KUOMBA MSAMAHA KWA ALLAH

Kimaumbile mwanadamu ni kiumbe mwenye udhaifu mwingi na ni kiumbe ambaye bila msaada wa Mwenyezi Mungu hana uwezo wa kujisaidia. Kwa ha...Kimaumbile mwanadamu ni kiumbe mwenye udhaifu mwingi na ni kiumbe ambaye bila msaada wa Mwenyezi Mungu hana uwezo wa kujisaidia. Kwa hali hilyo mwanadamu huweza kufanya makosa mengi katika maisha yake.

Anaweza kuwa muumini mwenye kujitahidi kujiepusha na makosa au madhambi makubwa lakini bado kwa vile yeye ni mja wa Allah mwenye upungufu, hatoweza kuwa huru kabisa na makosa yote.

Katika Qur,an tunafahamishwa kuwa mwanadamu mbele ya macho ya Allah anakasoro na madhambi:

Na kama Mwenyezi Mungu angaliwatesa watu kwasababu ya vile walivyovichuma basi asingaliacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini yeye anawaakhirishiya mpaka (ufike) Muda uliowekwa. Basi itakapokuja ajali yao, (hapo bila shaka watalipwa); na Mwenyezi Mungu anawajuwa vema waja wake. (35:45)

Kulingana na maelezo haya ya Qur’an muumini hatarajiwi kuwa na mwenendo wa kujiona kuwa yeye hana kasoro au dhambi. Badala yake muda wote anatakiwa awe mtu wa kuomba maghfra kwa Mwenye zImungu.

Huu hasa ndio mwenendo unaomtofautisha muumini na kafiri. Makafiri hufanya jitihada za kuficha kasoro na madhambi yao lakini muumini hathubutu hata kidogo kufanya hivyo.

Kilicho muhimu kwa muumini ni kule kujuta nafsini ambako humfanya ajirudi na kumgeukia Mola wake ili kumuomba msamaha.

Tunaposoma Qur’an, tunaona kuwa kuomba maghfra ni jambo la kawaida na ni sifa kwa Muumini. Kwasababu hiyo Waumini katu hawawezi kujiona watakatifu, wasio na dhambi wala kasoro. Siku zote na muda wote wao huomba Rehma za Mola wao. Katika aya ifuatayo jambo la kumuelekea Allah na kumuomba toba huesabbiwa kuwa ni moja ya sifa muhimu za Muumini:

(Hao walioahidiwa kupata hayo ni wale) wanaotubia (wakikosa), wanaofanya ibada, wanaomshukuru Mwenyezi Mungu, wanaofunga, wanaorukuu na kusujudu, wanaoamrisha mema na wanaokataza mabaya na wanaohifadhi mipaka ya Mwenyezi Mungu hawaipindukii). Basi wape habari njema hao walioamini. (9:112)

Tofauti kati ya dhana hizi mbili Toba na Maghafra lazima izingatiwe kwa makini. Kuomba maghfira ni jambo la kawaida na la kila siku katika maisha ya Ibada ya Muumini.

Mtu anaweza kuomba maghufira kwa Allah hata siku nzima kutokana na madhmbi yaliyofanywa kwa kukusudia au bila kukusudia au kwa kujuwa au bila kujuwa.

Katika lugha ya kiarabu neno istighifaru linamaana ya kuomba msamaa hii maana yake ni kumuomba Ghafuru yaani yule mwenye kughufiriya. Neno Ghafuru lina maana ya kufunika, kusitiri, kuhifadhi, kuficha na kurudisha upya.

Hivyo kuomba Maghufira kwa Allah maana yake ni kujitakasa nafsi na hivyo kuomba hifadhi katika Rehma za Mwenyezi Mungu.

Katika Qur’an waumini huomba kwa kusema “Mola wetu! Tumesikiya mwitaji anayeita kuwendeya Uislamu kwamba mwaminini Mola wenu. Tukaamini. Mola wetu! Tusamehe madhambi yetu na utufutiye makosa yetu na utufishe pamoja na watu wema” (3:193)

Jibu la Mwenyezi Mungu kuhusiyana na maombi hayo ni hili: Kwa yakini mimi ni pamoja nanyi. Kama mkisali na kutowa zaka na mkiwaamini Mitume wangu na kuwasaidiya na kumpa Mwenyezi Mungu karadha nzuri, bila shaka nitakufutiyeni maovu yenu na kukuingizeni katika mabustani ipitayo mito mbele yake. Lakini atakayekataa miongoni mwenu baada ya (ahadi) hii, bila shaka amepoteya njiya iliyosawa (5:12).

