ADABU ZA KUSOMA QUR AN

Adabu za kusoma Quran

Qur ani ni kitabu kitukufu na ndio muongozo wa maisha ya muislamu, hivyo tunatakiwa kuijua, na kujua maana yake kwa undani kabisa. Tukiachana na kuijua, lakini pia tunatakiwa kuisoma mara kwa mara ili kupata mazingatio ambayo yanapatikana ndani yake. Hivyo ni wajibu wetu sisi ambao bado hatujajua kusoma Quran kufanya jitihada zozote kadiri ya uwezo wetu ili kuhakikisha nasi tunakuwa miongoni mwa wenye kukijua kitabu hiki cha Mwenyezimungu.

Ingawa ulimwengu wa sasa tumetekwa sana na shughuli za kidunia, lakini bado tunayo nafasi kupitia mitandao yetu mbali mbali ya kijamii kuhakikisha tunapata elimu za bure ambazo hupatikana huko mitandaoni na hatuna sababu ya kulikwepa hili mbele ya Allaah.

Kwa uchache kabisa, leo nimekuandalia adabu za kuisoma Qur ani. Hizi ni miongoni mwa adabu nyingi za kukisoma kitabu cha Allaah.


1. Stara
Unatakiwa kujisitiri kama sheria inavyosema. Sheria inautambua uchi wa mwanaume kuwa ni sehemu ambayo ipo kati ya kitovu na magoti. Na uchi wa mwanamke kuwa ni mwili wake wote isipokuwa uso na viganja vya mikono. Hivyo basi unatakiwa wakati wa kusoma Qur ani ni lazima uhakikishe umejistiri ipasavyo.

2. Twahara
Twahara ni kuwa msafi wa mwili na mavazi. Hii inamaanisha kuwa ni lazima mwili wako uwe msafi, usiwe na janaba, uwe na udhu, na pia nguo zako ama mahala ulipo pasiwe na najisi yoyote kama vile mkojo, mavi, matapishi, damu na kadhalika.

3. Kuvaa vizuri
Qur ani ni mawasiliano ya moja kwa moja na Mola wako, hivyo inapendekezwa uvae vizuri ujipambe vizuri, ukae sehemu nzuri na kadhalika. Kama ambavyo unapokwenda kuzungumza na watu wakubwa wa kidunia ni lazima ujiandae, je unaonaje unapokwenda/unapotaka kuzungumza na Mola wako aliyekuumba?.

4. Kuelekea kibla
Ni sunna unapokaa kwa ajili ya kusoma Qur an uelekee Qibla. Ingawa unaweza kuelekea popote lakini ni bora zaidi kukaa kwa heshima na kuelekea huko.

5. Kuisoma kwa sauti nzuri
Kila mtu ana sauti yake ambayo amejaaliwa na ALLAH lakini tumehimizwa kusoma kwa sauti ambayo itakupendeza wewe mwenyewe lakini pia hata anaye kusikiliza. (kama yupo)

6. Kuzingatia maana yake
Qur an ni kitabu ambacho kinatakiwa kisomwe na kuzingatiwa maana zake na kufanyiwa kazi ipasavyo ama kupata mazingatio kwa visa mbali mbali vilivyomo humo. Hatutakiwi kusoma tu kama magazeti ya udaku.

7. Utulivu
Hakikisha wakaati unasoma Qur ani lazima uwe na utulivu. Kusiwe na kitu ambacho kitakushughulisha ama kushughulisha akili yako, mfano redio, simu, watu n.k. Kwani ni rahisi kuzisafirisha hisia zako na kukutoka katika maana.

8. Kusoma kwa mpangilio mzuri
Ni vizuri kusoma katika mpangilizo mzuri, sura hadi sura / aya hadi aya nyingine ili kupata maana kamili. Sio kuruka ruka bila sababu yoyote.

9. Kuuweka msahafu mahali palipo juu
Kama unaisoma Qur an kwa kutazama, basi inatakiwa kitu hicho unachokitumia kusomea kutokiweka chini. mfano unatumia msahafu, ubao au simu yako n.k. Shika/pakata kitu hicho katika njia nzuri, kwa mikono yako au kwa mkono wako wa kulia (ikiwezekana) au kuiweka juu ya kitu kingine.

10. Kuisoma kwa usahihi
Inatakiwa kuzingatia usomaji na kuipa kila herufi haki yake. Mfano kuvuta (mada), kukaza (shadda) kusimama na kuunga sehemu zinazostahili.

11. Kunyamaza inaposomwa
Mwenyezimungu amesema katika Qur ani kuwa "Inaposomwa Qur an basi nyamazeni"
Hivyo unapoisikia Qur ani inasomwa basi nyamaza. Haijalishi kuwa inasomwa kutoka kwa mwenzako uliyenaye, au unaisikia katika chombo kingine. Mambo wayafanyayo baadhi ya watu ya kupiga  kelele na nderemo pindi inaposomwa Qur an HAYAFAI.

12. Kumlaani sheitwani
Mwenyezimungu amesema katika Qur ani kuwa "Unaposoma Qur ani basi taka hifadhi kwa Mwenyezimungu kutokana na sheitwani aliyelaaniwa" Hivyo tunatakiwa tuanze kwa kusema  "Audhu billaahi minash shaitwaanir rajiiim. ili Mwenyezimungu atukinge na shari ya shetani wakati wa kusoma kitabu chake Kitukufu.

13. Kuomba dua baada ya kumaliza
Basi kwa kumalizia tu ni bora ukaomba dua baada ya kumaliza kusoma Kitabu hiki kitukufu. Kumuomba Mwenyezimungu akujaalie kuifuata na kuifanyia kazi sambamba na kuacha makatazo yake. Kama tujuavyo kuwa yaliyomo katika Qur ani ndio DINI yenyewe.

Haya ni baadhi tu ya mambo nimejaribu kushea nanyi elimu hii kwa uchache. Kama una nyongeza au masahihisho juu ya hili basi tuwekee hapo chini sehemu ya comenti au unaweza kututafuta katika mawasiliano yetu.

MWENYEZIMUNGU NDIYE AJUAYE ZAIDI, Hakuna mkamilifu ila ni yeye TU.

TUNAMUOMBA ALLAAH atulaajie tuwe ni wenye kusikiliza yaliyo ya kheri na kuyafuata, na atujaalie tuwe ni wenye kuyaacha makatazo yake

AAMIN

Imeandaliwa na kuchapishwa na SAIDI BUNDUKI
COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: ADABU ZA KUSOMA QUR AN
ADABU ZA KUSOMA QUR AN
Adabu za kusoma Quran
https://1.bp.blogspot.com/-cs7fdJ6xm4A/XkknUEGmZzI/AAAAAAAAQsI/Eq-jq-4wu-oQXguIqN_m0eQPamWvPhaFgCLcBGAsYHQ/s400/quran-fact-1080x530.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-cs7fdJ6xm4A/XkknUEGmZzI/AAAAAAAAQsI/Eq-jq-4wu-oQXguIqN_m0eQPamWvPhaFgCLcBGAsYHQ/s72-c/quran-fact-1080x530.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/02/adabu-za-kusoma-qur-an.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/02/adabu-za-kusoma-qur-an.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content