KWANINI ZINAA HULETA UFUKARA?

Zifahamu kwa uchache aina za ufukara unaoletwa na UZINIFU.

KWANINI / KIVIPI ZINAA HULETA UFUKARA?

Kila sifa njema anastahiki Mwenyezimungu Mola wa viumbe vyote

Nadhani Tulishazungumzia kwa kina juu ya swala za zinaa, maana yake na madhara yake katika jamii. Kama mada hii ilikupita bofya HAPA. Moja katika madhara hayo ilikuwa ni kuleta ufukara.

Unaweza kujiuliza kivipi zinaa inaweza kuleta ufukara? Mbona watu wengine ni matajiri na wanaendelea na dhambi hii lakini bado utajiri wao uko pale pale? Leo nitakujia na ufafanuzi kidogo juu ya jambo hili.

Endelea;  • Ufukara uliozungumziwa hapa unaweza ukawa katika njia nyingi, lakini nimejitahidi kueleza njia mbili. Iko njia ya moja kwa moja na ipo njia isio ya moja kwa moja ambayo huweza kujitokeza baada ya muda mrefu

1. UFUKARA KATIKA HALI YA KAWAIDA

Katika hali ya kawaida hapa kila mtu atakuwa shahidi juu ya hili kuwa pindi unapotaka kutimiza jambo lako la zinaa ni lazima kuna gharama zitumike ili uweze kufanikisha. Gharama hizi zinaweza kutofautiana baina ya mtu na mtu ama eneo kwa eneo. Wacha tujaribu kuzichambua kwa uchache;-

MAHALI / ENEO

Wengi katika wazinifu huwa wanatumia njia nyingi kuweza kujificha katika macho ya watu ili wasionekane na wanadamu wakati Huo Muumba wa Mbingu na ardhi anawaona. Hapa ni lazima watu wakodi eneo maalum. Eneo hili laweza kuwa nyumba ya wageni (Guest house) ama sehemu yoyote ile iliyombali na macho ya wanadamu.Mwengine anaweza kusema kuwa hahitaji kwenda Gest, Anatumia geto lake, ama sehemu nyingine ya bure kama vichaka n.k. Hii gharama yake inawea kukugharimu zaidi ya hivyo unavofikiria. Tutaelezea kwa namna yake siku nyingine Ishaallaah.


POSHO

Zinaa imejengwa sana sana katika ujira / malipo. Hasa  kwa wale ambao wameoa / kuolewa lakini wanaendelea na jambo la hili nje ya ndoa zao.

Wanawake wengi ambao wakijua umeoa watakuwa wanakutumia kama njia ya kukuingizia kipato. Hasa kama ukiwa ni mtu mwenye uwezo wa kifedha. Hapa utakuwa unamhudumia huenda zaidi ya vile ambavyo unamhudumia mkeo. 

Kama unabisha fanya uchunguzi.

Kuna mtu atasema kuwa mwanamke wake (mchepuko) huwa hahitajii pesa katika mahusiano yao. Basi ukiona hivyo lazima ufahamu mambo mawili  •    .Yuko ambaye anachunwa hiyo (badala yako) na wewe unatumika kama sehemu ya starehe tu. Lakini dhambi hii nayo haitokuacha salama kwani nawe ipo siku utakuja kuchunwa pesa na kupewa mwanaume mwingine. ZINAA NI DENI                                                                                                                                                                                    
  • .     Huenda mwanamke huyo bado anakuvutia kasi ili akija kukupiga mzinga unakuwa mzinga haswa ambao unaweza kukuyumbisha kiuchumi katika shuguli zako kama sio kukufilisi kabisa.


FAINI


Hapa ni pabaya zaidi katika hili, najua huenda hujaelewa hii faini ni nini?
Wacha nikupe mfano.


Mtu mmoja alikuwa anafanya zinaa na mke wa mtu mwingine. Jamaa mwenye mke alipozipata habari zile aliamua kumuwekea mtego wa kumnasa. Mtego ule ulifanikiwa. Baada ya kukamatwa jamaa alitakiwa kulipa pesa nyingi sana ambazo zilimpelekea kuuza kila kitu chake nakubaki kama alivyo. Na baada ya hapo jamaa walimfanyia kitu kibaya zaidi ya ile faini aliyolipa.

Hali kadhalika mifano iko mingi sana hata kwa wale ambao walibainika kuwa wanatembea na wanafunzi, hatima na miishilio yao haikuwa mizuri, wengine walijikuta wakiwa jela na kupoteza kila kitu chao na wengine walijikuta wakisalimika na jela lakini kwa kulipa nakuhonga marundo ya pesa.

Mwisho wa siku wanajikuta kule kule katika suala la ufukara ambao umezungumzwa na Mtume Muhammad Swallalaahu Alaihi wasallam

zipo gharama nyingi sana katika suala hili, hapa nimetaja chache lakini pia papoja na hayo kuna vitu kama usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, chakula, mavazi n.k.

Kila mmoja ana gharama zake tofauti. Sasa hebu piga gharama hizo kwa siku halafu jumlisha mara mwaka mzima au miaka mitano ni shilingi ngapi? 

Je? pesa hiyo ungeamua kuiweka katika kujikwamua kiuchumi leo hii ungekuwa wapi? 

