Bandugu wacha DHARAU, maisha hubadilika
Kijana wajisahau, Jua una pumbazika
Usijipandishe dau, sote watu wa Rabuka
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
Kijana wajisahau, Jua una pumbazika
Usijipandishe dau, sote watu wa Rabuka
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
Unaniona nyang'au, kisa nimetoka chaka
Lakini umesahau, Wewe sio malaika
Wewe meli, nami Dau, Sote majini twatweka
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
Kisa ni mweupe au?, watu wanababaika
Ama mi kimbau mbau, wewe kono la birika
Mwili wangu kau kau, wewe ume tipwitika
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
Mara uniite nyau, wanong'ona wasikika
Alinambia mdau, hilo ulipotamka
Wewe wa kuku pilau, mimi ng'onda wa kuoka
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
Wote tuko sawa HAU, Mungu alisha tamka
Usione upo juu, siri ipo kwa RABUKA
Uwe mweupe, bluu, na mimi mwenye mabaka
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
Kiumbe usidharau, Ni Muumba kakiweka
Tena naipiga mbiu, nadhani imesikika
Simcheke mwenye kiu, Nawe kesho takushika
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
By: bunduki.com
Lakini umesahau, Wewe sio malaika
Wewe meli, nami Dau, Sote majini twatweka
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
Kisa ni mweupe au?, watu wanababaika
Ama mi kimbau mbau, wewe kono la birika
Mwili wangu kau kau, wewe ume tipwitika
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
Mara uniite nyau, wanong'ona wasikika
Alinambia mdau, hilo ulipotamka
Wewe wa kuku pilau, mimi ng'onda wa kuoka
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
Wote tuko sawa HAU, Mungu alisha tamka
Usione upo juu, siri ipo kwa RABUKA
Uwe mweupe, bluu, na mimi mwenye mabaka
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
Kiumbe usidharau, Ni Muumba kakiweka
Tena naipiga mbiu, nadhani imesikika
Simcheke mwenye kiu, Nawe kesho takushika
Anaye mjua bora, ni yule alotuumba
COMMENTS