FAIDA 7 ZA KUSOMA VITABU

Wanasema ukitaka kumficha kitu mswahili basi weka kwenye kitabu. Hii ni kutokana na kutopenda tabia ya kupekua/kusoma vitabu.


Kama kuna orodha ya vitu vinavyochukiwa zaidi na Watanzania basi ni kusoma vitabu. Sijui ni kwasababu gani hasa.

  • Kuenea kwa teknolojia?
  • Kazi nyingi?
  • Uvivu?
  • Hakuna watunzi wazuri?
  • Hatujui umuhimu wake?

Mi nahisi itakuwa ni mazoea tu ama uvivu kama ni teknolojia huko kwa wazungu ndo imeenea zaidi, lakini mbona wao suala la kusoma wameliweka mbele zaidi? Laniki pia tumejaaliwa watunzi wazuri sana wa vitabu mbali mbali katika nchi yetu na pia teknolojia hiyo hiyo imeturahisishia kuweza kusoma vitabu katika simu na kompyuta zetu popote tulipo;-

  • Okeeey tuyaache hayo, najua si wote ambao ni wavivu katika hili. Lakini kama nawe ni miongoni mwa hao, leo nakuletea faida 7 tu za kusoma vitabu.
  • huenda baada ya hapo utapata kitu ambacho kinaweza kukusaidia katika maisha yako ya kila siku.
Nami nitajitahidi kuandika kwa ufanisi na kwa ufupi zaidi ili nisikuchoshe

***********************************


1. Kusisimua akili na kuupa ubongo mazoezi
Ingawa watu wengi hawapendi kusoma lakini ifahamike kuwa kusoma ni jambo ambalo huimarisha sana ubongo katika kufikiri, kuzingatia na kuelewa. Unajisikiaje unaposoma kitu hasa kinachokuvutia kama mfano wa makala hii nzuri?

Unaposoma mara nyingi akili yako inakuwa katika kile ambacho unakisoma. Basi hivi huufanya ubongo wako kuwa makini zaidi kuliko yule ambaye haushughulishi. Kwakuwa wanafunzi wanahitajika kuhimizwa zaidi katika kusoma ili kukuza bongo zao, nawe mtu mzima mwenzangu ni vema ukaanza kidogo kidogo kuuzoesha ubongo wako.

2. Utajiri wa lugha na misamiati
Haijalishi unachokisoma kipo katika lugha gani. Kama ni lugha ya Kiswahili basi utapata maneno mapya ambayo huenda hukuwa unayajua na kama ni lugha yoyote ya kigeni ndio utapata maneno mengi zaidi. Na muda wa kuwa unachokisoma ni chenye kuvutia hivyo ni rahisi zaidi kutafuta kamusi na kujua mengi zaidi.

3. Kupunguza msongo wa mawazo
Kama tulivyosema hapo awali, unaposoma huwa akili yako inaelekea katika kile unacho kisoma zaidi hivyo hupunguza mawazo na kujisikia huru katika akili yako. Na baadaye unaweza kupata suluhisho la kile ambacho kilikuwa kinakusumbua.


4. Kuimarisha uwezo wa uandishi
Si lazima uwe muandishi wa vitabu ndio msomi wa vitabu, imarisha uwezo wako wa kuandika, kuzungumza, kufikirti kwa kusoma vitabu kwani pia ni sehemu ya kuongeza busara.


5. Husaidia kulala
Kusoma hakukusaidii kulala ila kunasaidia kulala kuliko bora zaidi na kuufanya usingi wako kuwa wa amani. Pia kama unaona katika muda huo unataka kulala lakini huna usingizi basi chukua kitabu chenye hadithi nzuuuri na usome utaona matokeo yake. Hivyo kusoma husaidia pia kuvuta usingizi mnono na ndoto nzuuri kabisa.


6. Kuitia muangaza siku yako
Hivi umeshawahi kuwaza kuwa vitabu vinaweza kuleta furaha katika siku yako nzima? Hii hutokea pale ambapo umesoma stori nzuuri ambayo aidha imekuvutia ama imekufundisha kitu na hususan kikawa na manufaa kwako.


7. Kuongeza ubunifu
Kuna tofauti katika kusoma na kuangalia  movie. Katika kusoma huwa unatumia akili niyngi zaidi kuliko pale ambapo unatazama. Ukitazama ni rahisi zaidi fikra zako kuhama na kufikiri jambo jingine tofauti na pale unapo soma akili yote hufikiri kile unachokisoma na kukielewa vizuri na bila shaka unaweza kupata mbinu mpya katika mambo yako. Hii ndio maana tukasema tunaongeza ubunifu.


TUSOME NINI?

Kila mtu ana vitu ambavyo vinamvutia kuvijua, lakini Kuna vitu ambavyo ni muhimu kwa wote. Kwa mfano vitabu vya dini na mafundisho yake n.k. Hapa viongozi wa dini wamefaulu kwa kiasi kikubwa Sana. 

Lakini pia vipo vitabu muhimu vya mafunzo mbali mbali vyenye manufaa kwako Kama vitabu vya afya, hadithi za kale, sayansi n.k.

HIVYO BASI
  • Baada ya makala hii fupi nimekauandalia baadhi ya vitabu ambavyo kwa namna moja ama nyingine vinaweza kukupa faida katika maisha yako. jaribu kupitia hivi.

COMMENTS

BLOGGER: 3


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: FAIDA 7 ZA KUSOMA VITABU
FAIDA 7 ZA KUSOMA VITABU
Wanasema ukitaka kumficha kitu mswahili basi weka kwenye kitabu. Hii ni kutokana na kutopenda tabia ya kupekua/kusoma vitabu.
https://1.bp.blogspot.com/-uKXCqB0IrDQ/XqGRDZD1xyI/AAAAAAAASYo/VpWuqRrOJZQvLkXmfssj3LbfpqVoSvsTACLcBGAsYHQ/s320/bfa86e3361bd0e60.webp
https://1.bp.blogspot.com/-uKXCqB0IrDQ/XqGRDZD1xyI/AAAAAAAASYo/VpWuqRrOJZQvLkXmfssj3LbfpqVoSvsTACLcBGAsYHQ/s72-c/bfa86e3361bd0e60.webp
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/04/faida-7-za-kusoma-vitabu.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/04/faida-7-za-kusoma-vitabu.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content