Mtunzi hapa anasubiri jibu kutoka kwa mwanamke. Ameona amuimbie shairi tamu huenda akapata jibu zuri
Ni zaidi ya ukame, Leo wacha nitamke
Ikufikie Salome, ulotimu mwanamke
Mudi niache niseme, naomba usinicheke
JIBU LAKO NI MUHIMU, ZAIDI YA MBONI YANGU
Natambua una mume, hata nami nina mke
Jua mimi ni kidume, ni vema niwajibike
Kwako nazima umeme, mwili wako na uwake

hata wanikite sime, kwako nisitetereke
ujumbe huu usome, jibu zuri utamke
Ukinambia NIKOME, utafanya niteseke
JIBU LAKO NI MUHIMU, ZAIDI YA MBONI YANGU
Wallahi sikuangushi, jaribu hautojuta
Takunyunyiza marashi, ukirowa nakufuta
Sitokupa kashi kashi, Mudi sinaga matata
JIBU LAKO NI MUHIMU, ZAIDI YA MBONI YANGU
Kichozi chalenga lenga, kuisubiri ahadi
Nahisi umenitenga, Beby nahisi baridi
Unaponipiga chenga, kulia itanibidi
JIBU LAKO NI MUHIMU, ZAIDI YA MBONI YANGU
Kama pepo ipo kweli, basi nahisi ni wewe
Ninapokula ugali, mboga yangu huwa wewe
Nakupenda mwanamwali, raha yangu kuwa nawe
JIBU LAKO NI MUHIMU, ZAIDI YA MBONI YANGU
Limetungwa na : Mohammed S Shaban Sindi
MKALAMO PANGANI
COMMENTS