'Assalaaam alaykum warahmatullaahi wabarakaatuh' Ukiona mtu mzima analia, ujue kuna jambo Tunamshukuru Mwenyezimungu kwa ...
'Assalaaam alaykum
warahmatullaahi wabarakaatuh'
Ukiona mtu mzima analia, ujue kuna jambo
Tunamshukuru
Mwenyezimungu kwa kutujaalia afya njema na uhai. Mimi na wewe leo tumefanikiwa
kuipata ramadhani tukiwa na afya njema wakati kukiwa na wenzetu ambao
wametangulia mbele ya haki (wamefariki), kwani nao walitamani kufunga kama sisi. Tunapaswa tumshukuru Mwenyezimungu kwa kutupendelea.
siku chache zilizopita waislamu duniani kote wameanza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani
Kilio changu ni juu ya hali tulionayo leo kama dunia, bara, nchi, na hata
kaya zetu. Janga hili ni gonjwa hatari la mlipuko la corona.
Hii
imepelekea leo waislamu tunalia chini chini na mara nyingine kwa wazi wazi hata kama baadhi yetu vinywa vyetu viko kimya.
Haya ni maneno ambayo nimeongea na nafsi yangu lakini hatimaye moyo ukashindwa kunyamaza na mikono kuchukua hatua ya kukuandnikia wewe katika waraka huu.
KWANINI NALIA?
Nalia kwa sababu nilizoea kwamba - MWEZI WA RAMADHANI NI.................
1. Mwezi wa kutembeleana
Iko
wapi furaha yetu leo katika kutembeleana baina ya ndugu na ndugu, rafiki
na rafiki na muislamu na muislamu mwenzake? Leo waislamu tumekuwa ni watu
wa kunyanyapaana kutengana na kukimbiana. Na hii si kwa sababu ya kupenda ila ni kwasababu ya Korona
Iko
wapi furaha yetu, uko wapi utamaduni wetu wa kupeana mikono na kukumbatiana?
KORONA IMETUTAWANYA
2. Mwezi wa kula pamoja
Mwezi
wa kualikana futari na vyakula kem kem kula na kucheka pamoja. Masikini,
mafukara, wapita njia, wasafiri na wenye haja tulikuwa tunakula nao pamoja
futari nje katika jamvi. Leo tunajifungia ndani na familia zetu na kuwaacha
wasafiri ambao wamekatikiwa na safari kuteseka.
Yote hii ni kwa sababu ya Korona (Covid 19)
3. Mwezi wa kuswali swala
za jamaa
Ziko
wapi sala tano za jamaa? Zikifuatiwa na nyiradi zetu kule kijijini kwetu baada ya sala? Nyiradi
za kuomba msamaha na pepo ya Mwenyezimungu. Leo tumejibanza katika majumba yetu
na kuswali peke yetu na familia zetu.
4. Mwezi wa kukutana
katika darasa za ilmu
Huenda tulitarajia kuhudhuria katika darasa mbali mbali za tafsiri ya Quran, fiqihi na masomo mengine mengi ya dini. Leo hakuna tena darasa hizi. Tulitarajia kupata faida kutoka kwa
mashekhe zetu na kuuliza maswali yetu yanayotutatiza huku tukijibiwa pamoja na
kucheka na kufurahi na mashekhe zetu. Kabla ya kuomba dua kwa pamoja "Rabbana nfaanaa bimaa allamtanaa"
Leo
darasa zimekuwa mtihani na hatuna jinsi, tunaendelea kujifungia majumbani huku
nyoyo zetu zikimlilia Allah atuepushe na janga hili.
Ramadhani imekuwa ngumu kisha ikawa ngumu tena, si kwa waislamu peke yao bali ni kwa watu wote. Unajua ni kwanini?..........
Biashara / kazi / ajira zimeyumba
Tunajua
kuwa binadamu huishi kwa kutegemeana, hivyo mmoja anapokuwa amekwamisha
mzunguuko wa maisha basi sote tutakuwa tumekwama.
Leo biashara zetu zimekuwa
ngumu kutokana na baadhi ya maofisi kufungwa na mashule kwa ujumla. Inafikia kipindi
unakosa hata pesa ya kutumia.
Unatamani kumpa mzazi wako, ndugu yako, jamaa yako walau shilingi elfu moja ya
fungu la muhogo kwa ajili ya futari lakini unashindwa. Wakati huo huo mwenye
nyumba anataka kodi yake, bila kusahau bili ya umeme, maji n.k
TUFANYE
NINI?
Nikisema
sijui cha kufanya nitakuwa muongo. Chakufanya kwanza kabisa ni kuendelea
kumuomba Mwenyezimungu atuondolee janga hili kwani kwake yeye hakuna jambo
zito.
Tusisahau kuchukua tahadhari zinazosemwa na wataalamu wetu wa afya ili tuwe
salama na tuwaokoe wengine. Lakini pi tusisahau kuwaombea wenzetu ambao
wametangulia mbele ya haki kwa ugonjwa huu Mungu azipe subira familia zao na
awaweke pema peponi. Lakini kwa wale wagonjwa Mungu awasaidie wapone.
Nawe
chukua nafasi hii kuzungumza na watu wa
karibu yako juu ya kumuomba Mwenyezimungu ILI kutuondoshea Mtihani huu bila
kusahau kuchukua tahadhari kama isemwavyo.
TAHADHARI
NI BORA KULIKO DAWA
Hiki
kilikuwa ni kilio changu.
Ni
mimi mandishi wako SAIDI R BUNDUKI.

True
ReplyDelete