CHUNGA MAMBO HAYA

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA Tuchunge mazungumzo, tuwe na nidhamu ya kuzungumza mbele za watu Na Abdul Hamiid Ibn Badii Ni elimu na e...

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
Tuchunge mazungumzo, tuwe na nidhamu ya kuzungumza mbele za watu

Na Abdul Hamiid Ibn Badii

Ni elimu na elimu pekee inayoweza kuyaongoza maisha ya Muislamu kwa ujumla wake. Inamfahamisha na kumuelekeza njia ya imani, utaratibu wa kusema na kutenda. Hii inathibitika katika Qur’an:

“Wala usifuate (ukipita ukiyasema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa.” (17:36)

Tabia ya mtu katika maisha hunasibiana na akili kiasi kwamba kama akili inanyooka sawasawa, basi tabia yake nayo huwa hivyo hivyo. Kwani maneno na matendo yake si chochote bali ni mwagwi tu wa imani yake ambayo nayo ni matunda ya mchakato wa fikra anaoufikia kwa njia ya akili ya tafakuri na uchambuzi.

Na bila shaka, michakato ya fikra hutofautiana kwa viwango vya majazi na mapungufu. Katika kiwango cha juu ipo ilimu ambayo ndiyo njia ya kulifikia jambo kwa usahihi wake wa kufikiwa.

Katika kiwango cha pili, ipo dhana sahihi (valid assumption) ambayo ina maana ya kulitazama jambo kwa mtazamo yakinifu ambao kwao jambo hilo laweza kutafsiriwa.

Kisha wahm, uoni usio sahihi unakuja katika nafasi ya tatu ambayo ipo upande usioyakinika na uliopungukiwa mizani ya kupima mambo kwa usahihi wake.

Na mwisho, katika nafasi ya nne ipo shaka ambayo ni kulitazama jambo katika mitazamo miwili au zaidi inayolingana kiasi kwamba hakuna linaloonekana kulizidi jingine.

Ni dhahiri kuwa Wahm (uoni usio sahihi) na shakk (shaka) ni njia mbili za ilimu zisizoweza kutegemewa. Na kwa sababu udhaifu wa kimaumbile na pupa ya mwanadamu, wakati mwingine, humsukuma kutegemeza imani, kauli na matendo juu ya msingi wa maono yasiyo sahihi (delusions), shaka (doubts)au dhana potofu (invalid assumptions), basi mara nyingi hujikuta akipotea njia.

Mwenyezi Mungu anawaelekeza waja Wake kuwa wategemeze imani, kauli na matendo yao juu ya msingi imara wa elimu sahihi (genuine knowledge)

“Wala usifuate (ukipita ukiyasema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa.” (17:36)

Kwa kweli mara zote tuepuke mazingira ya kuamini bila kufanya tahakiki ya chochote kinachokatiza akilini mwetu. Badala yake, tunapaswa kujifunza namna ya kuyatafakari mambo kwa undani.

Na tunapopata elimu sahihi juu ya mambo hayo ndipo sasa tuyaamini. Kinyume chake, tuachane nayo pale yanapokuwa upande wa maono yasiyo sahihi na dhana potofu. Mtume, swallallahub alayhi wa sallam, amelizungumzia jambo hili: “Ni uongo kabisa anaousema mtu pale anaporudia-rudia kila jambo analolisikia.” (Muslim).

Isitoshe, kila inapotubidi kuzungumzia jambo fulani ambalo tuna elimu nalo kamili, lazima tufanye hivyo kwa kuzingatia kikamilifu mipaka ya kisheria ya Kiislamu ambayo inachunga na kuweka sawa nidhamu ya uzungumzaji mbele za watu, katika hadhira, na hata katika mazingira ya kupita njia.

Kisheria, tunapaswa kusema mambo kwa kuzingatia kiwango cha uelewa cha wale wanaotusikiliza, la sivyo, tutawatia mtihanini kama inavyosema Hadiyth hiyo.

