Salamu sana, wadau, nadhani mko vizuri Niko mwanana, ngalau, na mie niko ngangari Twakumbushana, walau, tupate kutafakari SHAIRI. D...
Salamu sana, wadau, nadhani mko vizuri
Niko mwanana, ngalau, na mie niko ngangari
Twakumbushana, walau, tupate kutafakari
SHAIRI.
Niko mwanana, ngalau, na mie niko ngangari
Twakumbushana, walau, tupate kutafakari
SHAIRI.
Dunia jama, mapito, na sisi ni wasafiri
Hebu tazama, kwa mato, kisha jipe tafsiri
Watu wa hima, fukuto, limewatia kabari
FIKIRI.
Hebu tazama, kwa mato, kisha jipe tafsiri
Watu wa hima, fukuto, limewatia kabari
FIKIRI.
Dunia nguo, chakavu, walisemaga wahenga
Vingi vileo, lemavu, vinatutia ujinga
Ukweli huo, angavu, uchukue utasonga
VIZURI
Vingi vileo, lemavu, vinatutia ujinga
Ukweli huo, angavu, uchukue utasonga
VIZURI
Tumche Mungu, jamani, jamani jamani jama
Ewe mwenzangu, jirani, nakueleza kwa hima
Sijui wangu, undani, umri lini wakoma
NI SIRI
Ewe mwenzangu, jirani, nakueleza kwa hima
Sijui wangu, undani, umri lini wakoma
NI SIRI
Lete khushui, upole, akuokoe Qahari
Kwani hujui, ya mbele, ni kumi au sifuri
Siwe bedui, misele, uache visa, kiburi
JEURI
Kwani hujui, ya mbele, ni kumi au sifuri
Siwe bedui, misele, uache visa, kiburi
JEURI
Tubia dhambi, muasi, piga konde wako moyo
Muepuke, ibilisi, wacha maovu lonayo
Iombe FIRDAUSI, kwa leo yangu ni hayo.
KWAHERI
Muepuke, ibilisi, wacha maovu lonayo
Iombe FIRDAUSI, kwa leo yangu ni hayo.
KWAHERI
COMMENTS