Muandishi anawatoa dhana potofu baadhi ya watu kuwa kila anayeishi mjini maisha yake ni mazuri (Hapana)
Kulonga
ni yangu jadi, kwa beti zilo uturi
Atabisha
mkaidi, huku moyo una kiri
Kisa
kasema SAIDI, wacha niweke kiburi
SIO
KILA WA MJINI, ANA MAISHA MAZURI
Wanatamani
kurudi, wanaogopa hekari
Muda
ume taradadi, ndo mana wana ghairi
Si
ajabu kuritadi, na kutafuta tunguri
SIO
KILA WA MJINI, ANA MAISHA MAZURI
Jama
ipo mijeledi, chai ni alaasiri
Usiku
vuta uradi, kwa muhogo kachumbari
Ndo
maisha yamebidi, neno hili tafakari
SIO
KILA WA MJINI, ANA MAISHA MAZURI
Mjini
pesa juhudi, ndipo upate salari
Sam
taim mijeledi, unapoosha magari
Maisha
ni kama mwiba, ule wa msonobari
SIO
KILA WA MJINI, ANA MAISHA MAZURI