LIKIZO YANGU- august 2019 (sehemu ya PILI)

IMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA bunduki.com SEHEMU YA PILI Hii ni likizo fupi ya mapumziko ya wiki mbili ambayo niliipata kwa viongo...


IMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA bunduki.com

SEHEMU YA PILI

Hii ni likizo fupi ya mapumziko ya wiki mbili ambayo niliipata kwa viongozi wangu wa kazi. Nayo ilikuwa ni baada ya sikukuu ya Iddi kubwa kuisha (IDD ALHAJJ). Kwakuwa familia yangu walikuwa wameshatangulia kijijini kwa ajili ya kujumuika pamoja na wazazi, ilinibidi safari ya kwenda niwe peke yangu.

Hii ni sehemu ya pili ambayo inahusiana na safari mbili ya Tanga - Arusha.

Tulianza safari rasmi kutoka Mkalamo na kuelekea  katika kijiji cha Mkata, ili siku inayofuata tuanze safari ya kuelekea Arusha na Hatimaye Mbeya. Nikiwa na familia yangu ambayo ni mke wangu na watoto wangu wawili. Tulianza safari siku ya alhamisi ya                           tarehe 29 / 08 / 2019. Tuliondoka Mkalamo kwa usafiri wa Basi la Kidato Bus Service. Tuliondoka Mkalamo majira ya saa tano asubuhi baada ya kusindikizwa na ndugu na jamaa mpaka stendi. Tulifika Mkata majira ya saa tisa jioni na kuelekea kwa mwenyeji wetu ambaye ni Ustadh Muhammad Bakari. Huyu bwana ni mwenyeji wangu wa muda mrefu sana tangu miaka ya 2011. Hivyo ni mara chache sana ambazo huenda Mkata na nisifike kwake na ni kwasababu maalum.
Tulikaa pale siku ile yote ili kusubiri siku ifuatayo na kuanza safari.

Kulingana na majukumu ya kikazi, niliataka familia yangu wao watangulie Mbeya kwa kupitia katika kijiji cha Ruvu ambako yuko dada yetu na kulala huko nami niende kuendelea na majukumu ya Kampuni na hatimae tukutane Mbeya. Hivo basi ilibidi siku ifuatayo wao waanze safari kuelekea Ruvu kwa dada Sofia nami nilianza safari ya kuelekea Arusha. Wakati nikielekea stendi nilikutana na vijana wangu ambao walikuwa wanakwenda masomoni Madrasa Dar es Salaam. Nikaona itapendeza kama nikipata nao walau picha (selfie)
Picha (kutoka nyuma) ikimuonesha Ustadh Muhammad akituongoza kuelekea stand.

Picha ikimuonesha Ustadh Muhammad na bunduki.com. Tukiwa katika harakati za kuisafirisha familia

Nikiwa na baadhi ya vijana wangu ambao walikuwa wanakwenda masomoni (Madrasa) Dar es Salaaam
Nilianza safari majira ya saa nne na nusu pale Mkata nikiwa na basi la "CHAKITO" ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam. nilifika majira ya saa moja usiku. Nilimsubiri ndugu yangu bwana Omy Krish ambaye yeye kwa siku ile alikuwa anatoka Mbeya kuja Arusha ambapo wote tulifika nyumbani kwao kwa Ustadh Hashim ambaye ni moja ya viongozi wakubwa wa Kampuni yetu ya Galaxy Computers. Bwana Omy krish alipokaribia kufika nilisogea maeneo ya stendi na kuweza kuelekea nyumbani pamoja. Kulipopambazuka asubuhi tulijiandaa na kuelekea HQ (MAKAO MAKUU) kwa ajili ya kukutana na kuianza safari ya kuelekea Kisongo kwa ajili ya semina.
Nikiwa na kiongozi HASHIM nje ya nyumba yake muda mchache
kabla ya kuondoka. (Picha na Omy Krishna)
Omy krish kabla ya kuanza safari ya kuelekea katika semina (Picha na bunduki.com)

Siku ya jumamosi, tarehe 31 / 08 / 2019 ndio ilikuwa siku rasmi ya Kikao ambacho tuliitwa kwacho. Kikao / Semina ile ilifanyika maeneo ya KISONGO ambako ni kama kilomita 30 kutoka Arusha mjini.