Kufuata kanuni hiyo ndiko kutakakofanya imani yetu iwe sahihi, kauli zetu ziwe za kweli, na matendo yetu yawe sawasawa. Kwani, kwa hakika, matatizo tunayoyaona katika imani za watu, kauli na matendo yao si kingine bali ni matunda machachu ya kupuuza kwao kanuni hiyo ya msingi.

Hivyo, kwa kuzingatia Aya tuliyoinukuu hapo juu, tunakatazwa kukifuata kile ambacho hatuna elimu nacho, na pia tunaelekezwa kuhakikisha kuwa imani zetu zinakuwa sahihi, kauli zetu zinakuwa za kweli, na matendo yetu yanakuwa sahihi.

Kwa upande wa imani sahihi, ama iwe ni katika kuamini mambo ya dini au kuamini mambo ya ya dunia hii, hakuna ubaya kuzichunga, na vivyo hivyo kuyachunga matendo yetu katika mambo ya dini na ya dunia. Lakini pale linapokuja suala la kauli sahihi, suala hili lazima lizingatiwe. Kwani si kila jambo la kweli lazima lisemwe.

Mathalani, kasoro za kitabia za mtu zisisemwe hadharani wakati mwenyewe hayupo. Vinginevyo, tutakuwa tunamteta, na wala zisisemwe wakati mwenyewe akiwepo. La sivyo, tutaumiza hisia zake.

Wakati pekee wa kuzitaja kasoro hizo mbele ya muhusika ni pale zinapokuja kwa njia ya kumnasihi jambo ambalo shurti na adabu zake lazima zizingatiwe, kama vile kuepuka kumnasihi mtu mbele za watu.

Hebu sasa tuzungumzie baadhi ya mambo yanayohusiana na imani na matendo na hali za watu wanaohusika nayo.

Ø Mtu anayeamini jambo fulani ambalo hana elimu nalo sahihi, akalitenda na kulisema kwa msingi huo wa kutolijua, basi imani yake ni dhaifu kwa mitazamo miwili; mosi, kufuatilia jambo asilo na elimu nalo, na pili, kuizungumza na kuitekeleza imani isiyo sahihi.

Ø Mtu anayefuata mkumbo wa kuwaiga wengine katika kuyakubali mambo yanayohusiana na imani (Aqiida) bila kujua dalili za kitaalamu zinazowathibitishia mambo hayo, basi huyo naye anafuata jambo asilo na elimu nalo. Hata hivyo, mtu anaweza kuepuka lawama kama ana dalili ya jumla ya mambo anayoyaamini, kama vile kutumia ushahidi wa maumbile kuamini kuwa Mungu yupo, jambo ambalo, kimsing, linaunda elimu.

Ø Kutekeleza taqliid yaani kukubali, kuamini na kutekeleza fatwa za wanazuoni katika ufafanuzi na ufasiri wao wa mas’ala ya Shariah ambayo si sehemu ya Aqiidah hakuhesabiwi kama ni imani ya kibubusa kwa sababu Mwenyezi Mungu anasema, “Na wale wasiojua wawaulize wenye kujua..” (16:43). Na hivyo imani ya mtu huyu yaweza kuelezewa kwa usahihi kuwa inatokana na elimu sahihi.
Njia Sahihi ya kufundisha Aqiida
Vipengele vya Imani ya Kiislamu na dalili za kuthibitisha vipengele hivyo vinawasilishwa na kupambanuliwa ndani ya Qur’an kwa mtindo wa wazi na mwepesi kabisa.

Hivyo basi, Wanazuoni wa Kiislamu wanashauriwa kufuata utaratibu wa Qur’an pale wanapofundisha Aqiidah kwa watu wa kawaida. Kwani, kwa hakika utaratibu wa Qur’an ni mwepesi mno kueleweka katika akili ya mtu kuliko taratibu ngumu na zenye msamiati mgumu wa wanatheolojia ambazo zimewatisha watu hata kuiogopa ilimu ya dini jambo ambalo linalaumiwa kwa kukwaza ufahamu wa mafundisho ya imani ya Kiislamu katika zama hizi.

