SITOSAHAU - (AJALI)

Mishale ya saa kumi na moja alfajiri tukiwa tumelala fofofo. Ghafla nilisikia mlio wa ubapa wa panga likigonga kwa nguvu katika nguzo ya kibanda chetu. Jamaa alikuwa anatuamsha kwa ghadhabu na hasira akisema "AMKENI AMKENI, watu wamekufa wote. Amkeni jama".


Ilikuwa ni takriban kama siku ya tatu tangu tuende kule shambani kwa mwalimu ambako tulikuwa tukipalilia mahindi pamoja na mihogo maeneo ya Kijiji cha Mkanyageni njiani ukielekea Muheza kutoka Tanga. Wakati huo nilikuwa katika madrasa ya Shamsul maarifi jijini Tanga mwaka 2010.

Nikiwa ni miongoni mwa wanafunzi sita ambao tulichaguliwa na moja ya waalimu wetu kwa ajili ya kwenda kumsaidia kazi ya kupalilia mahindi shambani. Nyuma yetu tuliwaacha wenzetu wakijiandaa na safari ya kwenda katika hafla ya maulidi Kijijini Kibafuta njia ya kutoka Tanga kuelekea Mombasa. Walifanikiwa kwenda salama safari ile lakini Mungu alitupa mtihani kwani wakati wanarudi ile gari waliokuwa wakisafiri nayo ilipata ajali eneo la Mabanda ya papa (round about) Tanga mjini.

Taarifa ile ilitukuta tukiwa kule shambani na tulifikishiwa na mwanafunzi mwenzetu ambaye alikuwa anaishi kule kule shambani (mbali kidogo na tulipo). Yeye alipigiwa simu kutoka Mjini kuwa gari ile (fuso) waliokuwa wakisafiria iliacha njia na kupinduka eneo Hilo wakati Dereva alipokuwa akijaribu kuizungusha gari katika mzunguko ule wa barabara      (round about) na hatimae gari kupinduka na kuwafunika wanafunzi wengi ambao baadhi yao walikufa palepale na wengine wengi kujeruhiwa. Zaidi ya wanafunzi kumi na sita walifariki na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa wakiwemo waliovunjika mikono.

"Tukiwa tumelala katika kibanda chetu huko shambani, mishale ya saa kumi na moja alfajiri tukiwa tumelala fofofo. Ghafla nilisikia mlio wa ubapa wa panga likigonga kwa nguvu katika nguzo ya kibanda chetu. Jamaa alikuwa anatuamsha kwa ghadhabu na hasira akisema "AMKENI AMKENI, watu wamekufa wote". Amkeni jama". Tulipoamka jamaa alitueleza kuwa wenzetu waliokuwa wakitoka Kibafuta walifariki. Kwakuwa hakuwa na taarifa rasmi na akili ilikuwa imeshachanganyikiwa hakujua kwa haraka haraka kuwa ni watu wangapi walikuwa wamefariki. Lakini alisisitiza kuwa watu wamefariki wengi mno.

Tulianza kujiandaa muda huo ili kurudi mjini. Tulipofika eneo la tukio mida ya saa 4 asubuhi, tulishuhudia umati wa watu wakiwa wamejaa eneo lile, ajali ilitokea usiku majira ya saa 8 usiku.

Wakati ule (asubuhi) majeruhi walikuwa hospitali ya Mkoa wa Tanga (Bombo). Kwakweli ilikuwa ni siku ya huzuni sana ambayo sijawahi kuishuhudia maishani mwangu kabla, hasa pale ambapo tunawaona ndugu zetu waliokufa wakiwa hospitali, na majeruhi wakiwa katika hali mbaya.                Daah kwakweli ni siku ambayo katika maisha yangu sitoisahau milele. Nikiwakumbuka rafiki zangu wa karibu ambao nilikuwa nao siku chache wakiwa wamefariki. Nikishuhudia wenzangu niliowaacha wakiwa wazima leo wakiwa wamepoteza viungo vyao? Madrasa nzima ilikuwa ni vilio na simanzi.

Narudia tena sitoisahau siku hii katika maisha yangu.

Mungu awalaze pema waumini wote wake na waume, na awape shifaa wagonjwa wote walioko majumbani na hospitalini (AAMIN)

Tukutane jumamosi nyingine kwa visa na mikasa ambayo haitosahauliwa katika maisha ya binadamu.


JE?
Una kisa au mkasa wowote? shea nasi kisa hicho.

FANYA HIVI;-
Weka Komenti yako hapo chini au wasiliana nasi katika namba zetu zilizoko katika sehemu ya "contact" chini kabisa ya blog hii.ASANTECOMMENTS

BLOGGER: 5


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,28,Dini,98,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: SITOSAHAU - (AJALI)
SITOSAHAU - (AJALI)
https://1.bp.blogspot.com/-4yVinYzS4SI/Xz_GQRuTAMI/AAAAAAAAXVE/6AHhdtslPf4lQY_DXVg05rWoQ42LzJgIgCLcBGAsYHQ/s0/mfano%2Bhai.png
https://1.bp.blogspot.com/-4yVinYzS4SI/Xz_GQRuTAMI/AAAAAAAAXVE/6AHhdtslPf4lQY_DXVg05rWoQ42LzJgIgCLcBGAsYHQ/s72-c/mfano%2Bhai.png
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/02/sitosahau-ajali-ya-fuso.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/02/sitosahau-ajali-ya-fuso.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content