1. NGANGANGA
UMETAITI, MITHILIYO NI MKANDA
HATA MATE
HAYAPITI, TASEMA PETE NA CHANDA
WAKULILIA
UMATI, WAKURUDI NA WANAKWENDA
Maisha punguza kasi, mbona umebana sana?
2. KWELI
NILIJIDHATITI, MAANA NILIKUPENDA
NIWE MWAKO
KATIKATI, NIKAIANZA KALENDA
LEO SINA
HATA KITI, SISEMI HICHO KITANDA
Maisha
punguza kasi, mbona umebana sana?
3. MAISHA
UMEDHIBITI, NYANJA ZOTE ZIMEPINDA
HATA MKATE
SIPATI, WALA UGALI MLENDA
SI ANDAZI SI
CHAPATI, MAISHA MWENZI NAKONDA
Maisha
punguza kasi, mbona umebana sana?
4. KILA KAZI NI
KIBUTI, MAMBO YANAGOMA KWENDA
NIMESHACHOMA
BARUTI, NIKAJARIBU KUWINDA
MARA NIPO
MTU KATI, WAMESHANITOA NUNDA
Maisha
punguza kasi, mbona umebana sana?
5. MAISHA
MSAMIATI, KUFUMBUA WANISHINDA
WATOTO NAO
UMATI, WANANIFANYA NAKONDA
BORA NILE MKUYATI, NITAFURAHI HUENDA
Maisha punguza kasi, mbona umebana sana?
BY: bunduki.com
COMMENTS