Je? kama ungeamua kuisaidia familia yako ungepata thawabu kiasi gani?

Kuna watu leo hii wanakufa hospitalini kwa kukosa shilingi elfu tano tu ya dawa (Unalijua hilo?)

Kuna mwenzako analalana njaa kwa kwa kukosa shilingi elfu mbili ya unga na fungu la mchicha 

HUU NI MFANO WA MASWALI KADHA WA KADHA AMBAYO UNATAKIWA UJIULIZE

TAFAKARI!!!!


2. UFUKARA KATIKA HALI ISIO YA KAWAIDA

Hapa katika point hii ndio inawafikia moja kwa moja wale ambao wanaona kuwa zinaa kwao si tatizo kwa sababu wanadanganywa na shilingi chache walizo kuwa nazo. Wanadanganywa na uwezao walionao wa  kubadili mboga, chakula, nguo, magari na nyumba. Hebu tuone na hapa kwa uchache;-
NDOA ZISIZO TARAJIWA

Suala hili lina mchango mkubwa wa kusababisha ufukara katika namna ifuatayo. Umefanya zinaa na mtoto wa watu kwa muda mrefu, labda ukaja ukafumaniwa na kuozeshwa. Ama wakati wa mahusiano yenu akajifanya kuwa ni mke mwena kuona kuwa anafaa kuolewa nawe. Ukaja ukamuoa bwana

Sasa mziki unakuja pale anapokuwa ndani ya ndoa na kuonesha hali yake ya kawaida ambao ulikuwa huijui (tabia yake mbaya), Hapo unaweza kupata mfadhaiko wa moyo na kuweza kupoteza dira nzima ya maisha yako na kushuka sana kiuchumi ama kufanya kazi zako nje ya kiwango kinachotarajiwa.

Ama tena inawezekana ikawa mwanamke yule si wa kheri kwako ukajuta kuwa naye ama akakupelekea msongo wa mawazo ambao unaweza kuja kukutia tena katika janga la zinaa mpya kwa ajili ya kutafuta faraja ambayo kamwe hutoipata.


VITOTO VYA ZINAA


Unajua bwana, maisha ni marefu sana, matokeo mengi ya zinaa ni mimba zisizo tarajiwa (Ukiachana na ndoa zisizo tarajiwa kwa baadhi ya watu)

Madhara haya huonekana baadaye sana hata baada ya mtoto kukua na kuwa mkubwa. Mtoto yule anaweza akaja kukudhuru wewe mzazi kwa namna moja ama nyingine. Suala hili mifano yake iko wazi.

Unajiuliza mbona wengine wanawalea watoto wao wa zinaa vizuri na baadaye wanakuja kuwasaidia? Jibu ni kwamba huwa tunaangalia juu juu katika hili. Lakini huenda kukawa na undani ambao umejificha sana ambao mimi na wewe hatuujui. Lakini kwa kujaribu kulizungumzia hili ni kwamba kwanza watoto wengi wa zinaa husingiziwa baba na hulelewa na baba ambao sio halisi. Jambo ambalo nibaya zaidi ya unavofikiria

Lakini pia kama tunavyojua kuwa mtoto wa zinaa hua harithi pale ambapo inayesemekana kuwa ni baba yake amefariki. 

Hapa mzazi anaweza kuchukua jukumu la kumgawia mali yake kabla yuko hai ili pale ambapo atakufa basi asihesabiwe. Hii ubaya wake ni kwamba inaweza ikaleta tafrani kubwa kwa watoto walio ndani ya ndoa na hatimaye kusababisha madhara makubwa zaidi.

Madhara hayo ni kusambaratika kwa familia na kukosa mshikamano na hatimaye ni kuangukia kule kule katika jambola ufukara.

HITIMISHO

Hakuna mjanja juu ya kuiepuka dhambi hii ila ni kwa msaada wa Mwenyezimungu. Kwa ambao walishakosea tunamuomba Mwenyezimungu awasamehe na wasirudie tena. Kwa ambao wamebahatika kutoingia katika dhambi hii Mwenyezimungu awabariki sana na awaepushie vishawishi na shetani na awatafutie wenzi walio wema.

Mimi si mjuzi wa elimu ya dini, hivyo pale ambapo nimeteleza basi Mwenyezimungu anisamehe na anijuze vilivyo ndivyo.


MWENYEZI MUNGU NDIYE MJUZI ZAIDI

Unaweza pia kupitia masomo hayaCOMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: KWANINI ZINAA HULETA UFUKARA?
KWANINI ZINAA HULETA UFUKARA?
Zifahamu kwa uchache aina za ufukara unaoletwa na UZINIFU.
https://1.bp.blogspot.com/-x5WcIkIsRV4/YAqRInOH2AI/AAAAAAAAbyA/KX3vd7aMlsAuYVAKtRPSvyWYeGghrw8mACLcBGAsYHQ/w237-h158/111.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-x5WcIkIsRV4/YAqRInOH2AI/AAAAAAAAbyA/KX3vd7aMlsAuYVAKtRPSvyWYeGghrw8mACLcBGAsYHQ/s72-w237-c-h158/111.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/03/kwanini-zinaa-huleta-ufukara.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/03/kwanini-zinaa-huleta-ufukara.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content