MAMBO 13 USIYOYAJUWA KUHUSU VIRUSI VYA CORONA NA NAMNA YA KUJIKINGA NAVYO
USISAHAU KUSHEA NA MWINGINE ELIMU HII.

1. virusi vya corona si virusi vigeni duniani. Historia inathibitisha kuwa virusi hivi ni mara ya pili kujitokeza nchini China na kusambaa katika nchi kadhaa. Na si china tu pia vilishawahi kutokea Saud Arabia na kusambaa nchi kadhaa. Virusi hivi ni katika virusi vinavyo huambukizwa kutoka  kwa wanyama kama popo, ngamia, paka na samaki.


2. Virusi vya corona (CoV) viligundulika toka miaka ya 1960. Virusi hivi vimetambulika kwa kuwa ni katika virusi vinavyoathiri mfumo wa upumuaji, na pia wakati mwingine huweza kuathiri mfumo wa chakula (gastrointestine). toka kuanza kugundulika maradhi yaletwayo na virusi hivi mwaka 2003 zaidi ya watu 1600, wameshafariki.

3. Hivi miaka ya karibuni virusi hivi vimeanza kuchukuwa sura ya zoonotic virus yaani virusi ambavyo vinaweza kusambaa kutoka kwa wanyama kwend kwa biadamu na kusababisha maradhi. Mwaka 2003 ugonjwa utambulikao kama SARS yaani Severe Respirator Syndrome na kuuwa zaia ya watu 800 na mwaka 2012 ugonjwa uitwao MERS yaani Middle East Respirator Syndrome na kuuwa yapata watu 800. maradhi yote haya yanasababishwa na virusi vya corona.

4. Virusi hivi vya corona vipo katika aina nyingi, miongoni mwa aina hizo ni kama:- Betacoronavirus ,HCoV-OC43 na HCoV-HKU1 na pia Alphacoronavirus HCoV-NL63 zote hizi ni aina za virusi vya corona ambavyo vinaweza kuathiri binadamu na kusababisha homa ya mafua. Kwa pamoja virusi hivi vyote husababisha matatizo katika mfumo wa kupumulia ama mfumo wa chakula.

5. Virusi hivi vya corona mpaka kufikia sasa vimeweza kusababisha maradhi kadhaa kama vile;-            SARS-CoV (2002) uliosababishwa na virusi vya corona aina ya Betacoronavirus                       (kundi la Sarbecovirus) na ugonjwa wa MERS-CoV (2012 unaosababishwa na virusi vya corona aina ya Betacoronavirus kundi la Merbecovirus). na mwishoni mwa mwaka 2019 ugonjwa mwingine umeibuka unaosababishwa na virusi vya corona. Ugonjwa huo unafahamika kama 2019-nCoV nao una mahusiano makubwa na ugonjwa wa SARS ambao husababishwa na virusi vya corona aina ya Betacoronavirus kundi la Sarbecovirus.

6. Neno corona asili yake ni neno la kilatini lenye maana ya taji kwa lugha ya kiingereza ni crown. Virusi hivi vimepewa jina hili kwa kuwa vinafanana sana na umbo la taji. Na virusi hivi vinatoka kwa wanyama kama samaki, popo, ngamia, paka na wanyama wengine na kusambaa kwa binadamu. Virusi hivi vinaweza kusambazwa kwa njia ya hewa ama kugusana kutoka mtu na mtu.

7. Itambulike kuwa kugusana huku kunaweza kusababisha kama tu virusi hivi vitaweza kuingia mdomoni au puani. Yaani unaweza kumgusa mgonjwa na usipate. Ni kwamba endapo mgonjwa atapiga chafya virusi husambaa kwenye hewa, na endapo mtu mwingine vikimpata na kuingia moja kwa moja mdomoni ama puani anaweza kupata virusi. Ama endapo virusi vitaingia mkononi mwa mtu na bila ya kuosha mikono akala kitu ama akajigusa mdomoni ama puani hapa ataweza kupata virusi hivi.

8. Endapo utamgusa mgonjwa kwa mkono na ukapata virusi hivyo na ukajigusa pua ama mdomo bila ya kunawa basi ni rahisi kuvipata virusi hivi. Pia vinaweza kukaa kwenye mavazi kwa kuwa vinasambaa hewani na endapo mavazi yale yataweza kugusana na mdomo ama pua hapa pia mtua ataweza kupata virusi.

