BACHELA
Siku mpya ikianza, huwa pesa nawazia
Nikosapo najibanza, hakuna
wakusumbua
Wewe ukikosa manza, watoto watakuua
Acha
mke kula bata.
MWENYE NDOA
Kijana hebu sikiza, hwenda bado
hujakua
Najua unanibeza, (ila) utoto wakusumbua
Swali moja nakuliza, kichaa
umeugua?
Nitakuchapa
mambata.
BACHELA
Wanichekesha ajuza, pozi zimekuishia
Umezaa umekuza, kutwa kiguu na njia
Yupo wa kuniliwaza, nikitaka hunijia
Hakuna
tantaranta.
MWENYE NDOA
Madhambi unaongeza, unamuudhi
Jalia
Kutwa kucha kutongoza, mwishowe
utaumia
Mwenzio nala nasaza, ndoani
nimetulia
Makubwa
yatakupata.
BACHELA
Sema kidogo bakiza, yako nisije
fichua
Huyo mkeo Aziza, ulianza kubomoa
Sasa unanishangaza, uwokovu kujitia
Mkia
umeufyata.
MWENYE NDOA
Hebu jaziba punguza, kubaya
waelekea
Mimi nakuelekeza, ufanyacho
wakosea
Mwanadamu kuteleza, kawaida
kukosea
Ni
mambo yalishapita.
BACHELA
Ndowa kujipandikiza, mawazo kutwa
kulia
Ndo mana naipuuza, nimechoka kujutia
Ukitoka unawaza, wesije kukuchapia
Nisije
nikaja juta.
MWENYE NDOA
Unaona wajiweza, yakudanganya
dunia
Umri waenda faza, utabaki kuongea
Uzeeni utaoza, ni nani atakulea
Wenzio
yeshawakuta.
BACHELA
Bwana we wanichukiza, nioe nitafulia
Ukishakuitwa faza, watoto wanasumbua
Kesho nakufa naoza, yanini nisotulia?
Mishe
zangu zitasita.
MWENYE NDOA
Kijana unajibeza, kutwa pesa
unatoa
Gesti kujipenyeza, nguvu
zinakuishia
Hivyo visupu vya pweza, mwishowe
utapotea
Unakausha
mafuta.
Huo ujana ni kiza, totoro
kilotulia
Usijione waweza, UKIMWI utakuuwa
Hilo ninakudokeza, kaa chini
fikiria
Duniani
tunapita.
COMMENTS