Mtunzi amekumbukwa na vijana wenzake wa kijijini kwao baada ya kuondoka kwa muda mrefu. Lakini akasema jamani ndugu zangu "Nitarudi Sijauwa"
Huenda mwanikumbuka, ndugu yenu niko hai
Sasa ni kumi miaka, Nimewapa bai bai
Bado hawajanizika, Afya tele sipo moi
Nitarudi sijauwa
Maisha yaso kanuni, sikupenda kuwa mbali
Ni mipango ya manani, Alopanga hii hali
Nimekumbuka nyumbani, hasa kupiga matari
Nitarudi sijauwa
Yaendaje michakato, Sina shaka mko vema
Bado yapita Kidato? Ama ilikwisha buma?
Nilowaacha watoto, Sasa ni watu wazima
Nitarudi sijauwa
Sasa ni kumi miaka, Nimewapa bai bai
Bado hawajanizika, Afya tele sipo moi
Nitarudi sijauwa
Maisha yaso kanuni, sikupenda kuwa mbali
Ni mipango ya manani, Alopanga hii hali
Nimekumbuka nyumbani, hasa kupiga matari
Nitarudi sijauwa
Yaendaje michakato, Sina shaka mko vema
Bado yapita Kidato? Ama ilikwisha buma?
Nilowaacha watoto, Sasa ni watu wazima
Nitarudi sijauwa
Walimu pale shuleni, sana nimewakumbuka
Sijui
wapo kazini?, Mwinyipingu na Mashaka
Na vipi utamaduni, lile goma la MANGAKA
NITARUDI
SIJAUWA
Nimezimisi boribo, msimu umeshafika?
Na
omari ungarobo, yupo au kaondoka?
Ila habari za KIBO, ninazo nahuzunika
NITARUDI
SIJAUWA
Nasikia kumekucha, umeme ulishafika
Vipi
Mahamudu kocha, Star bado yawika?
Ni muda nimewaacha, leo nimewakumbuka
NITARUDI
SIJAUWA
Kumbe sasa mambo poa, reli wameirudisha
Safari
zetu za Dar, Moshi mpaka Arusha
Maana ilichakaa, kambi zote
zilikwisha
NITARUDI
SIJAUWA
Msalimieni Shida, wakumuita Madaba
Nisalimieni Meda, sijamsahau Jeba
Salamu ziwafikie.
Mpeni hai Mbonea, pamoja na Jua kali
Na Tajiri Mungu pia, Kifudu na fundi Ali
Salamu ziwafikie.
Salamu zende kwa Ponji, Timba, babu
Kanchele
Na babu Ali wa Zenji, Na Mzee Kaburule
Salamu ziwafikie.
Kafobe, Deko na Nyese, Mwetambara na
Mbagurwa
Mitumba, Moshi, Chikwese, na yule baunsa
Kurwa
Salamu ziwafikie.
Hapa mwisho piga nyundo, ni mwisho natia
nukta
Mpeni hai Mfundo, Basi ALLAAH ATALETA.
Salamu ziwafikie.