LIKIZO YANGU- august 2019 (sehemu ya KWANZA)

IMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA bunduki.com SEHEMU YA KWANZA (1) Hii ni likizo fupi ya mapumziko ya wiki mbili ambayo niliipata kwa vio...

IMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA bunduki.com

SEHEMU YA KWANZA (1)

Hii ni likizo fupi ya mapumziko ya wiki mbili ambayo niliipata kwa viongozi wangu wa kazi. Nayo ilikuwa ni baada ya sikukuu ya Iddi kubwa kuisha (IDD ALHAJJ). Kwakuwa familia yangu walikuwa wameshatangulia kijijini kwa ajili ya kujumuika pamoja na wazazi, ilinibidi safari ya kwenda niwe peke yangu.

Niliondoka mjini Mbeya majira ya saa 12 asubuji nikiwa katika basi la kampuni ya SAULI LUXURY COACH. Safari ilikuwa ya raha na salama bila changamoto zozote mpaka niliposhuka chalinze majira ya saa 11 jioni. Nilipata chakula kisha kutafuta gari nyingine ya kuelekea MKATA.

Hili ni basi la SAULI LUXURY COACH ambalo nililitumia katika safari toka Mbeya mpaka chalinze.

bunduki. com akiwa ndani ya Basi

Mnamo majira ya saa kumi nambili jioni nilianza safari namba mbili ya kuelekea Mkata ambapo nilifanikiwa kufika salama kabisa majira ya saa moja na dakika 55 usiku. Kwakuwa muda ulikuwa umekwenda sana nikaona ni bora nilale pale ili Mungu akijaalia kesho yake (jumanne) nianze safari namba tatu ya kuelekea kijijini kwetu Mkalamo.

 Kulipopambazuka nipata chai mgahawani na kuanza safari kwa kutumia usafiri wa pikipiki (boda boda). Nilifika Mkalamo saa tano asubuhi na kuikuta familia yangu pamoja na wazazi wangu wote wakiwa na afya njema na furaha na hamu kubwa ya kunisubiri. 

Ndugu jamaa na marafiki wote walikuwa na hamu dhidi yangu. Nilimshukuru Mungu kwa kuwakutat wote wakiwa vyema na wakiendelea na shughuli zao za kila siku.
Hii ni picha ambayo imepigwa wakati nikiingia kijijini kwetu MKALAMO

Hapa ni nyumbani kwetu kwa Sheikh Rashidi Samfyomi Bunduki

Likizo hii ilikuwa na lengo la kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki, waliopo Mkalamo na walioko nje ya Mkalamo kwa sababu ni wengi ambao hatujaonana kitambo. Miongoni mwa maeneo ambayo nilikusudia kufanya ziara ni pamoja na KWEDIHWAHWALA, MAGUNGA, KOMUNGU, KWAMSISI NA KWAMSENGA.

Siku ya jumanne na jumatano nilizitumia kwa kufanya shughuli za pale pale kijijini ikiwemo ni kuwasalimia walimu na wanafunzi wenzangu wa Madrasatil Maawa Mkalamo ya Handeni na kubadilishana mawazo ya hapa na pale.
Majengo ya Madrasa pamoja na msitiki. Mkalamo Handeni


Bunduki.com akiwa na baadhi ya wanafunzi wa Maawa

Baadhi ya wanafunzi wakike wa Madrasatil Maawa

Nilifarijika sana kuona Madrasa yetu imeendelea sana hasa katika uimarishaji wa majengo yake pamoja na majengo ya msikiti kama ambavyo umejionea hapo juu.

Siku ya Alhamisi tarehe 22 / 08 / 2019 nilianza ziara yangu kwa kuelekea Kwedihwahwala kwa ndugu zangu ambao tuliachana muda mrefu sana takriban miaka minne ilopita. Watu kama Adamu Bichuka, Mudi Kazungu, Juma mbanga, Rashidi Kingi na wengineo ni watu ambao muda mrefu hatujaonana hivyo nikaona ni bora kufunga safari na kwenda kuwasalimia. 

Lakini pia kwakuwa nami ni mpenzi wa ng’ombe (dufu) niliona hii ni fursa adhimu ya mimi kwenda kushiriki japo siku moja na vijana wenzangu katika suala hili la kumsifu mtume. 

Lakini pia nikaona sio vema kwenda peke yangu, hivyo nikaona ni vema niende na mke wangu na mwanangu mdogo (Ibrahimu) ili nao waweze kunipa sapoti katika safari yangu lakini pia nao wakawajuwe rafiki zangu.