9. Unaweza kupata virusi hivi kutoka kwa mgonjwa kwa kupitia hewa kwa umbali wa futi sita kutoka kwa mgonjwa. Mgonjwa akikohoa ama kupiga chafya mamilioni ya virusi husambaa hewani. Ni vyema kwa mgonjwa kujiziba kwa mguo ama kitambaa na si kwa mkono. Pia kama upo katika eneo lililo athirika katu usijizibe kwa mikono unapopiga chafya. Ukikosa basi tumia hata nguo yako uliyoivaa.

10.  Tafiti bado zinafanyika kutafuta dawa ama chanjo lakini mpaka sasa hakuna dawa maalumu wala chanjo ya virusi hivi. Kuna njia za kujilinda na virusi hivi kama vile kutumia mask za kuziba pua na mdomo, sambamba na njia hizi zipo njia njingine kama:-

A. Kuosha mikono kabla kula kwa maji yanayochirizika japo kwa sekunde 20
B. Kutokuingiza chochote mdomoni hata kama ni kidole bila ya kukiosha kwa maji yanayochirizika japo kwa sekunde 20
C. Ukikosa maji unaweza kutumia kimiminika maalumu chenye alcohol.

11.  Baada ya kupata virusi hivi na kuingia mwilini vinaweza kukaa kwa muda wa siku 3 mpaka 14 kabla ya kupata dalili za ugonjwa huu. Dalili za ugonjwa wa virusi vya corona ni homa inaweza kuwa na mafua, kukohoa na kushindwa kupumua vyema. Wakati mwingine virusi hivi vinaweza kuathiri mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kitaalamu hutambulika kama gastrointestine. Dalili zinaweza kuendelea na hali kuwa mbaya zaidi na hata mgonjwa kupoteza maisha.

12.  Kwakuwa hakuna tiba ya magonjwa haya ya virusi vya corona hii haimaanishi kuwa anayepata virusi hivi atafariki. Hii si kweli kwani zipo tiba za kupunguza dalili hizi na hata kuondoa japokuwa hakuna dawa maalumu ya magonjwa haya. Pia itambulike kuwa yapo magonjwa mengi ya virusi ambayo bado hayana tiba lakini haimaanishi kuwa anayepata virusi hivi atakufa.

13.  Virusi vya corona si virusi pekee vyenye asili yake kwa wanyama, hata HIV asili yake ni kwa wanyama ndipo vikaja kwa binadamu. Pia vipo virusi vingi mbavyo vinasambazwa na mbu na kusababisha homa kali na maradhi mengine na hata kupelekea vifo. Virusi vya ZIKA ni mojawapo ya aina za virusi ambavyo husambazwa kwa mbu.

USIACHE KUSOMA POSTI ZIFUATAZO:
Vyakula vya vitamini

Utayapata masomo hayo kupitia katika blog yetu ya BONGOCLASS, bonyeza link hii hapa chini.


Usiache pia kutembelea makataba yetu ya vitabu ili upeta kusoma bure vitabu vya afya na burudani, hadithi na chemshabongo buree. Bofya hapa kuingia kwenye makataba yetu bila ya kujisajili, upate kuona vitabu vyetu. Bonyeza link hapa chini.


N.B
Rudi tena ukurasa huu upate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu afya, usisahau pia kusubscribe kwenye chanel yetu ya youtube bunduki.com 

COMMENTS

BLOGGER: 2
  1. sildenafil 100 mg is used to treat erectile dysfunction in men. sildenafil 100 mg is used to treat erectile dysfunction or impotence in men. This medicine can be used as per the advice of the doctor. The store is utilized to sell the best prescriptions at reasonable costs.

    ReplyDelete


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: MAMBO 13 USIYOYAJUWA KUHUSU VIRUSI VYA CORONA NA NAMNA YA KUJIKINGA NAVYO
MAMBO 13 USIYOYAJUWA KUHUSU VIRUSI VYA CORONA NA NAMNA YA KUJIKINGA NAVYO
https://1.bp.blogspot.com/-2ghiIf2Vmbw/Xjwx5M3txgI/AAAAAAAAOkw/l5_BbcvMbbkijmierFQsujxp8M7hdEu8wCLcBGAsYHQ/w640-h318/CORONA2.png
https://1.bp.blogspot.com/-2ghiIf2Vmbw/Xjwx5M3txgI/AAAAAAAAOkw/l5_BbcvMbbkijmierFQsujxp8M7hdEu8wCLcBGAsYHQ/s72-w640-c-h318/CORONA2.png
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/02/mambo-13-usiyoyajuwa-kuhusu-virusi-vya.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/02/mambo-13-usiyoyajuwa-kuhusu-virusi-vya.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content