KWANINI DUA ZETU HAZIJIBIWI?

Kwanini dua zetu hazibiwi?Dua ni katika ibada tunazotakiwa tufanye kila siku. Allah amesha ahidi kwenye quran kuwa "Tukimuomba kwa hakika atatujibu dua zetu", na ahadi ya Allah katu haivunjiki. Lakini kumekuwa na maswali ya kujiuliza ni kwa nini dua zetu hazijibiwi?, ama ni kwa nini maombi yetu tunayoomba hatupati mafanikio? Je ni kitu gani tunakikosea, au Allah ana watu wake maalumu?, kama ndivyo ni kwa nini amesema tumuombe watu wote?. makala hii itakwenda kujibu maswali haya yote.

Makala hii imendikwa na Al-Ustadh Rajabu Athuman na kuchapishwa na Sayyid Bunduki kutoka mr.bunduki.com. Unaweza kutuunga mkono kwa kuishea makala hii. Tunafanya kazi hii kwa ajili ya Allah na si vinginevyo, tafadhali wasiliana nasi kwa haraka ukiona kuna kosa, ama ukiwa na ushauri. Pia usisahau kupata makala nyingine za dini hapa.

Mpenzi msomaji kwanza tambuwa kuwa huenda ikawa dua uliyoiomba imekwisha kujibiwa bila ya wewe kujua, ama tena Allah amekukuwekea malipo zaidi ya kukupa hicho ulichoomba. Sasa lamda kwanza tuone njia ambazo dua hujibiwa.


Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema مَا مِنْ أَحَدٍ يَدْعُو بِدُعَاءٍ إِلاَّ آتَاهُ اللَّهُ مَا سَأَلَ أَوْ كَفَّ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهُ مَا لَمْ يَدْعُ بِإِثْمٍ أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ ‏"‏ “ “mtu yeyote anayeomba dua ila atajibiwa ima awahishiwe kujibiwa hapahapa duniani, au acheleweshewe (kujibiwa hapa duniani na badala yake ) ajibiwe akhera au asamehewe madhambi yake  kwa kiasi kile alichoomba.

Kwa mujibu wa hadithi hii tunajifunza kuwa dua hujibiwa katika njia kuu tatu ambazo ni:
i. Kupewa kile ulichokiomba.
ii. Kwa kufutiwa madhambi.
iii. Kujibiwa siku ya qiyama kwa kupewa kilichobora zaidi.

Kwa ufupi ni kuwa unaweza kukawa umeomba na usipate ulichokitaka, na kwa kuwa Allah anataka kukupa kilicho bora zaidi, hivyo Allah badala ya kukupatia ulichoomba atakufutia madhambi ama kukucheleweshea hadi siku ya Qiyana ama kukupa ulichokiomba hapa duniani ijapokuwa kitachelewa. Kwani Allah anakupa kilichobora kwa wakati ulio sahihi zaidi.

2. Pia wakati mwingine dua zetu hazijibiwi kwa sababu ya kutokufuatia masharti ya dua. 

Kwa kutokufuata masharti ya dua huenda dua isikubalike ama ichelewe kujibiwa. Hebu kwa haraka tuone baadhi tu ya masharti ya dua. Kama ilivyo ibada nyingine basi itambulike kuwa hata dua zina masharti na adabu zake. Miongoni mwa masharti ya dua ni :-

i. Kujiepusha na mambo yaliyo haramu. Ukitaka dua zako zijibiwe kwa haraka basi jiepushe na mambo ambayo Allah ameyakataza. Mambo ya haramu katika kauli na vitendo. Vipi dua yako itajibiwa wakati Allah anakuchukia kwa kufanya matendo ya haramu?.

ii. Kuchunga adabu za dua; dua zina adabu zake kama ilivyo ibada nyingine. Hakikisaha unafata adabu zote za dua.

iii. Sifa za dua yenyewe. Vi vyema kuzijua sifa za dua iliyo bora, kwani unaweza ukawa unaomba dua kumbe unaingia kwenye SHIRKI. Kwa hakika Allah hatakukubalia dua yenye SHIRKI ndani yake.

iv. Kuchunga nyakati na mazingira ambayo yanazunguuka dua yenyewe. Kwa hakika Allah hawezi kuikubali dua inayoombwa katika maeneo ambayo yanamuasi Allah. Basi muombaji ahakikishe anaiomba dua yake katika mazingira yaliyo salama kiimani, yaliyo safi kulingana na wakati alionao  Muombaji.

v. Kuwa twahara; atakayeomba dua akiwa amevaa mavazi machafu na yenye najisi sio sawa na yule atakayeomba akiwa na mavazi yaliyo safi na nadhifu. Hivyo kuwa twahara ni katika masharti yanayotajwa kuwa ni masharti ya dua.

