NANI UNAMPA KURA?

MASHAKA
Wajifanya umeganda, na mke wako wa ndani
Mwajifanya pete, chanda, heti wako abadani
Sasa ile misambwanda, unaitizama nini?
NJE KUNA MAMBO MENGI, LAZIMA TU REFRESH

MSHAMU
Sikiliza ndugu kaka, tamaa zitakuuwa
Jina lako tu Mashaka, maisha hujayajuwa
Tofauti naitaka, wapi unapochagua
KWANINI UNACHEPUKA?, WAKATI NI ILE ILE?

MASHAKA
Sio ile ile moja, Mkubwa una wehuka
mbona waleta viroja, ajabu kubwa ya mwaka
Nje napata faraja, NDANI gubu likiwaka
NJE KUNA MAMBO MENGI, LAZIMA TU REFRESH

MSHAMU
Gubu unajitakia, tabiazo si nzuri
Mke atakuwakia, unapoleta kiburi
Hatoweza vumilia, nje kwenda kuvinjari
KWANINI UNACHEPUKA?, WAKATI NI ILE ILE?

MASHAKA
hwenda weye una dhiki, ndo mana waleta hoja
MWANAUME haridhiki, na mwanamke mmoja
Mambo yako yakitiki, tutajakuwa pamoja
NJE KUNA MAMBO MENGI, LAZIMA TU REFRESH

MSHAMU
Mimi ni mume rijali, sikiliza wewe boya
Pande zote ni kamili, usinelewe vibaya
Nimeridhika na hali, sipendi hizo hekaya
KWANINI UNACHEPUKA, WAKATI NI ILE ILE

MASHAKA
Haya wewe tulizana, kwangu haiwezekani
Omba na mamie wana, asije anza uhuni
Tusije kutafutana, na kushikana ugoni
NJE KUNA MAMBO MENGI, LAZIMA TU REFRESH

MSHAMU
Ishike adabu yako, mwana izaya wahedi
Ubaki huko uliko, mwache wangu Mama Medi
Wanaokupa ujiko, Subiri na mijeledi
MWISHO WAKO NI MARADHI, NA ADHABU YA KABURI

MTUNZI
Kama una mushkeli, wewe utaniambia
Hawa vijana wawili, nani amekuvutia
Ni nani msema kweli, kwa ulivo jionea

@bunduki.com

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: NANI UNAMPA KURA?
NANI UNAMPA KURA?
https://1.bp.blogspot.com/-mllH4aKmg7Q/XvSDpAAon8I/AAAAAAAAVCA/NhZVUTTugTYg8K06nErygtwR2vv7XsjwQCK4BGAsYHg/w256-h181/SHAIRI%2B2.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-mllH4aKmg7Q/XvSDpAAon8I/AAAAAAAAVCA/NhZVUTTugTYg8K06nErygtwR2vv7XsjwQCK4BGAsYHg/s72-w256-c-h181/SHAIRI%2B2.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2019/02/nani-unampa-kura-yako.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2019/02/nani-unampa-kura-yako.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content