Usiku wake Manani kuna
mengi yafanyika
Ni vigumu kuamini, kuna
nyingi patashika
Kwa watu pia majini,
wengi wanahangaika
Laiti ungeyajua,
hungetamani kuishi
Kwanza wale wanozini,
ndio muda muafaka
Kwenye nyumba za wageni,
na njiani kadhalika
Wanadhani hawaoni,
Mwenyezi alotukuka
Laiti ungeyajua,
hungetamani kuishi
Wezi nao majumbani, ndo
muda wanozunguka
Kunyapia barazani, wewe
uko nyaka nyaka
Kujipenya hadi ndani,
huiba na kuondoka
Laiti ungeyajua,
hungetamani kuishi
Wachawi na mashetani, ndo
nao wanazinduka
Wale wa makaburini, muda
kwao umefika
Warukaji wa angani, ndo
wanaanza kuruka
Laiti ungeyajua,
hungetamani kuishi
Misukule mashambani, ndo
muda wa kupigika
Na vijembe mikononi,
kulima heka kwa heka
Japo sisi hatuoni, lakini
yapo hakika
Laiti ungeyajua,
hungetamani kuishi
Lakini kwa waumini, ndo
huchukua birika
Maji hujaza pomoni, na kisha
kutwaharika
Huingia ibadani, kumlilia
Rabuka
Allah tujalie nasi, tuwe miongoni mwao
Ni kheri kwa waumini,
muda wa kutononoka
Hupanda zao imani, kwa
sala za uhakika
Humlilia Mannani, hutaraji kuongoka
Ila hawa ni wachache,
Mungu atuweke nasi
Mambo mengi tafarani,
usiku yanafanyika
Machache hayo nadhani,
yanatosha kuandika
Wosia-tudumisheni, ibada,
sala na zaka
Hapo tutaepukana, na
mambo yakupoteza
Bunduki.com
COMMENTS