3. Kutokuharakisha maombi: 

Unapoomba dua haitakiwi sasa uwe unamlaumu Allah na kusema “nimeomba lakini sijajibiwa” haya maneno ni katika maneno ya kukatia tamaa. Hairuhusiwi kulalamika kuwa hujajibiwa, unachotakiwa ni kuwa mvumilivu na kusubiria siku ambayo Allah atakujibu dua yako.

Kwa mujibu wa hadithi nyingi na zilizo sahihi nyakati zifuatazo zinanukuliwa kuwa Allah hujibu dua kwenye nyakati hizo:-
1. Theluthi ya mwisho ya usiku
2. Baada ya swala za faradhi
3. Kati ya adhana na iqama
4. Wakati wa kusujudi
5. Muda wa kukutana majeshi kwenye vita vya jihadi
6. Siku ya Ijumaa

1. Kuelekea kibla
2. Kunyanyua mikono juu
3. Kuanza dua kwa kumshukuru na kumsifu Allah na kumswalia mtume
4. Kuanza kuomba kua kwa kujiombea mwenyewe kama unataka kumuombea mtu mwingine
5. Kurudia rudia katika maombi
6. Kuwa na yaqini juu ya kujibiwa
7. Usiharakishe kujibiwa.
8. Kuitikia Aaamin

Kwa nini makafiri dua zao hujibiwa

Kuna swali la msingi la kujiuliza kama ndivyo kama tulivyoona hapo juu, sasa ni kwa nini makafiri dua zao hujibiwa, na wakati mwingine waumini dua zao hazijibiwi?. kabla ya kulijibu swali hili kwanza tuone hadithi ifuatayo:-

Amesimulia Jabir رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “Hakika (Malaika) Jibril ndiye aliyepewa kazi ya kutekeleza haja za wanaadamu, basi pindi mja kafiri anapoomba dua Allah husema kumwambia Jibril ‘ewe Jibril mpe haja yake kwani mimi sipendi kusikia dua yake. Na pindi anapoomba dua Mja muumini Allah humwambia Jibril ‘ewe Jibril izuie haja yake (usimjibu dua yake) kwani mimi napenda kusikia dua yake’”. )amepokea Ibn Najar).

Hivyo Allah anaweza kumjibu kafiri kwa kuwa hapendi sauti yake akimuomba, hivyo anampa kwa ajili ya kumziba mdomo. Allah anapenda waumini wamuombe, na anafurahi sana pindi akiombwa, hivyo huzuia na kuchelewesha majibu ya muumini ili aendelee kumuomba. Pindi muumini asipojibiwa dua yake kwa kupewa anachokitaka hufutiwa madhambi ama kuekewa mpaka siku ya qiyama alipwe kilichobora zaidi kya kuliko kile alichoomba.

SHIRKI KATIKA DUA

Kama tulivyokwisha kuona kuwa unaweza kufanya shirki katika dua, yaani kuna aina ya shirki ambazo hupatikana katika dua. Unaweza kufanya shirki katika hali zifuatazo:
1. Kuomba dua kwa asiyekuwa Allah kwa mfano kuomba mizimu, mashetani na makaburi
2. Kuomba dua kwa waliokufa kama kuomba Mitume, Manabii, Waja wema, Wazazi waliokufa
3. Kutilia shaka kwa uwezo wa Allah katika kufanya chochote.

HITIMISHO
Nduguyangu Muislamu, tunafanya kazi hii kwa ajili ya Allah, na hakuna anayetulipa kwa kazi hii. Tafadhali tuunge mkono kushea na kusambaza makala hii kwa waislamu wengine ama kwa kuongeza maarifa na elimu kwenye makala zetu, ama tutumie makala ama shea na wengine makala hizi. Unaweza pia ukajiunga kwenye maktaba yetu kwa kubofya hapa

Darsa nyingine kwa ajili yako:-

COMMENTS

BLOGGER: 2


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: KWANINI DUA ZETU HAZIJIBIWI?
KWANINI DUA ZETU HAZIJIBIWI?
Kwanini dua zetu hazibiwi?
https://1.bp.blogspot.com/-N2NqUUVhQJ0/XmCjuXHhJPI/AAAAAAAAOo0/v1cjyMoqXuwfczxKmT49Mlvt_Q8a4UytQCLcBGAsYHQ/s400/dua.webp
https://1.bp.blogspot.com/-N2NqUUVhQJ0/XmCjuXHhJPI/AAAAAAAAOo0/v1cjyMoqXuwfczxKmT49Mlvt_Q8a4UytQCLcBGAsYHQ/s72-c/dua.webp
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/03/kwanini-dua-zetu-hazijibiwi.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/03/kwanini-dua-zetu-hazijibiwi.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content