NJIA 6 ZA KUMUEPUKA SHEITWANI

Kumuepuka shetani

"Audhu billaahi minashhaitwaanir Rajiiim"

Nataka ifadhi (Najikinga) kwa Mwenyezimungu kutokana na Sheitwani aliyelaaniwa (Aliyeko mbali na Rehma za Mwenyezimungu)


Bismillahir Rahmaanir Rahiim

(Kwa jina la Mwenyezimungu Mwingi wa rehma mwenye kurehemu)

Katika harakati za kuamrishana MEMA na kukatazana MABAYA, leo nakuja na nukuu fupi juu ya suala zima la kujiepusha na sheitwani katika shughuli na maisha yetu ya kila siku. Nkukumbushe tu ndugu yangu muislamu kuwa mimi sio mjuzi sana wa elimu ya dini,hivyo pale ambapo utakutana na mapungufu basi wasiliana nami haraka kwa kubofya HAPA au unaweza kuweka maoni yako sehemu ya comment

Watu wengi wakisikia habari ya sheitwani moja kwa moja wanafikiri kuwa moja kwa moja ni JINNI, lakini ukweli ni kwamba sheitwani anaweza kuwa mwanadamu au jinni, huyu ni kiumbe ambaye anakushawishi katika kuacha mambo mema na anayekuamrisha katika kufanya mambo maovu. 'Anaamrisha Maovu na kukataza mema' Tukiachana na nafsi zetu – hili tutakuja kulizungumzia siku nyingine namna gani ya kujiepusha na vishawishi vya nafsi. Leo nitajitahidi kuzungumza nawe njia sita nyepesi ambazo kwa uwezo wa Allaah tunaweza kufanikiwa kujiepusha na Sheitwani na kuweza kuepuka maasi ambayo tumekatazwa.

Tambua kuwa Sheitwani yupo

Katika njia rahisi ya kuweza kupambana na adui yeyote kwanza ni lazima ujue kwa dhati kwamba yupo, na ikiwezekana ujue namna ya utendaji kazi wake na ujue udhaifu wake. Hivyo jambo muhimu kabisa ni kujua kuwa huyu shetani yupo, na ni lazima ujue kuwa yupo shetani wa ki jini ambaye haonekani lakini pia yupo shetani wa kibinaadamu ambaye ananonekana na anaweza kuwa mtu yeyote katika walio kuzunguuka. Baada ya kujua sasa fanya mbinu hizi kumuepuka na kutokukuingiza katika masuala ya madhambi.

1.   Yajue ya haramu

Nafikiri iko wazi kuwa kila mtu anayajua mambo ambayo ni haramu ambayo Allaah amekataza tusifanye. Hivyo unatakiwa kuyatambua kutoka ndani ya nafsi yako na kujua kuwa kuyafanya haya ni makosa makubwa. Hii ifanye iwe ni sehemu yako ya maisha ya kila siku. Kabla hujafanya jambo / kuzungumza chochote ni lazima upime katika mizani ya dini kuwa ni haki kufanya au LAA.

2.   Zijue adhabu za AllaahYJH7

Soma, sikiliza, uliza na ufahamu  juu ya adhabu atakazo adhibiwa mtu mwenye kufanya maovu. Jua kuwa Mungu yupo na adhabu zake ni kazi na zipo kwa ajili ya yeyote ambaye atakiuka mipaka yake.

3.   Tambua madhara ya kila ovu. Duniani na akhera

Tambua madhara ya kila ovu ambalo unakusudia kulifanya. Kila ambalo limekatazwa ujue lina madhara kuanzia hapa duniani na kesho Akhera.
Mfano ni jambo la ZINAA jambo hili madhara yake yako wazi kabisa kuanzia EDChapa duniani na kesho akhera. Tulijaribu kueleza madhara ya zinaa kwa uchache kwa hapa duniani. Kama mada hii uliikosa unaweza kupitia hapo chini kabla ya kuendelea.


