Yanini
kuungulika, mwenyewe hana taimu
Kichwani
hawezi toka, namfanya ni muhimu
Kutwa
nikihangaika, kwenye meseji na simu
Shobo za
nini lakini, mbona ninahangaika
Nimekuwa
mamluki, sijui ninachotenda
Moyoni
anidhihaki, aniona mwana kwenda
Kwangu
haiishi dhiki, ndio sababu kupenda?
Shobo za
nini lakini?, Ishaallah nitasahau
Nataka
kumsahau, lakini moyo wagoma
Moyoni
kauli mbiu, ni yeye dada HALIMA
NIFANYE
NINI WADAU, kupoza wangu mtima
Ila shobo
zitakwisha, Nitapiga moyo konde
Afanya
anavotaka, kisa kwake siongei
Simuni
napomsaka, mara nyingi hapokei
Ipo siku
tafunguka, kama mbwai iwe mbwai
Mapenzi
yakija isha, tusije laumiana
Bora
nitafute mbinu, nikate huu mzizi
Niutwange
kwenye kinu?, niuchune kama ngozi?
Maana
mapenzi tunu, na ni ngumu ku balanzi
Nitajikaza
kiume, mwisho nitamsahau
Shobo
namshobokea, sijui shobo za nini?
Uzuri we wa
bandia, na wala si wa mjini
Ni mweusi
atishia, kama mafuta ya GANI
Nitajikaza
kiume, mwisho nitamsahau
COMMENTS