1. Leo nasema ya kwamba, nakiri ukweli wake
Alonambia mjomba, yanohusu wanawake
Alitaja nyingi namba, naleta uchache wake
Yanohusu wanawake, alinambia mjomba
2. Dhaifu nguvu za mwili, mdomoni mwendo kasi
Akipigwa kofi chali, ila subiri matusi
Hawapendagi ukweli, labda uwe kiasi
Hawa ndio wanawake, alinambia mjomba
3. Hawajali wakipenda, hupenda hata kichaa
Alitaja nyingi namba, naleta uchache wake
Yanohusu wanawake, alinambia mjomba
2. Dhaifu nguvu za mwili, mdomoni mwendo kasi
Akipigwa kofi chali, ila subiri matusi
Hawapendagi ukweli, labda uwe kiasi
Hawa ndio wanawake, alinambia mjomba
3. Hawajali wakipenda, hupenda hata kichaa
Atakwacha mwana kwenda, mimacho umeduwaa
Pesa zako atadunda, ubaki kwenye mataa
Hawa ndio wanawake, alinambia mjomba
4. Sijui hupenda nini, hawa watu yailahi
Amepewa bilioni, atoroka asubuhi
Kwenda kwa mkata kuni, moyo wake ufurahi
Hawa ndio wanawake, alinambia mjomba
6. Mvumilivu wa tabu, kwa yule ampendae
Toka enzi za mababu, mume anakufanae
Azipatapo ghadhabu, hafikirii badae
Ni viumbe wa ajabu, anowajua ni Mungu
7. Jamii ni mwanamke, kupindisha / kuongoa
Ukitaka usitake, mlezi wa familia
Akisema abweteke, watoto wanapotea
Hawa ndio wanawake, alinambia mjomba
8. Nguo laki na ushee, jana memnunulia
Mtaani atembee, vizuri ananukia
Akitokea bwashee, kidogo akimsifia
Hwenda akatoka naye, kwona ni muhimu kwake
9. Tamaa wameumbiwa, abadani haenezi
Ukimpa kitumbua, atatamani kiazi
Ukipenda akijua, ndo utaipata kazi
Hawa ndio wanawake, alinambia mjomba
10. Huwa hawakui hao, huwaga kama watoto
" Mjomba ukiwa nao," jiandae changamoto
Wewe ndo mlezi wao, ikibidi mkong'oto
Hawa ndio wanawake, alinambia mjomba
11. Kuna muda hawafai, huficha yao makucha
Maneno kukulaghai, wavimba kila kukicha
Kumbe ndugu Side BOI, naye anampekecha
Hawa ndio wanawake, alinambia mjomba
COMMENTS