4.   Tambua umuhimu wa Kumcha Mungu
Mche Mungu, mtaje Mungu kila wakati, tambua kuwa Mungu anakuona kila nukta ya maisha yako. Wengi wetu tunasali na kufunga tu kwa kufuata mkumbo hatujawa na imani thabiti kwRTFGVBa Allaah. Hivyo tunapaswa kumjua Mwenyezimungu kwa kina kabisa ili tukijue kile tunachokifanya.

5.   Isome na uisikilize sana Quran

Si wote tunaweza kuielewa Quran na maana yake, lakini sote tunatakiwa kuisoma, kuisikiliza na kufuata yaliyomo Najua uko bize sana na dunia yetu ya leo lakini jaribu kutenga muda walau wa dakika 30 ndani ya siku nzima ujaribu kupitia maneno haya matukufu ambayo ndio muongozo wa Muislamu (QURAN). Na kama sehemu yako ya kazi pana utulivu jitahidi sana badala ya kusikiliza muziki basi usikilize Quran/mawaidha. Siku hizi pia ulimwengu umekuwa rahisi kusoma Quran sio mpaka uwe na Msahafu, Quran unaweza kuipata kwenye simu na kwa lugha yako wewe ambayo unaelewa na unaweza kusoma maana na tafsiri yake kwa urahisi kabisa.

6.   Msimamo binafsi

Baada ya kuyajua hayo kuwa na msimamo wewe kama wewe, usiwe mwepesi kushawishiwa na kitu kingine kama nafsi na mtu mwingine. Ingawa nafsi nayo hua inaamrisha maovu muda mwingine, unatakiwa kuidhibiti kwani hata sheitwani wa kijini anapotaka kukushawishi hupitia katika nafsi yako.

HITIMISHO

ALLAAH anasema katika Quran “Hakika Sheitwani kwenu nyinyi ni adui nasi tunatakiwa tumfanye kuwa ni adui”

Na kwa kumalizia tu naweza kusema kuwa yote hayo yanahitaji subira ya hali ya juu sana. Kwani katika hali ya kawaida mambo ya maasi yamepambwa sana na yanavutia katika macho ya mwenye kutazama ma katika masikio ya mwenye kusikiliza. Mfano mdogo tu ni vishawishi ambavyo tunaviona katika sehemu mbali mbali za maisha yetu, makazini, barabarani, majumbani n.k. Lakini pia maasi yamepambwa sana katika masikio ya mwenye kusikiliza mfano ni nyimbo na mambo mengine ya upuuzi. Kiukweli kabisa hakuna atakaye toka katika mabano haya ila ni kumtegemea sana Mwenyezimungu na kuazimia hasa katika hilo.

KWANINI?

Kwa sababu tumekuwa ni Umma bora, kwakuwa tunaamrishana mema na kukatazana maasi. Hivyo jukumu hili sio la mashekhe peke yao bali ni la kila mmoja. Kwa kuwa nami ni mmoja katika Umma huu bora nimeona niitumie fursa hii kuwaeleza jambo hili. Kama utapata wasaa   nawe ni bora ukashea na mwingine walau kwa uchache aipate elimu hii.

Makala hii fupi imeandaliwa na kuandikwa na Saidi Bunduki kutoka katika mtandao wa mrbunduki.com


MWENYEEZIMUNGU NDIYE MJUZI ZAIDI


Baadhi ya Darasa muhimu zilizopita

Salaat Al istikhaara
Adabu za kusoma Qur ani
Maana ya swala 

COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: NJIA 6 ZA KUMUEPUKA SHEITWANI
NJIA 6 ZA KUMUEPUKA SHEITWANI
Kumuepuka shetani
https://1.bp.blogspot.com/-qMZeFC-R7HQ/XxAj-6ePIJI/AAAAAAAAWR8/285RgOR4gG80ITlLBXiVZf8l882qarGkwCLcBGAsYHQ/w234-h128/censer-2949641_640-300x200.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-qMZeFC-R7HQ/XxAj-6ePIJI/AAAAAAAAWR8/285RgOR4gG80ITlLBXiVZf8l882qarGkwCLcBGAsYHQ/s72-w234-c-h128/censer-2949641_640-300x200.jpg
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/03/njia-6-za-kumuepuka-sheitwani.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/03/njia-6-za-kumuepuka-sheitwani.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content