Iitikadi za mavumba, ni mambo ya kibazazi
Kutupiana na ndumba, ni kuvurugana kazi
Upendo ni fumbo fumba, moyo wako uwe radhi
Kupenda moyo si ndumba, ni kupotezana muda
Upendo otomatiki, huota ndani moyoni
Moyo ukipiga tiki, kifatacho ni mwilini
Mapenzi hayana kiki, kurogana chuguuni
Mapenzi ya kurogana, hayadumu asilani
Kama hupendwi nyamaa, tafuta kwingine bwana
Kama amekukataa, yupo mtaeendana
Epuka mbaya tamaa, kwa waganga kurogana
Dawa zikiisha nguvu, chuki ipo pale pale.

COMMENTS