Vyakula vimegawanyika katika makundi mengi. Hapa nakudokeza vyakula vya vitamin A pekee

Leo katika makala yetu ya afya
tutazungumzia kwa ufupi kabisa vyakula ambavyo vina vitamin A na, Faida zake, pamoja na hasara
zake kwa kukosa vyakula hivyo.
Muandishi wa makala hii ni mimi SAIDI R BUNDUKI
Moja katika mambo ambayo yanazikumba jamii zetu ni magonjwa mbali mbali kwa watoto na watu wazima. Lakini baadhi ya magonjwa yanaweza kusababishwa na ukosefu ama kuacha kutumia aina ya vyakula aidha kwa kukosa uwezo au kwa kutokujua umuhimu wake katika maisha ya kila siku.
Kama kichwa cha habari kinavyosema, leo tutazungumzia kidogo kuhusu vitamin A
Viko vitamin aina tofauti
tofauti lakini leo nimeona tuzungumzie vitamin A pekee.
Lakini pia unaweza kupitia baadhi ya
posti zetu ambazo tumezungumzia vyakula vya vitamin kwa ujumla.
AINA ZA VITAMI A
Kuna aina mbili za vitamin A
- Aina ya kwanza ni RETINOL, hii ni aina ya vyakula ambayo haina rangi na inapatikana tu katika vyakula vinavyotokana na wanyama, ndege na samaki. Vyanzo vikubwa vya vitamin A aina ya RETINOL ni maziwa ya mama, maziwa ya wanyama na maini.
- Aina ya pili ya vitamin A ni CAROTENES ambayo ni rangi ya njano. Hii inapatikana zaidi katika vyakula vinavyotokana na mimea. Vyakula vya aina hii ni kama vile MAPAPAI, VIAZI VITAMU - (hasa vya manjano), MAPAPAI, MATIKITI, EMBE, MAFUTA MEKUNDU YA MAWESE, KAROTI, MBOGA ZA MAJANI ZILIZOKOLEA UKIJANI N.K.
Kwa ujumlavyakula vyenye vitamin A
kwa wingi zaidi ni maziwa ya mama (zaidi yale ya kwanza (colostrum), ndege,
maini, samaki, kiini cha yai (mayai ya kienyeji), mboga za majani zenye ukijani
zaidi kama vile spinach, kisamvu
lakini pia bila kusahau mahindi ya njano
na ambavyo tumekwisha vitaja hapo awali.
Pia kuna baadhi ya aina ya vyakula
ambavyo vimeongezwa vitamin A, vyakula ivyo ni kama vile SIAGI, MAZIWA YA UNGA
na MAZIWA YA WATOTO.
FAIDA YA KULA VYAKULA VYA VITAMIN ‘A’
- Vitamin A husaidia kuimarisha utando uliopo katika midomo, utumbo, mfumo wa upuaji, kope za macho na hivyo huweza kusaidia kuzuia vijidudu vinavyoweza kusababisha maradhi kuweza kuingia kwa urahisi.
- Vitamin A huimarisha kinga ya mwili hivyo huweza kupambana na vijidudu na kemikali hatari zinazozalishwa mwilini zinazoitwa ‘free radicals’.
- Kuusaidia mwili kuweza kukua vizuri pia kuimarisha afya ya macho kuweza kuona vizuri hata katika mwanga hafifu.
- Kuimarisha ngozi ya mwili, hivyo kuifanya ngozi kutoingiliwa kiurahisi navidudu vinavyoweza kusababisha maradhi.
MADHARA YA KUKOSA VITAMIN ‘A’
Yafuatayo ni madhara ambayo yanaweza
kusababishwa kwa kukosa vyakula vya vitamin ‘A’
- Upungufu wa vitamin hudoofisha kinga ya mwili na hivyo kuwa rahisi kupata maambukizi ya virusi (viral infection)
- Huweza kusababisha upofu (hasa kwa watoto wadogo).
HITIMISHO
Mahitaji ya vitamin A ni muhimu sana
hasa kwa watoto na wamama waja wazito. Hivyo ukiwa kama mzazi ni lazima kulijua
hili katika familia yako. Ingawa baadhi yetu tunaishi katika mazigira ya kimasikini sana
lakini pale ambapo tumepata fursa ni lazima tukumbuke kula/kuwalisha watoto
wetu vyakula hivi ili kuweza kuimarisha afya zao. Hii pia itasaidia kuliokoa
taifa na gharama za matone ya vitamin ‘A’
MWISHO
Unaweza kushea na mwenzio nukuu hii muhimu ili nae aweze kupata somo hili muhimu la afya. Kama una maoni unaweza kutuandikia hapo sehemu ya chini ya COMMENT. Unaweza kuto ushauri au mapendekezo n.k.
Pitia Machapisho muhimu ya afya ambayo huenda uliyakosa
COMMENTS