nukuu za dini
KUPATA SAADA YA ALLAAH

Naiusia
nafsi yangu pamoja na kuwausia ndugu zangu waislamu katika Suala zima la kumcha
Allaah Subhaanahu wataala. Leo nitawaletea nukuu tano ambazo zitamfanya
Muislamu kupata saada ama wema wa Maisha hapa duniani na kesho Akhera. Saada ni
amani, utulivu na Baraka katika maisha na huko Akhera ni pepo ya Allaah.
Yaogope ya haramu
Utakuwa mchamungu mbele ya watu)
(a) Mche Mungu kwa kuyaacha mambo ya haramu ambayo ameyakataza.
(b) Mche Mungu kwa kuyaendea kwa pupa mambo yote aliyoyaamrisha.
Wacha mambo maovu si kwa ajili ya
kuwaogopa / kuwahofia wanadamu. Usiwache madhambi kwa sababu ya kumuogopa bosi
wako, mke wako, mume wako ama jamii iliyokuzunguka “HAPANA”. Jua kwamba
Mwenyezimungu anakuona na ipo siku atakuadhibu adhabu kali kwa dhambi
unazozifanya.
Ridhika na kichache (ulichonacho) -
(Utakuwa tajiri)
Mtume anasema kuwa ‘Utajiri si wingi wa mali, bali utajiri ni
utajiri wa nafsi yaani Kuridhika.
Tunatakiwa kuridhika na kichache ambacho tumejaaliwa na Allaah katika hali zetu na mali zetu kwa ujumla. Na
siku zote ili uweze kumshukuru Mwenyezimungu kwa ulichonacho katika mali basi
mtazame wa chini yako, usimtazame tajiri ama mtu mwenye mali nyingi kuliko
wewe.
Mpende Jirani yako
(Utakuwa Muumin)
Siku hizi tumekuwa tukizijali nafsi zetu na familia zetu tu, kitu
ambacho Bwana Mtume Muhammad hakufanya hivyo. Ukiamka walau mjulie hali jirani
yako, Mjue kama ana shida ambayo utaweza kumsaidia umsaidie, Ukila hakikisha na
jirani yako naye amekula walau kwa uchache. Tunaishi na majirani kama maadui
kwa sababu tumekuwa ni watu wa kusengenyana, kutukanana, kusemana vibaya baina
ya jirani na jirani. Unasubiri jirani yako apate shida ili umcheke. HAPANA hii haiko
sawa ndugu zangu watukufu waislamu. “TUMCHE ALLAAH katika hili.”
Penda apate mwenzako jambo ambalo inapenda nafsi yako
Tuombeane dua, tutakiane kheri kutoka katika nafsi zetu na sio
kunafiki. Wewe umejaaliwa kazi (kazi nzuri) basi Jitahidi na ndugu yako
kumtafutia chochote ambacho naye anaweza kuishi vizuri. Kama huna uwezo basi
muombee dua kwa Allaah katika ibada zako. Basi hakika nawe Allaah hatokusahau
katika mambo yako.
Usikithirishe (Usizidishe) kucheka
(Kuzidisha kucheka huuwa nafsi)
Moyo (nafsi) unakufa na unakuwa mbali na Kumkumbuka Mwenyezimungu. Htujaambiwa
tusicheke bali tumeambiwa tucheke kwa kiasi.
HITIMISHO
Nimejaribu kunukuu mambo haya matano ili niwafikishie nanyi ndugu
zangu katika Iiman. Tunamuomba ALLAAH atuongoze katika ibada zake na mambo yote
ya kheri na atuepushe na yote aliyoyakataza.
Mwenyezimungu ndiye mjuzi zaidi
Imesimuliwa
na SHEIKH;- IBRAHIMU OMARI BOMBO
Imeandikwa
na SAIDI RASHIDI BUNDUKI.
Kutoka
masjid Baraa bin Azib
MBEYA MJINI (ISANGA)
COMMENTS