Yawapasa pia wanazuoni wa Kiislamu kujenga utamaduni kwamba pale wanapofafanua elimu ya dini kwa watu wa kawaida kutoa fatwa zao kwa dalili madhubuti kutoka kwenye Qur’an na Sunna kwani hili litawawezesha Waislamu hao kufahamu mizizi ya dini yao, na itawawezesha kutii maamrisho ya Mwenyezi Mungu ndani ya nyoyo zao.

Wanazuoni wa Kiislamu waepuke kuthibitisha masuala ya Imani au yale yanayohusiana na hukumu za Kisheria kwa kutumia Hadith dhaifu. Hata hivyo, kama hukumu tayari imekwishawekwa na Hadith sahihi kama vile fadhila za kisimamo cha Usiku au Swala ya Usiku, na tukakutana na hadith dhaifu kidogo inayosisitizia fadhila za Swala za Usiku, twaweza kuinukuu maadam tubainishe kuwa hiyo ni Hadith dhaifu.

Hii inatokana na kanuni ya kisheria ambayo inasema, “Hadiyth dhaifu zaweza kutumika kuongeza msisitizo wa fadhila zilizothibitika za matendo ya ibada.”

Ambacho kinabainishwa na kanuni hiyo ni kwamba Hadith dhaifu hutumika kama uthibitisho tu wa ziada wa hukumu ambazo tayari zimekwishathibitishwa na dalili sahihi.

Sehemu kubwa ya ilimu kuhusu maisha ya barazak, Matukio ya Siku ya Hesabu, dalili za Kiyama,, Malaika, Majini, Arshi, Lauhin Mahfudh na kadhalika yote ipo upande wa elimu ya ghaibu ambayo yaweza tu kufahamika kwa njia ya wahyi.

Ndiyo kusema, sisi tuzingatie ile ilimu ghaibu ambayo Qur’an na Hadith Sahihi zinatufahamisha kwa pamoja. Ni jambo la kusikitisha kuwa vitabu vingi vya rejea vya dini vinakutwa na maneno na maelezo kuhusu mambo ya ghaibu ambayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na riwaya za uzushi mtupu. Tusiitilie maanani ilimu isiyo sahihi.

Mwisho, mara zote, tunapaswa kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu atatuuliza Siku ya Hukumu juu ya kila jambo tulifanyalo katika maisha haya ya dunia. Hili linathibitika katika Qur’an:

“Wala usifuate (ukipita ukiyasema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo, hivyo vyote vitaulizwa.” (17:36)

Hivyo, mtu akisema nimeona hiki na kile, au nimesikia hivi na vile, au nimeamini hivi na hivi, basi moyo wake, macho yake, na masikio yake vitachukua nafasi ya kutoa ushahidi Siku hiyo ili kuthibitisha au kukataa. Mwenyezi Mungu anasema, “Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao, na mikono yao na miguu yao, kwa yale waliyokuwa wakiyafanya.” (24:24)


Ukinyoa upara usiokote madorianiCOMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: CHUNGA MAMBO HAYA
CHUNGA MAMBO HAYA
https://1.bp.blogspot.com/-2orQfRbJRgA/WTJ4gDn_YDI/AAAAAAAABRo/-G-XMOfj6N86Hgw0rPeen4mMOXHTABdlwCPcBGAYYCw/s400/IMG_20170421_082656.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-2orQfRbJRgA/WTJ4gDn_YDI/AAAAAAAABRo/-G-XMOfj6N86Hgw0rPeen4mMOXHTABdlwCPcBGAYYCw/s72-c/IMG_20170421_082656.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/06/chunga-mambo-haya.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/06/chunga-mambo-haya.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content