UMUHIMU WA SIKU YA IJUMAA KWA MUISLAMU

SIKU YA IJUMAA KWA MUISLAMU Inajenga nidhamu ya kuchunga muda · Inajenga ustaarabu wa kijamii Na Dkt. Hassan Abu Ghuddah, mfasiri S. Huss...

SIKU YA IJUMAA KWA MUISLAMU

Inajenga nidhamu ya kuchunga muda
· Inajenga ustaarabu wa kijamii


Na Dkt. Hassan Abu Ghuddah, mfasiri S. Hussein

Mwenyezi Mungu anasema, “Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya Sala ya siku ya Ijumaa, nendeni upesi kumtaja Mwenyezi Mungu na acheni biashara. Kufanya hivi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua (hivi basi fanyeni). Na itakapokwisha Sala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufaulu.” (62:9-10)

Ijumaa ni Siku ya Wiki ambayo Mwenyezi Mungu ameichagua maalum kwa ajili ya Waislamu. Hii ndiyo Siku ambayo Kiama kitasimama. Yasemekana kuwa sababu ya siku hii kuitwa ‘Aljumuah” ni kwamba ndiyo siku ambayo Adam aliumbwa (ju-me-‘a-maana yake, ‘kuunganishwa pamoja); yaani aliumbwa siku ya Ijumaa.

Abu Huraira kasimulia kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, “Siku bora kuchomozewa na jua ni Ijumaa. Ndiyo Siku ambayo Adam aliingia Peponi, na ndiyo Siku aliyotolewa humo.” (Muslim)

Siku ya Ijumaa ina hadhi kubwa katika Uislamu. Kila Ijumaa, kuna muda ambao Mwenyezi Mungu anazijibu dua. Mwenyezi Mungu ameuweka muda huu katika wakati ambao haukutajwa. Hatujui ni wakati gani jambo hilo hutokea. Hii imeachwa hivyo ili watu wahamasike na kuhangaika kutafuta fadhila za Ijumaa Siku nzima.

Abu Hurairah kasimulia kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, “hakuna saa katika siku ya Ijumaa ambayo Mja Muislamu wa Allah anayesimama katika Sala na kumuomba kitu ila Mwenyezi Mungu humpa kitu hicho.” (Bukharin a Muslim).

Uislamu umeweka matendo fulani ya kidini na kijamii kwa ajili ya Ijumaa. Hayo ni matendo mahususi kwa mnasaba wa Siku hii. Miongoni mwa matendo hayo ni kufanya josho (ghusl), usafi, kujitia manukato, na kupendeza.

Imesimuliwa kuwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, “Inapokuwa ni Siku ya Ijumaa, halafu mtu akaoga, akapaka nywele mafuta, akatia manukato mazuri zaidi, akavaa nguo nzuri zaidi, kisha akatoka kwenda kuswali, na akaepuka kuwapangua watu waliokaa pamoja Msikitini, kisha akamsikiliza Khatibu anayekhutubu, basi dhambi zake zitasamehewa baina ya Ijumaa hii na iliyopita, na siku tatu zaidi (yaani jumla ya siku kumi)” (Ibn Khuzaymah).

Mtu anayeyatafakari matendo hayo, ataona kuwa kila moja lina lengo lenye manufaa. Kwa kutumia maji kunawa na kutia udhu, Waislamu hijikinga na maradhi na maambukizi yanayoweza kutokea katika mikusanyiko. Manukato na muonekano mzuri huleta utangamano, ukaribu na urafiki. Haya ndiyo malengo mema ambayo kila jamii njema hutaka kuyafikia.

Mambo mengine ya kidini yanayohitajika kufanyika Siku ya Ijumaa ni pamoja na: kwenda Msikitini mapema, kuepuka kuwasumbua watu kwa kuwaruka-ruka au kuwabana-bana, au kuwasogeza-sogeza pale walipokaa, na kutowavurugia mazingatio wakati wanapojielekeza katika ibada. Mkusanyiko wa watu hupendezeshwa na unadhifu na usafi.

