USIOMBE YAKUKUTE

Yowe langu kigong’ondo, sikia pwani na bara
Wasikie wa Kibondo, Lindi mpaka Mtwara
Wasikie walo kando, dimbwini na bara bara
Usiombe yakukute.

Kufumaniwa kwauma, sikilia kwa wenzio
Unaweza ukazima, kwa kupigwa na pumbao
Wengine hupigwa chuma, kupoteza utu wao
Usiombe yakukute.

Usiombe kuchawiwa, kwa sababu ya mapenzi
Mijidawa kuwekewa, unyunyu kwenye mchuzi
Wallahi utapagawa, kupelekwa kama mbuzi
Usiombe yakukute.

Usiombe ukaachwa, na yule unompenda
Hapo utaona kichwa, chawasha kama kidonda
Kila jua likikuchwa, wakichukia kitanda
Usiombe yakukute.

Kuoa uso mtaka, mke wa kulazimishwa
Ile ndoa ya mkeka, siku ulo furumushwa
Nafsi itakauka, kama papa lo kaushwa
Usiombe yakukute.

Kuibiwa ni kubaya, kile uno kithamini
Mda mrefu wagwaya, kukipata cha moyoni
Leo BOYA bila haya, kakitia mikononi
Usiomba yakukute.

Leo umetimamia, viungo vyote mwilini
Kwa madaha watembea, kujivuna majiani
Usiombe kuumia, kupoteza vya mwilini
Usiombe yakukute.

Ulikuwa una hela, wala wavaa wadunda
Masikini kwako fala, chapa fimbo kama punda
Kuamka na kulala, wazikuta zishakwenda
Usiombe yakukute

Usiombe kupomoka, toka juu kuja chini
Utajiri kukutoka, kufata umasikini
Twaweza tukakuzika, usipokuwa makini
Usiombe yakukute.

Nakoma ninatoweka, yalikuwa ni maoni
Mekosa cha kuandika, hiki hiki chukueni
Nimechoka nyaka nyaka, natulia kivulini
Nawatakia siku njema.
                                                                      

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: USIOMBE YAKUKUTE
USIOMBE YAKUKUTE
https://1.bp.blogspot.com/-BXVq3GnXdbE/XvSJVXOLPjI/AAAAAAAAVGY/2Je1NDNMW9EsEjG-W8NzEX7l9LUmIYubwCK4BGAsYHg/w256-h181/SHAIRI%2B2.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-BXVq3GnXdbE/XvSJVXOLPjI/AAAAAAAAVGY/2Je1NDNMW9EsEjG-W8NzEX7l9LUmIYubwCK4BGAsYHg/s72-w256-c-h181/SHAIRI%2B2.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/05/normal-0-false-false-false-en-us-x-none.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/05/normal-0-false-false-false-en-us-x-none.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content