Nilipokuwa mtoto kuna mambo niliyapenda sana, ila umri haukuruhusu.... Nadhani hapa nimeyataja baadhi yake......
Kuitika
marahaba, salamu toka kwa wana
Nazipendaga
si haba, nitaja nenepeana
Sidhani nitazishiba,
haitaja wezekana
Nitakuwa
kama baba, siku nikiwa mkubwa
Napenda kuheshimiwa,
nami niwe nakoroma
Napenda
kuamkiwa, kama afanyavyo mama
Chakula kupelekewa,
ninapokuwa kulima
Nikija kuwa
mkubwa, nitakuwa kama baba
Kukicha
alfajiri, huwahi kwenda ibada
Baada ya
adhkari, hufikia ule muda
Kuenda kuchoma
ngiri, hotel kwa mama ADA
Nikija kuwa
mkubwa, nitakuwa kama baba
Kisha hulinoa
panga, na kubadili mavazi
Miti kwenda
kucharanga, kwenye shamba la minazi
Kisha uji
wa karanga, hupewa bakuli shazi
Nikija kuwa
mkubwa, nitakuwa kama baba
Kisha jembe
mkononi, anza kung’oa visiki
Hata jua
halioni, baba kweli hashikiki
Muda wa
msikitini, ibada huidiriki
Nikija kuwa
mkubwa, nitakuwja kama baba
Napenda
pale mchana, mida ile ya chakula
Anavotuita
wana, na mama tujapo kula
Ukileta
uvulana, utachezea bakora
Nikija kuwa
mkubwa, nitakuwa kama baba
Kisha
hutupa mkazo, jioni ikiwasili
Hulitangaza
tangazo, kufika kumi kamili
Tuisitishe michezo,
madrasa kukabili
Nikija kuwa
mkubwa, nitakuwa kama baba
Vile napenda
ubwabwa, tanunua kilo saba
Kwenye sufuria
kubwa, ndi ndi ndi niweze shiba
Napenda kuwa
mkubwa, japo ukubwa suluba
Nikija kuwa
mkubwa, nitakuwa kama baba
Wazo hili nilikuwa nalo nikiwa na umri
chini ya miaka 10.
KWA WAPENZI
WA MASHAIRI TEMBELEA BLOG Yetu