MCHAGUA SANA

Mchagua sana huambukia Koroma

Kuna muda na wasaa, na kitambo hupitia
Majira usipojua, dakika zitapotea,
Ukija kuhesabiwa, masaa yemetimia,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !

Dahari hatukupewa, ni sekunde twaachiwa,
KIla zinapochepua, ngozi zetu zikavia,
Na pumzi huchelewa, mengi tukajichokea,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Bahati ikiwajia, bado wataichambua,
Kisha hujiinukia, mbele ikaendelea,
Halafu huangukia, pua zao kuumia,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Wa msimu huingia, upepo wa kulowea,
UKiisha wapepea, heri wakategemea,
Ukijawageukia, kama ukichaa huwa,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Wastani huachia, zaidi kukimbilia,
Huko akishaingia, nakisi huigundua,
Nyuma akigeukia, tayari kimetwaliwa,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Uzuri atachagua, akakuta walemaa,
Rijali akivizia, akakuta una waa,
Awe mme mke huwa, katika hii dunia,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Akili akifatia, huingia ukichaa,
Bora alichochagua, kikawa chamchachia,
Werevu akaezua,  mvi akajipambia,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Mali hukimbilia, uzani ukatitia,
Mbio hapo husanzua, kwingine kuelekea,
Hali akatarajia, atakuta iko sawa,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Huko akafumania, nayo yamejichachia,
Katikati hubakia, kama amenatishiwa,
Akiweza kujitoa, nusura huwa kulia,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Kikaango hukimbia, motoni akaingia,
Huruma hatoijua, hadi majivu akawa,
Huo mwisho wake kuwa, akaiaga dunia,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Ndivyo ilivyo dunia, ya mchezo na sanaa,
Saburi inaijua, kisha mkubwa wasaa,
Haraka haijaijua, ila napojifungua,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Unachokujionea, lenga hapo na kutua,
Kibakaika radhia, hatua utapotea,
Mwanangu binti kukaya, huu ni wangu wasia,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !


Sijisumbue kung'aa, huja kuwa ni balaa,
Mtake wako Jalia, ombilo kukuridhia,
Ibada mkiijua, yeye atawaangalia,
Kila mchagua sana, hubaki kuhangaika !

Shairi hili limenakiliwa kutoka MTANDAONI

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MCHAGUA SANA
MCHAGUA SANA
Mchagua sana huambukia Koroma
https://1.bp.blogspot.com/-XcT4xJONtLs/XvR_zzC3qsI/AAAAAAAAU8Y/ArVciAkNmsga-ZcKwoy1rORGiOhgOHaEQCK4BGAsYHg/w256-h181/SHAIRI%2B2.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-XcT4xJONtLs/XvR_zzC3qsI/AAAAAAAAU8Y/ArVciAkNmsga-ZcKwoy1rORGiOhgOHaEQCK4BGAsYHg/s72-w256-c-h181/SHAIRI%2B2.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2019/07/mchagua-sana.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2019/07/mchagua-sana.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content