Kama ilivyoelezwa hapo juu kumuomba maghufira mwenyezi Mungu ni jambo linaloweza kufanywa kwa yote mawili; ama kwa dhambi iliyotendwa kwa makusudi au kwa dhambi iliyotendwa bila kukusudiya au kwa madhambi ya waumini wengine. Hii ni tofauti kuu kati ya kuomba Maghufira na kuomba Toba.

Ingawaje kuomba Maghufira ni duwa ya siku zote ya Muumini lakini kutubiya ni mwenendo thabiti wa kutubu kwa dhambi fulani au kwa kasoro fulani. Hapa mtu hudhamiriya kwa dhati kutorudiya tena dhambi aliyoitenda.

Kutubiya ni kukimbiliya kwa Allah kwa dhambi ambayo mtu ameitenda, mtu hujuta na kuahidi kutoitenda tena na zaidi ya hivyo huomba uongofu na msaada wa Allah. Hii hasa ndiyo maana ya Toba yaani “kujirudi.”

Kwahiyo Toba ni ahadi thabiti ya kutotenda tena dhambi. Niya ya mtu katika toba isiwe tena kurudiya dhambi hiyo. Mwenyezi Mungu anawaamrisha hivi Waumini:KUOMBA MSAMAHA KWA MWE NYEZI MUNGU

Enyi mlioamini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu Toba iliyo ya kweli; huenda Mola wenu akakufutiyeni maovu yenu na kukuingizeni katika pepo zipitazo mito mbele yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Mtume wala wale walioamini pamoja naye, Nuru yao itakuwa inakwenda mbele yao na pande zao za kulia na huku wanasema:

“Mola wetu! Tutimiziye nuru yetu, na utughufiriye, hakika wewe ni mwenye uweza juu ya kila kitu


Hata hivyo hii haina maana kuwa muumini hutubu dhambi au kosa lake mara moja tu. Eti kwamba anaweza kutubiya wakati fulani na kisha kurudiya tena kosa lile lile ingawaje Rehma za Mwenyezi Mungu haziishi kumshukiya mja.

Kwa hiyo basi bado mtu anayo nafasi ya kutubiya kwa dhambi yoyote iwayo. Mwenyezi Mungu anawaambiya hivi waja wake:

“Enyi waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu! Msikate tamaa na Rehma ya Mwenyezi Mungu; bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zot; hakika yeye ni mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu. Na rejeeni kwa Mola wenu na mnyenyekee kwake kabla ya kukujieni adhabu, kisha hamtanusuriwa. (39:53-54).

Lakini kuna aina ya toba ambayo Mwenyezi Mungu hataikubali. Toba isiyo na Ikhilaswi ambayo hutolewa pale mauti yanapomfika mtu. Huu ni wakati ambapo mtu hufikiwa na maika wa kifo. Kuhusiyana na hili, Qur’an inasema:

Toba inayopokelewa na Mwenyezi Mugngu ni ya wale wanaofanya uwovu kwa ujinga, kisha wakatubiya kwa wepesi. Hao ndiyo Mwenyezi Mungu huipokeya Toba yao. Na Mwenyezi ni Mjuzi na mwenye hikima.

Hawana toba wale ambao hufanya maovu mpaka mauti yamemuhudhuriya mmoja wao, akasema: “ Hakika mimi sasa natubu.” Wala hawana toba wale ambao wanakufa katika hali ya ukafiri. Hao tumewaandalia adhabu iumizayo. (4:17-18).


sayyidbunduki.blogspot.com

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: KUOMBA MSAMAHA KWA ALLAH
KUOMBA MSAMAHA KWA ALLAH
https://1.bp.blogspot.com/-cBQktuXARJM/XSSW0aJTh5I/AAAAAAAAHmw/2XbA6Ofx81AFZUzCebAZ52ZjVT2fXGypACLcBGAs/s400/dua.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-cBQktuXARJM/XSSW0aJTh5I/AAAAAAAAHmw/2XbA6Ofx81AFZUzCebAZ52ZjVT2fXGypACLcBGAs/s72-c/dua.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/06/kuomba-msamaha-kwa-allah.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/06/kuomba-msamaha-kwa-allah.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content