara ili kumdumishia maasi yake.

Ikiwa hawatajinasihi katika muda huu wa rehma na maghfira wakumbuke kuwa wamo hatarini ya kupoteza imani.
Badala ya kuketi mabarazani kusengenyana na kufitiniana, tunahimizwa kuingia misikitini na kuendesha ibada mbali mbali na tukisome kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa wingi yaani Qur'ani. Kwani pasi na kufanya hivyo, tutakuwa tunaupoteza wakati wetu ambao ni wa thamani sana kama ilivyopokelewa katika kauli za wahenga wa kiarabu kwamba: 'Wakati ni kama upanga, usipouvunja, (mwishowe) utakukata.'

niwatakie week end njema na Ramadhani njemabunduki.com

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: Nasaha kwa vijana
Nasaha kwa vijana
nasaha kwa vijana
https://3.bp.blogspot.com/-AGsciM2EAYk/WwpvzXnsOwI/AAAAAAAACiM/1iCIDbCwXIosqEBseLb7vafKD0VbVrUVgCLcBGAs/s400/ramadhan_kareem_2014_by_madremedia-d7na62g.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-AGsciM2EAYk/WwpvzXnsOwI/AAAAAAAACiM/1iCIDbCwXIosqEBseLb7vafKD0VbVrUVgCLcBGAs/s72-c/ramadhan_kareem_2014_by_madremedia-d7na62g.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/05/nasaha-kwa-vijana.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/05/nasaha-kwa-vijana.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content