MASHARTI YA SWAUM

Saumu Ni Wajibu Kwa Masharti Manane Mwenenyezi Mungu amesema: "Basi atakayekuwa katika mji (asiwe msafiri) katika mwezi huu afung...

Saumu Ni Wajibu Kwa Masharti Manane

Mwenenyezi Mungu amesema: "Basi atakayekuwa katika mji (asiwe msafiri) katika mwezi huu afunge". Qur'ani 2:185.
Wakati tunapojiandaa kwa kuianza Ramadhani, tunapaswa kujua kwamba, amri ya kufunga ni yake Mwenyezi Mungu. Na wala amri hii haikuwa ya yeyote yule kati ya viumbe. Muda huu wa Saumu mtu hutakiwa kufanya ibada kwa wingi. Kuomba, kusoma dua mbali mbali na kuomba maghfira.
Na masharti yafuatayo ukiwa umeyakamilisha utalazimika kuanza Saumu, na wala hutokuwa na udhuru wowote ukuzuiao kufunga.

1. Al-Islam: Uislamu ni shuruti moja katika shuruti za kukubaliwa Saumu na ibada zote. Ijapokuwa juu ya kafiri pia ni wajibu kufunga na kufanya ibada zote, lakini kwa vile yeye si Mwislamu basi haitasihi na kukubaliwa ibada zake.
Mwenyezi Mungu anaamrisha wasali lakini shuruti (watawadhe au watayammamu). Basi kafiri pia inampasa afunge, lakini shururti za kusihi hiyo saumu yake ni kukubali Islamu, na Kafiri anaweza kusilimu.

2. Baleghe: Ukiwa umebaleghe (mwanamume) kwa kutimiza miaka kumi na mitano na mwanamke kwa kutimiza miaka tisa; au ukiwa wewe ni mwanamke aliyewahi kutokwa na damu ya mwezi, au ukiwa umewahi kuota ndoto kama unatangamana na mke (ukiwa mume) au na mume (ukiwa mke) na kutokwa na manii kwa ndoto hiyo, utalazimika kuanza kufunga.

3. Nia: Ni makusudio ya kutenda, nayo ni fardhi kwa kila ibada na ni sharti katika ibada zote. Lazima kunuia kujizuia na kila kinachobatilisha Saumu, na si lazima wakati wa nia kuzikumbuka zote kwa jina, inatosha kuweka nia ya kujitenga na kila kinacho haribu na kubatilisha Saumu.
Kuweka nia ni wajib. Ikiwa kwa mfano, siku moja kabla ya kuingia Ramadhani mtu bila ya nia ya kufunga akalala na asizindukane ila baada ya magharibi ya usiku wa pili wa mwezi wa Ramadhani, basi kukosa kula na kunywa siku hiyo moja ya Ramadhani bila ya nia haitasihi, na lazima baadaye ailipe.
Mtu anaweza kila usiku wa Ramadhani kuweka nia ya kufunga kesho yake, na ni vizuri usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani aweke nia ya mwezi mzima.

Wakati Wa Kuweka Nia

Wakati wa kuweka nia ya Saumu ni kutoka mwanzo wa usiku hadi adhana ya asubuhi (Alfajiri) kwa saumu za fardhi, ama saumu za sunna huanzia mwanzo wa usiku, hadi kiasi cha kunuia kumebaki kufikia magharibi, ikiwa mpaka wakati ule hakutenda kitu cha kuvunja saumu, basi hapo aweke nia ya saumu, na saumu itasihi.
Ikiwa mtu bila ya kuweka nia kabla ya Alfajiri akalala, na akaamka kabla ya adhuhuri na hapo akiweka nia, saumu yake itasihi, ikiwa saumu ya fardhi au ya sunna; lakini akizindukana baada ya adhuhuri, basi hapo hawezi kuweka nia ya saumu ya fardhi. Ikiwa kabla ya alfajiri kanuia na akalala na asiamke ila baada ya magharibi, saumu hiyo itasihi haidhuru neno.
Al-Khuluus
Lil-Laahi Ta'ala, maana yake, kufunga kwake iwe Lil-Laahi, Ta'ala tu, lau akiongeza Riya (kwa kujipendekeza) tu hapa saumu yake haitasihi.

