SALAT AL-ISTIKHARA NA FAIDA ZAKE

SALAT AL-ISTIKHARA

Salat al - istikhara ni sala ya kuomba muongozo wa Jambo lolote lile kwa Mwenyezimungu.

Kuna muda mwanadamu unaweza kukabiliwa na maamuzi magumu ambayo katika akili yako binafsi ni ngumu kuamua kufanya /kuacha - kuchagua A au B. Ukiachana na maamuzi ya kawaida labda hapa nilipo mvua inanyesha ngoja nisogee / Njaa inauma ngoja nikanunue chakula n.k.
HAYA TUNASEMA NI MAAMUZI MADOGO AMBAYO NI MAISHA YA KILA SIKU


Maamuzi ambayo tunayazungumzia hapa ni kwa mfano unaweza ukawa umekusudia kufanya biashara fulani, lakini hujui mwishilio wake utakuwaje. Ama umetafutiwa au unataka kutafuta mchumba MUME/MKE lakini hujui itakuwaje katika maisha yenu. Hapa ni lazima kutaka ushauri wa jambo hilo kwa Mwenyezimgu ambaye yeye ndiye mjuzi wa mambo ya baadaye na mambo ya ghaibu (mambo yaliyofichikana)

Kwa kukosa hilo, watu wengi wamejikuta wakiangukia mambo Mabaya na waliobahatika wamejikuta wakibahatika kupatia (bila kuwa na uhakika)

ALLAAH anasema katika Qur an (Surat Al baqara - aya ya 216)
"NA HUENDA MKACHUKIA KITU NACHO NI KHERI KWENU, NA HUENDA MKAPENDA KITU NACHO NI SHARI KWENU, NA MWENYEZIMUNGU ANAJUA NA NYINYI HAMJUI"

Aya hiyo inatufahamisha kuwa binadamu ni mwenye uwezo mdogo katika kujua mambo. Mara nyingi anaweza kutamani kitu hali ya kuwa hakina kheri kwake na anaweza kuchukia kitu na kumbe kikawa na kheri kwake. Mjuzi wa mambo ni yeye mwenyewe ALLAH Muumba mbingu na Ardhi na vilivyomo.

Mtihani tulionao waislamu ni kwamba leo tumeacha mafundisho ya dini yetu tukufu ikiwemo mafundisho kama haya si wengi wenye kuyajua. Ndio maana nimeona nitoe nukuu hii leo kwa ufupi sana kwa ambao watabahatika kupitia hapa wanaweza kushea na waislamu wenzao. Na Mwenyezimungu atujaalie tuwe ni wenye kusikiliza yalio ya haki na kuyafuata na kuyaepuka yaliyo baatil.

Tunapokuwa katika SALA huwa tunasoma Suratul Fatiha, na tunaposoma Suratul fatiha huwa tunasema "WEWE TU NDIYE TUNAYEKUABUDU, NA WEWE TU NDIYE TUNAYEKUOMBA MSAADA" Basi ndugu yangu Muislamu moja katika msaada ambao tunatakiwa kuomba kwa Mungu ni huu yaani Salaat al istikhara. Ili mtu asiangukie katika majuto, iwe ni ndoa, safari, kazi, biashara, kufunga mkataba ama maamuzi yoyote magumu katika maisha.

Amesema Mtume Muhammadi (Rehmn na amani ziwe juu yake)
"Ikiwa yeyote miongoni mwenu anafikiria kufanya jambo lolote, na aswali rakaa mbili tofauti na sala ya faradhi na aseme baada ya sala"


Inasomeka hivi;-

"Allaahumma Innii astakhiruka bi ilmika, waastaqdiruka biqudratika, wa as aluka min fadhlika aladhiim. Fainnaka taqdiru walaa aqdiru, wataalamu walaa aalamu, wa anta allaamul ghuyuub

Allaahumma inkunta taalamu anna haadhal amru___ khairulii fii diiniii wamaashii waaqibatu amrii au aajil amrii waajilihii, faqdirhu lii wayasarhulii, thumma baarik lii fiih.

wainkuta taalamu anna haadhal amru___ sharrulii, fii diiniii, wamaashii waaqibatu amrii, au aajil amrii wa aajilihii, faswrifhu annii waswrifunii anhu waqdirlia alkhaira haithu kaana thumma arllwinii bih"

HII hapo juu NDIO DUA YA ISTIKHARA

ZIADA
Imependekezwa baada ya kumaliza swala kabla ya kusoma dua hiyo hapo juu, basi ni bora utangulize dhikri hizi

1. "Astaghfirullaahi (mara 100 au zaidi")

2. "Subhaanallaah, walhamdulillaah, walaailaaha illallaahu Allaahu akbaru, walaa haula walaa
      quwwata illaa billaahi al aliyyul adhiim (mara 11 au mara 100 - ukiweza)

  • Baada ya adhkari hizo mbili ndipo utasoma dua hiyo maalum ya Istikhara, kisha unapofika katika tamko linalosema (Hadhal amru___ utalitaja jambo lako.
  • Swala hii huswaliwa wakati wowote, lakini ni bora ukaiswali baada ya swala ya INSHA
  • Dua ya istikhara ni kama dua nyingine, hivyo lazima tufuate nidhamu za dua.


MAMBO YA KUZINGATIA BAADA YA KUMALIZA 

1. Ondoa shaka.
2. Ridhika na matokeo kwani hayo ndio sahihi
3. Rudia kuswali tena na tena kama hujapambaukiwa vizuri
4. Penda kulala na udhu baada ya istikhara
5. Usitake majibu yatokee haraka

MATOKEO
  • Kama uliazimia mambo mawili basi utaona nguvu ikielekea juu ya jambo moja
  • Kuonyeshwa majibu katika ndoto

Pia unaweza kutuunga mkono kwa kupitia na darasa hizi


COMMENTS

BLOGGER: 1


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: SALAT AL-ISTIKHARA NA FAIDA ZAKE
SALAT AL-ISTIKHARA NA FAIDA ZAKE
SALAT AL-ISTIKHARA
https://1.bp.blogspot.com/-4utAgIXZo3g/Xmzj4mCFhFI/AAAAAAAARc8/CHJDArH9CukLZvcOqhMzN1IyzVvz2HU5gCLcBGAsYHQ/s400/ist.png
https://1.bp.blogspot.com/-4utAgIXZo3g/Xmzj4mCFhFI/AAAAAAAARc8/CHJDArH9CukLZvcOqhMzN1IyzVvz2HU5gCLcBGAsYHQ/s72-c/ist.png
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/03/salat-al-istikhara.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/03/salat-al-istikhara.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content