Maandalizi ya kumi la mwisho la RAMADHANI.

KUMI LA MWISHO LA RAMADHANI SIFA zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Azzawajalla, Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na nyingine nd...

KUMI LA MWISHO LA RAMADHANI

SIFA zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Azzawajalla, Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na nyingine ndogo ndogo. Swala na salamu zimwendee Mtume Muhammad Swaalla Allahu 'alayhi Wasallam. Enyi Waislamu, Siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani zinaendelea kuisha. Na hivi sasa tunaelekea katika kumi la mwisho.
Je ndugu yangu Muislamu umejiuliza suala moja; Je, nimefaidika kiasi gani na siku zilizopita? Kuwa mkweli na nafsi yako na ujifanyie hisabu ya vitendo vyako kabla hujafika siku ya kufanyiwa hisabu.
Ndugu Muislamu, bado wakati upo, na fursa ya kufanya mambo ya kheri bado inaendelea.
Kumi la mwishio ni muhimu katika umri wa mwanadamu, ndani yake kuna usiku mtukufu. Mwenye kuafikiwa usiku huo basi amepata kheri ya dunia na akhera. Na mwenye kukosa usiku huo basi amekosa kheri ya dunia na akhera.
Ni hasara iliyoje mtu kuishi duniani miaka mingi kisha aondoke duniani patupu bila ya kupata kheri ya dunia wala kheri ya akhera.

 Tafakari na uzingatie, hujui kama utafika mwakani ili uweze kufunga Mwezi wa Ramadhan.
Watu wema walikuwa wakimuomba Allah mwaka mzima awaafikie kuweza kuzifikia siku hizi za kheri.
Na wakifikiwa nazo huwa na furaha nyingi, kwa kupata bahati ya kuishi mpaka kuweza kufunga Mwezi wa Ramadhani. Ndugu Muislamu Mtume Muhammad Swalla Llahu 'alayhi wasallam Ametufundisha mambo mengi na ibada nyingi ambazo Muislamu anaweza kuzifanya kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allah Subuhaanahu wa Taala.
Katika Ibada hizo ni kama ifuatavyo; Kufanya bidii kusali swala ya usiku, na kuwahimiza watu wako nyumbani kuamka kusali pamoja na wewe.
Kusamehewa madhambi yaliyotangulia
Amesema Mtume Swalla Llahu 'alayhi wasallam): Mwenye kusimama usiku katika mwezi wa Ramadhan kwa Ikhlasi na kutarajia malipo kwa Allah, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.
Ilikuwa likifikia kumi la mwisho Mtume alikuwa akigura matandiko yake na akijitahidi kusimama usiku na kuamsha wake zake na familia yake.
Kuzidisha juhudi kutafuta Usiku wa cheo. Usiku huu ni bora kuliko miezi elfu moja, bali ni bora kushinda vitu vyote vilivyomo duniani.

 Mwenye kuafikiwa kupata usiku huu basi kwa hakika amefaulu na kupata kheri ya dunia na akhera. Katiak mafundisho ya Mtume Swalla Llahu 'alayhi wasallam) kuhusu usiku mtukufu; 

Ni sunna kuzidisha kusoma Qur’an kwa wingi, kumsifu Allah na kumtukuza na kumsalia Mtume, kutoa sadaka. Na ni sunna kuomba dua kwa wingi. Bibi Aisha Alimuuliza Mtume: Je niombe dua gani katika usiku huu? Akamuambia sema: 

Ewe Mola hakika yako wewe ni mwenye kusamehe waja wako na unapenda kusamehe. Nakuomba unisamehe.


Mwenyezimungu ndiye ajuwae zaidi.

Imenakiliwa na mrbunduki.com

Asanteni sanaCOMMENTS

BLOGGER: 2
  1. Shukran sana ndugu zaku waislam kwa mafunzo mazuri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante Sana. Tunashkuru KWA ushirikiano wako🙏🙏

      Delete


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: Maandalizi ya kumi la mwisho la RAMADHANI.
Maandalizi ya kumi la mwisho la RAMADHANI.
https://3.bp.blogspot.com/-lSdKCgVp2sg/WxOGbDw9zaI/AAAAAAAACko/cPjddWGqRlA9_MEw90Q2e8TrowDl1Q9MgCLcBGAs/s400/ramadan-kareem-greeting_1826922.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-lSdKCgVp2sg/WxOGbDw9zaI/AAAAAAAACko/cPjddWGqRlA9_MEw90Q2e8TrowDl1Q9MgCLcBGAs/s72-c/ramadan-kareem-greeting_1826922.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/06/maandalizi-ya-kumi-la-mwisho-la.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/06/maandalizi-ya-kumi-la-mwisho-la.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content