4. Ukiwa (wewe mke) unayo damu ya mwezi au ya uzazi, unashauriwa kusubiri hadi itakapokoma ndipo uanze kufunga, hata hivyo utalazimika kuzilipia siku ambazo zimekupita.

5. Kwa aliye na kichaa na wazimu huyo anasamehewa Saumu zitakazompita muda wa udhuru wake huo.

6. Ukiwa umgonjwa hulazimiki kufunga hadi utakapopata nafuu, hata hivyo ni ugonjwa usiokuwezesha kufunga tu ndio unaokusudiwa kwa hapa, kama mtu mwenyewe anajihisi udhaifu, na kutovumilia Saumu atafuturu.

7. Ujue vile vile kwamba, msafiri (safari yenye umbali maalumu) si halali kwake kufunga hadi arudipo uwenyejini.

8. Pia kwa aliye na ugonjwa wa kifafa halazimiki kufunga na badala yake anaruhusiwa kula.

Hukumu ya Mzee

Mzee mkubwa, na kadhalika vikongwe wasio na uwezo wa kustahamilia Saumu, wanaruhusiwa na sheria wasifunge na watoe sadaka ya kibaba (sawa na kilo kasorobo) kwa kila siku. Kibaba hiki kiwe ni cha chakula kitumiwacho sana na watu wa sehemu hiyo, na pia hukumu hii humhusu mwanamke anayenyonyesha na aliye na mimba wakijichelea au kuchelea wana wao, wanaruhusiwa na sheria kufuturu.
Isipokuwa hawa wawili wa mwisho watalazimika kulipa nyudhuru zao zikiisha kabla ya Ramadhani nyengine kufika.
Msafiri asafiriye umbali wa Km. 48 halazimiki kufunga, bali atafuturu ingawa haambiwi ale bali atajizuia vivyo hivyo na kulipa baada ya Ramadhani kumalizika. Na safari, sharti iwe ya halali; pia isiwe kazi yake kama kondakta, dereva nahodha n.k. asiwe atakaa huko zaidi ya siku 10 akiwa atakaa zaidi ya siku 10 atafunga hata huko huko safarini.
Kafiri wa kuzaliwa akisilimu halazimiki kulipa Saumu zilizompita alipokuwa ukafirini. Kadhalika mtoto akibaleghe, na aliyekuwa na kicha (wazimu). Ama aliyepitiwa na Saumu kwa kuwa na hedhi, nifasi, ugonjwa,n.k. hulipa.

Pia Sala

Ili kuthibitisha utiifu wetu kwa Mwenyezi Mungu na ili Saumu zetu zikubaliwe, ni sharti tutekeleze amri zake zote pasina kuziacha zingine. Sala ni mojawapo wa mahimizo makubwa kwa Mwislamu na lau atajisumbua kwa kuumwa na njaa bure pasina kusali, ajuwe kuwa hana fungu lolote katika Saumu yake. Kwa hivyo tukiwa tunataka thawabu zaidi na zaidi ni lazima sala hata tusiziache.
Sala ni nguzo ya pili katika nguzo za Islamu, na tukumbuke kwamba, tukiwa na sala pungufu, hata mali zetu zi katika mafungu yasiyotakikana, na zikiwa kamili, hata ibada zinginezo zitakuwa makbuli Inshaallah.
MWENYEZIMUNGU NDIYE MWENYE KUJUA ZAIDI

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MASHARTI YA SWAUM
MASHARTI YA SWAUM
https://1.bp.blogspot.com/-GaqgSx4U9Gk/Wv16legbL3I/AAAAAAAACfc/q3HzMaiorZgzCQaisRcyz7MFsBDctYu4QCPcBGAYYCw/s400/ramadan-kareem-quotes.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-GaqgSx4U9Gk/Wv16legbL3I/AAAAAAAACfc/q3HzMaiorZgzCQaisRcyz7MFsBDctYu4QCPcBGAYYCw/s72-c/ramadan-kareem-quotes.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/05/saumu-ni-wajibu-kwa-masharti-manane.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/05/saumu-ni-wajibu-kwa-masharti-manane.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content