Kutoka kushoto - Juma Mbanga,bunduki, Rashidi Kingi na Adamu bichuka

Kutoka Kulia - Juma Mbanga, Saidi Bunduki, Dula Mbanga, Rashidi Kingi na Adamu Bichuka

Nikiwa na baadhi ya vijana wenzangu wa Kwedihwahwala.

Ndugu zangu walinipokea vizuri sana sana lakini pia nilimkuta rafiki yangu Adamu bichuka akiwa amepatiwa zawadi ya mtoto mwingine mwingine mashaallaah hivyo safari yetu ilikuwa na neema

Siku ya ijumaa ya tarehe 23 tulianza safari ya kurudi nyumbani (Mkalamo) wenyeji walituandalia zawadi mbali mbali na kututafutia na usafiri wa kurudi mpaka kijijini kwetu. Safari yetu ilikuwa njema sana ALHAMDU LILLAAHI tulifika Mkalamo mnamo saa 6 na nusu mchana na kuiwahi swala ya ijumaa.
Maandalizi kabla ya kuondoka kurudi Mkalamo

Furaha ilikuwa ni sehemu kubwa ya maisha yetu. Mda mchache kabla ya kuondoka


Jioni ya siku ya ijumaa niliwaomba waalimu wa madrasa yetu pale mkalamo tufanye zoezi kidogo la burudani ya dufu angalau kidogo nikumbuke zamani. Basi nao bila khiyana walinikubalia na kufanya kama tulivopanga na jambo lilikwenda vizuri sana.
Hawa ni baadhi ya vijana wangu wa Madrasa Maawa Mkalamo Handeni. wakiwa na mwalimu wao Maneno.
Siku ya jumapili ni siku ambayo kulikuwa na shughuli ya maulidi ya kuwarehemu wazee wetu walotangulia akhera. Maulidi hayo yalipangwa kufanyika katika kijiji cha Magunga kata ya Kwamsisi Wilayani Handeni. Haya yalikuwa ni maulidi ya familia (ukoo) wetu ambayo siku za nyuma yalikuwa yakifanyika katika kijiji cha Komkonga. Hivyo basi ile likuwa ni fursa nyingine kwa upande wangu kwa ajili ya kuonana na ndugu na jamaa wengine badala ya kumtembelea mmoja mmoja kwake. Niliondoka asubuhi  na mama watoto tukielekea Magunga kwa ajili ya shughuli hiyo. Kutoka Mkalamo Mpaka kijiji cha Magunga ni mwendo wa takriban kilomita kumi tu hivi.Hapa shuguli ikiwa imeanza Rasmi.

Shughuli ikiwa wakati wa kiyamu.

Sheikh Hamis Samtoro akitoa mawaidha baada ya SHUGHULI kuisha.

Sheikh Samfyomi akiutoa mawaidha baada ya Samtoro kumaliza

Nilipanga kuanza safari ya kurudi Mbeya mnamo tarehe 28 lakini nilipewa taarifa ya uwepo wa Kikao kwa baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni yetu. Hivyo kwa kuwa tarehe za kikazo zilikuwa zimekaribia sana na kikao kilikuwa kifanyike Arusha, basi wakuu wa kazi wakasema ni bora nibaki mpaka tarehe 31 tukutane Arusha na kumaliza kikao kabisa na hatimaye kurudi Mbeya.

Hilo kwangu lilikuwa jambo jema.

Kwa leo nitaishia hapa, nitakuwa kuendelea na sehemu ya pili ambayo itahusisha safari ya kwenda Arusha na kurudi kwangu Mbeya.

Asante kwa kuwa nasi.

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: LIKIZO YANGU- august 2019 (sehemu ya KWANZA)
LIKIZO YANGU- august 2019 (sehemu ya KWANZA)
https://1.bp.blogspot.com/-DIPMs6QM7uw/XYnpxCDMltI/AAAAAAAAKJ8/ouXEvvArk_kct9ajJxjXzB4ihN1JPDs4gCLcBGAsYHQ/w498-h237/IMG_20190819_054803_4.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-DIPMs6QM7uw/XYnpxCDMltI/AAAAAAAAKJ8/ouXEvvArk_kct9ajJxjXzB4ihN1JPDs4gCLcBGAsYHQ/s72-w498-c-h237/IMG_20190819_054803_4.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2019/10/likizo-yangu-august-2019-sehemu-ya.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2019/10/likizo-yangu-august-2019-sehemu-ya.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content