WATER FALLS TOUR (B) Katika sehemu hii tutaangalia jinsi gani vijana wazalendo walijitolea kutembelea vivutio vilivyoko ndani ya nchi ...
WATER FALLS TOUR (B)
Katika sehemu hii tutaangalia jinsi gani vijana wazalendo walijitolea kutembelea vivutio vilivyoko ndani ya nchi yao.
Hapa safari ilikuwa imebaki sehemu fupi kiasi lakini ilikuwa nayo na changamoto kadhaa za kushuka kwenye milima yenye msitu mkubwa na mawe mengi.
Safari hii ya pili iliongozwa na Kijana ambaye tulimkuta maeneo yale. Jamaa yule aliacha kazi zake na kuamua kutupeleka mpaka huko chini kabisa iliko WATER FALLS
Huu ni uwanda wa mahala ambapo tulikuwa tunaelekea. |
Msafara wa kushuka bondeni kuelekea WATER FALLS ukiendelea kwa sehemu ya pili. |
Omy krish kulia akiwa na Kijana wake Mujide Khan katika harakati za kushuka mteremko mkali. |
|
Kwa mbali wakionekana washiriki wakiwa katika harakati za kushuka mlima kuelekea huko Mtoni. |
Baadhi ya eneo la uoto wa misitu ya kijani eneo hilo |
Baada ya muda wa takriban dakika ishirini tulifanikiwa kufika katika ule mkondo wa maji na kuanza kupandisha upande wa juu kwa ajili kuyatafuta maanguko hayo ya ajabu. Changamoto ambayo ilitukusumbua sana ni maji kuwa na baridi kali kiasi kwamba kutembea bila viatu ilikuwa ni shida kubwa ingawa haikuwa na budi.
Omy Krish akiwa katika baadhi ya maeneo ya mto |
Baada ya muda mchache hatimaye tulifika eneo tulilokusudia. Vijana walionesha kuwa na furaha sana, pamoja na changamoto ya baridi kali lakini haikuwa shida sana. Vijana walendelea kuchukua picha na video kwa ajili ya kumbukumbu.
Kutoka kushoto ni Donley Gucky, Omy Krish na Fahad |
Saidi R Bunduki |
Kiongozi wa msafara mzima OMARI NTISI (Donley Guck) |
![]() |
Furaha tele ndani ya WATER FALLS |
Haya ndio maporomoko ya maji (Mount meru Water Falls) |
Baada ya kumaliza safari yetu tuliamua kurudi nyumbani kuendelea na majukumu mengine. Bado tulikuwa na yule mwenyeji wetu ambaye alitupeleka mpaka kule.
Kwa kuwa kulikuwa na njia nyingine ya mkato ya kurudi jamaa alitushauri tutumie hiyo, lakini pia kwa kuwa watu wote walikuwa wamechoka sana tulikubaliana kupita njia hiyo ambayo tungefika kijiji jirani kwa haraka na kupata usafiri wa boda boda mpaka Arusha mjini.
Mlima wa wakati wa kurudi nao ulikuwa mkubwa sana japokuwa si kama wa kwanza lakini uliwachosha sana wadau wetu.
Ngedere juu ya mti ndani ya msitu wa Mount Meru. |
Uchovu ukichukua mkondon wake kwa baba la baba (The Chugga Kabadishaa) |
Katika msitu ule kulikuwa na mandhari murua sana yenye kuvutia, miongoni mwa mandhari hiyo ni msitu mnene wa miti ya mitiki ambayo humburudisha yeyote mwenye kuutazama. Bunduki.com imeona isikuache hivihivi, ikuletee kidogo mandhari hii nawe angalau uweze kuburudisha macho yako.
![]() |
Picha ya pamoja wakati tukikaribia Kijiji jirani. |
Maeneo ya msitu wa mitiki |
Tulipomaliza shamba/msitu ule wa miti mingi, hatimaye tulifika nyumbani kijijini ambapo tulipumzika na kupata supu ya ng'ombe. Furaha nyingine ilipatikana pale maeneo ya Mgahawani watu wakiwa wakijipongeza baada ya mateso ya muda mrefu. Lakini pia tuliwakuta baadhi ya wananchi wa eneo lile ambao nao walikuwa wakipata huduma nyingine za vyakula na vinywaji.
Wakati wa kusubiri huduma ya chakula mgahahawani |
Wakati wa kusubiri supu, tukijipongeza na kufurahia baadhi ya video na picha zetu za matukio |
Baada ya kumaliza kula, boda boda zilikuwa zipo tayari kwa aji ya kuanza safari yetu ya kurudi Arusha mjini. Ili kupunguza gharama tulichukua boda boda 3 ili kila moja wapande abiria wawili. Pikipiki ya kwanza alipanda Mujahid na Victor, piki piki ya pili aliweko bwana Omy Krish na Donley Guck, wakati boda boda ya tatu tulikuwa mimi na bwana Fahad.
![]() |
Mda mchache kabla ya kuondoka |
![]() |
Tukiwa katika usafiri kurudi Mjini. |
Hatimaye mnamo majira ya saa 12:40 jioni tulifanikiwa kurudi mjini na kuendelea na majukumu mengine ya hapa na pale.
Na huu ndio ulikua mwisho wa safari yetu hii ya Kihistoria ya kutembelea moja ya vivutio vya watalii katika Mkoa wa Arusha. Asante sana kwa kufuatia makala zetu.
Na huu ndio ulikua mwisho wa safari yetu hii ya Kihistoria ya kutembelea moja ya vivutio vya watalii katika Mkoa wa Arusha. Asante sana kwa kufuatia makala zetu.
WASHIRIKI
OMARI NTISI - Muongozaji (Mwenyeji)
OMY KRISH - Director (Kiongozi wa Msafara)
FAHAD (Galaxy man)
MUJAHID (Mujide Khan)
VICTOR CHRISS
SAIDI BUNDUKI (Mwandishi na Kiongozi wa mtandao wa
'bunduki MEDIA'
ASANTE KWA WOTE WALIOSHIRIKI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE
imedhaminiwa na;-
GREEN TASTE
Wauzaji na wasambazaji wa juisi ya matunda JIJINI Arusha
COMMENTS