Safari hii ilikuwa ni kwa ajili ya kwenda kwenye semina ya kufunga mwaka ya GALAXY COMPUTERS. Kwa kawa...
Safari hii ilikuwa ni kwa ajili ya kwenda kwenye semina ya kufunga mwaka ya GALAXY COMPUTERS.
Kwa kawaida huwa kila mwaka kuna semina ya kufunga mwaka na kuwasilisha takwimu mbali mbali za biuashara yetu. Mwaka huu semina hii ilifanyika katika jiji la TANGA.
Kwa upande wa MBEYA BRANCH tuliandaa mtiririko wa safari yote kwa ujumla. Chini ya ungozi wa OMY KRISH (Baba la baba)
Washiriki ambao walikuwemo katika safari hii tukufu walikuwa ni kama ifuatavyo:
1. Omary Iddi/Omy Krish (Kiongozi wa msafara) - Director
2. Omary Ntisi (Kamati ya ulinzi na usalama) - Brigedia DONNIE
3.Omari Saidi (Kijana cha Besha) - Mwenyeji wetu katika jiji la TANGA (MWARABU)
4. Saidi Bunduki (Mpiga picha & mwandishi wa makala hii
Makala hii itakuletea safari yote kuanzia Mbeya mpaka Tanga na matukio yote kwa picha na maelezo.
Tuliondoka Mbeya siku ya tarehe 22 / 12 / 2018 siku ya jumamosi. tuliondoka nyumbani majira ya saa 11 usiku. Lakini kama kawaida picha zilianza hapo nyumbani kama ilivyo ada.

Muda mchache kabla ya kuanza safari. Vijana wakiwa tayari kuondoka. Kutoka kushoto ni Omary Saidi, Omy Krish na Omary Ntisi.
|
Omary Ntisi (kushoto) akiwa na Omy Krish |
Kutoka kushoto ni Omy Krish, Saidi Bunduki na Omary Ntisi. |
Baada ya kuondoka nyumbani tulielekea stend kuu ya mabasi na hatimaye mnamo majira ya saa 12:09 asubuhi gari yetu ilianza safari (ABOOD BUS SERVICE)
Kwa ujumla tulikuwa watu wanne. Huyu bwana Omary Ntisi alikuwa ni mgeni wetu ambaye alitutembelea ndugu zake. Kwahiyo katika safari hii naye alikuwa anaelekea safari yake ya kurudi Arusha. Lakini kwa sababu sisi tulikuwa tunakwenda Tanga hivyo tukamuomba atupe Kampani mpaka Tanga kisha ataelekea Arusha, naye alikubali na kufanya hivyo.
Gari hii ilikuwa inafanya safari zake kati ya MBEYA na DAR, hivyo sisi tulipaswa kushukia Chalinze na kutafuta usafiri mwingine wa TANGA.
Saidi bunduki (wakwanza) akiwa na Omari Saidi - ndani ya BUS |
Omari Ntisi (kulia) akiwa na Omy Krish - ndani ya BUS |
Haya ni maeneo ya Ipogolo - Iringa |
Uoto wa asili katika hifadhi ya msitu wa mlima KITONGA |
Kwambali zikionekana safu za mlima kitoka, katika mkoa wa Iringa. |
Mnamo majira ya saa kumi na moja jioni tuliingia katika mji wa Morogoro. Kama kawaida tuliingia katika ofisi za ABOOD ili kufanyiwa ukaguzi kisha tuendelee na safari.
![]() |
Ofisi za ABOOD BUS maeneo ya morogoro mjini. Kutoka kushoto ni Omari Ntisi, Chuga Kabadshaa na bunduki.com - picha na KIJANA CHA BESHA |
Tulifika Chalinze majira ya saa mbili usiku. Kwamuda huo tulibahatika kupata gari ya kuelekea Tanga mjini. Ingawa kulikuwa na changamoto za hapa na pale lakini mwisho wa siku tulibahatika kuanza safari ya pili ya kuelekea Tanga.
Kwabahatiu mbaya safari hii ya pili hatukubahatika kupata picha za moja kwa moja kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu.
Tulifika Tanga mjini mnamo majira ya saa nane usiku.Tukaenda maeneo ya Besha ambako mwenyeji wetu alitupeleka huko.
Tulilala na asubuhi tulikuwa na ratiba kuu tatu
1. Kwenda NEMA kwa mzee saidi. Baba yake Omari Saidi
2. Kutembelea makumbusho ya mapango ya amboni
3. Kutembelea beach
usikose sehemu ya pili ambayo tutakuletea mtiririko wa matukio yote haya.
Asante.
bunduki.com
COMMENTS