Omy Krish akitoa maelezo mafupi kwa waandishi wetu kuhusiana na semina hiyo elekezi
(Picha na bunduki.com)

Katika ukumbi rasmi wa Mkutano wa Galaxy katika shule ya sekondari ya Assalafi islamic
Kutoka kushoto ni Iyaka, Omy Krish, Bunduki.com, Kombo, Mohamed pamoja na Kasim
(Picha na mpigapicha wetu)Omy Krish akiwa na Ally Mote nje ya ukumbi wa Mkutano wakizungumza jambo
(Picha na bunduki.com)Muda wa chai - Omy krish (kulia) akiwa na bunduki
(Picha na Mohamed Iyyaka)

Semina yetu ilimalizika mnamo majira ya saa kumi jioni, baada ya hapo tuliamuriwa kuelekea makao makuu ambapo ni Arusha mjini kwa ajili ya mafunzo mengine ya muda mfupi.


Picha ambayo haina ubora sana ikimuonesha Omy krish akiwa maeneo ya Godown Galaxy computers (HQ)

Kasimu akielendelea na kuwaellimisha wafanyakazi wa Galaxy kuhusu
 baadhi ya spea za toner cartridge (Picha na bunduki.com)
Bwana Kasim akitoa darasa juu ya baadhi ya toner cartridge. (Picha na Bunduki.com)


Baada ya kupata mafunzo mafupi pale godown HQ, kiongozi wetu Sheikh Mubaraka aliamuru watu waelekee maeneo ya Ofisi mpya za Galaxy computers tawi la Arusha kumalizia shughuli za mwisho mwisho na kuweza kuondoka.

ZIFUATAZO ni picha zikionesha ofisi mpya ha Galaxi Arusha na baadhi ya wafanyakazi wakifurahia uwepo wao hapo


Kutoka kulia nia Kasim, Abuu na Omy krish.


Bunnduki.com akiwa na Kasim
Bunduki.com kulia akiwa na Bwana Bakari - wakiwa na furaha iliyo taradadi.


Baadhi ya wafanyakazi wa Galaaxy wakiwa nje ya ofisi.


Baada ya muda tuliruhusiwa na kwenda kupumzika kwani mpaka hapo tayari ilikuwa ni saa moja kama na nusu usiku.


Siku iliofuata ilikuwa ni jumapili, ingetakiwa siku ile turudi Mbeya lakini haikuwezekana kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu. Hivyo siku ile tuliitumia kwa ajili ya kutembea maeneo tofauti tofauti ya Jiji la Arusha. 

Utakutana na vijana mashuhuri na machachari waliozaliwa na kukulia Arusha wakiongozwa na BRIGEDIER DONLEY GUCKY(OGOPA SANA)

Kwa leo tuishie hapa katika sehemu hii ya pili ya likizo yangu.

Tafadhali usikje ukakosa sehemu ya tatu na ya mwisho ambapo bado tukiwa ndani ya jiji la Arusha (CHUGGA) na viunga vyake.

Shukrani za dhati ziwaendee wote walioshiriki katika kuhakikisha jambo hili linafanikiwa kwa namna moja ama nyingine.


COMMENTS

BLOGGER: 2


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: LIKIZO YANGU- august 2019 (sehemu ya PILI)
LIKIZO YANGU- august 2019 (sehemu ya PILI)
https://1.bp.blogspot.com/-Aj-gL_siDCM/XZWsaqY3sQI/AAAAAAAAKZ0/yqzCcGu_MKgZZsRSv28n-2Xeq2ArBXHxACKgBGAsYHg/s640/IMG_20190830_092803_2.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-Aj-gL_siDCM/XZWsaqY3sQI/AAAAAAAAKZ0/yqzCcGu_MKgZZsRSv28n-2Xeq2ArBXHxACKgBGAsYHg/s72-c/IMG_20190830_092803_2.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2019/11/likizo-yangu-august-2019-sehemu-ya-pili.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2019/11/likizo-yangu-august-2019-sehemu-ya-pili.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content