Abu Umamah amesema, “nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, akisema, “Malaika hukaa kwenye milango ya Msikiti. Wanamwandika mtu wa kwanza, wa pili, na wa tatu kuingia Msikitini, hadi Imam (Khatibu) anapotokea (kutoa khutuba), ndipo yaliyoandikwa yanapopaishwa juu.” (Ahmad).

Uislamu umetahadharisha juu ya mambo hasi ili kulinda hadhi ya Msikiti. Na hayo humsaidia kudumisha unyenyekevu, tafakuri na taqwa. Wale wanaochelewa Msikitini lakini bado wakatafuta nafasi ya mbele waache tabia hiyo na badala yake wawahi Msikitini kama wanataka kupata fadhila za Ijumaa.

Matendo mengine yanayopendeza Siku ya Ijumaa ni pamoja na kusoma aya za Qur’an, kumswalia Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, na kusikiliza khutuba.

Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, “yeyote anayesoma Suratul al-Kahf siku ya Ijumaa, nuru itamng’aria hadi Ijumaa nyingine.” (Baihaqi).

Pia anaweza kusoma chochote anachoweza kutoka katika Qur’an kwani kila herufi inayosomwa hupata thawabu kumi. Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema, “Siku bora katika Siku zenu ni Ijumaa. Basi kithirisheni kunisalia ndani yake.” (Abu Dawud na An-Nasa’i)


Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alitutahadharisha juu ya wajibu wa kumsikiliza Khatibu anapokhutubu na kuepuka kuvuruga mazingatio wakati wa khutba:

“Ukimwambia mwenzio Siku ya Ijumaa, “Sikiliza!’ ilihali Khatibu anazungumza, basi umefanya kosa.” (Bukhari na Muslim). Kwa maneno mengine, utakuwa umepunguza fadhila zako za Sala ya Ijumaa.

Makala hii imetaja matendo mengi yanayohimizwa Siku ya Ijumaa, na mengi ambayo yanakatazwa. Baadhi ya hayo yamehukumiwa kisheria, na baadhi hayakuhukumiwa.

Lakini yote yakichanganywa pamoja, ni dhahiri kuwa Uislamu ni mfumo wa jamii unaokusanya utamaduni wa kimaadili. Ni mfumo unaofundisha ustaarabu katika mambo yote.

Uchungaji wa muda katika kuwahi Ijumaa, Usafi katika kutia udhu, nidhamu ya kutowakarahisha wengine wakati wakiwa wamekaa, utulivu wa kumsikiliza Imamu, haya yote ni mafunzo ya ustaarabu ambayo yakizingatiwa katika sehemu nyingine za maisha, humjengea mtu heshima ya hali ya juu.

Hiyo ndiyo nafasi ya Ijumaa katika maisha ya Muislamu. Ni fursa ya kustawisha afya ya mwili na ya roho, ni fursa ya kujenga Umoja na Mshikamano miongoni mwa Waislamu, ni fursa ya kujenga utamaduni wa Kiislamu. Kwa kuzingatia yote hayo ndipo falsafa ya Mwito wa Mwenyezi Mungu inapofahamika:

“Mwenyezi Mungu anasema, “Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya Sala ya siku ya Ijumaa, nendeni upesi kumtaja Mwenyezi Mungu na acheni biashara. Kufanya hivi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua (hivi basi fanyeni). Na itakapokwisha Sala, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufaulu.” (62:9-10)IMENAKILIWA NA sayyidbunduki.blogspot.com


kutoka katika vyanzo vinavyoaminika.
COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: UMUHIMU WA SIKU YA IJUMAA KWA MUISLAMU
UMUHIMU WA SIKU YA IJUMAA KWA MUISLAMU
https://1.bp.blogspot.com/-uGRTwhTlWBs/XSSXYlpVRjI/AAAAAAAAHnA/XWYko927xC4BywYWYaaCT4fj4t87tst4gCLcBGAs/s400/jumaa%2Bkareem.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-uGRTwhTlWBs/XSSXYlpVRjI/AAAAAAAAHnA/XWYko927xC4BywYWYaaCT4fj4t87tst4gCLcBGAs/s72-c/jumaa%2Bkareem.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2018/06/umuhimu-wa-siku-ya-ijumaa-kwa-muislamu.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2018/06/umuhimu-wa-siku-ya-ijumaa-kwa-muislamu.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content