Magonjwa 14 ya milipuko kuwahi kutokea kabla ya KORONA

Tuko katika janga la gonjwa la mripuko (CORONA). Lakini kumbe huko miaka ya nyuma kuna magojnwa mengi yalizuka na kuuwa watu wengi

                                        

Katika historia ya mwanadamu yamepita magonjwa mengi  hatari ya milipuko. Magonjwa ambayo yaliutingisha ulimwengu kwa namna moja au nyingine. Leo nitakusogezea magonjwa 14 hatari zaidi kuwahi kutokea katika ULIMWENGU.


1. The black death
Ugonjwa huu ni aina ya ugonjwa ambao unatokana na bacteria wanaitwa Yersinia pestis ambao inasemekana kuwa husababishwa na utitiri uliotoka katika panya. Ugonjwa huu ulitoka bara la Asia mpaka Ulaya (Europe) 

Ni pigo liliobadilisha kabisa historia ya bara la Ulaya ambapo watu walipoteza ajira, kupanda kwa bei za vyakula lakini pia huenda ikawa ni chachu ya maendeleo  katika kuifanya teknolojia kukuwa zaidi. Hii ilikuwa ni mwaka 1346 hadi 1353.


2. Cocoliztli epidemic
Hii ni homa ambayo ilisababishwa na virusi vililvyojulikana kama 'hamorhagic'Janga hili lilitokea huko nchini Mexico mwaka 1545 - 1548 na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu milioni 15 wa Mexico na Amerika na kati.

Hivi karibuni wanasansi walifanya uchunguzi wa DNA kutoka katika mifupa ya baadhi ya watu na kugundua kuwa watu hao waliambukizwa na vijidudu vinavyojulikana kama        'S. paratyphi C' ambapo pia huweza kusababisha homa iitwayo ENTERIC FEVER  hii ni jamii ya homa ya TYPHOID ambayo bado ni tishio mpaka leo.


3. American plague
Haya ni miongoni mwa magonjwa ya mlipuko ambayo yaliletwa na wapelelezi kutoka bara la Ulaya ambayo miongoni mwao ni NDUI. Gonjwa hili ni miongoni mwa magonjwa ambayo yaliwamaliza sana watu wa magharibi zaidi ya 80%.

Magonjwa haya yalilisaidia jeshi la Uhispania lilioongozwa na Hernan cortes kushinda mji mkuu wa Aztec na mnamo mwaka 1519 na jeshi jingine la Uhispania lilioongozwa na Francisco Pizzaro kushinda Inca  mnamo mwaka 1532.


4. Great plague of London
Balaa hili huko Mjini London liliuwa watu wengi tena wakiongozwa na kiongozi wao wa enzi hizo mfalme CHARLESS II ambalo lilianza mwaka 1665. watu zaidi ya 100,000 walifariki ikiwa ni asilimia 15% ya watu wote wa London kwa wakati huo. Lakini pia hii haikuwa mwisho wa majanga ya mji huo kwani ilifuatiwa na kuzuka kwa moto mkubwa Mjini London THE GREAT FIRE OF LONDON mwaka 1666 ambao ulidumu kwa siku 4.


5. Great Plague of Marseille
Huu ulikuwa ni mlipuko wa ugonjwa ulioitwa BOBUNIC ambao ulienea kutoka magharibi mwa Ulaya kuelekea Marseille Ufaransa mnamo mwaka 1720. Ugonjwa huu uliwauwa watu 150,000 katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo. Pamoja na kuwa watu wengi na nguvukazi waliangamia lakini Marseille ilisimama tena kiuchumi baada ya miaka michache.


6. Philadelphia yellow fever epidemic
Hii ni homa ya manjano ambayo iliingia katika maeneo hayo. Wazungu waliamini kuwa watu weusi walikuwa na kinga dhidi ya ugonjwa huo ndipo waliandikishwa ili kuwanyonyesha watoto. Lakini ikawa kinyume na matarajio yao mpaka walipokuja kushituka zaidi ya watu elfu tano (5,000) walikuwa wamesha kufa. Hii ilikuwa ni mwaka 1793.


7. Flu pandemic: 1889 - 1890
Mafua haya hatari yaliyotokea huko Urusi yaliweza kuenea haraka hasa kupitia mikusanyiko na vyombo vya usafiri na kuuwa watu zaidi ya milioni moja ndani ya miezi michache.


8. American polio epidemic
Polio iliyozuka huko America ilisababisha visa zaidi ya 27,000 na vifo 6,000. Ugonjwa huu huathiri sana watoto na wakati mwingine pia husababisha ulemavu wa kudumu. Ugonjwa wa polio ulikuwa unatokea mara kwa mara huko Amerika na duniani kwa ujumla mpaka pale chanjo ilipopatikana mnamo mwaka 1954. Chanjo hii ilipunguza sana na kusaidia katika ugonjwa huu mpaka sasa polio imesahaulika kabisa.


09. Spanish Flu
Haya ni mafua ambayo yalizuka huko nchini Uhispania mwaka 1918 - 1920. Takriban watu milioni 500 waliathiriwa na mafua haya ambapo theluthi ya idadi hii walifariki. Lakini pia wataalamu wanasema kuwa ugonjwa huu haukuanzia Uhispania lakini uliathiri zaidi nchi hii ndipo jina likapatikana kama Spanish Flu.10. Asian Flu
Haya ni miongoni mwa mafua ya ndege kuwahi kutokea huko China ambapo watu zaidi ya milioni moja waliathiriwa. Gonjwa hili liliathiri sehemu nyingi kwa muda tofauti ikiwemo HONGKONG na SINGAPORE 1957.


11. AIDS pandemic and epidemic
Zaidi ya watu milioni 35 wameathirika na ugonjwa huu hatari tangu ulipogundulika. Virusi vya VVU ambavyo ndivyo husababisha Ugonjwa huu viligundulika kutoka kwa Sokwe kuja kwa binadamu huko AFRIKA MAGHARIBI mwaka 1920. Virusi vilienea Ulimwenguni kote na kuwa ugonjwa mwishoni mwa Karne ya 20. Mpaka sasa ugonjwa huu hauna dawa maalum ambayo imegundulika ila zipo dawa za kureusha maisha na kupunguza makali ya virusi.


12. H1N1 swine Flu pandemic 2009 - 2010
Hii ni homa ya nguruwe iliyojulikana kwa jina la H1N1 ambayo ilianzia huko Mexico mwaka 2009 na kuenea ulimwenguni kote. 

Unaambiwa ndani ya mwaka mmoja virusi hivi vilienea kwa watu zaidi ya bilioni 1.4 na kuuwa watu zaidi ya 200,000. Ugonjwa huu uliathiri zaidi watoto na watu wazima walio na umri zaidi ya miaka 65


13. West African Ebola epidemic 2014 - 2014
Ugonjwa huu ulianzia huko afrika Magharibi na mtu wa kwanza alipatikana nchini Guinea mnamo mwaka 2013. Watu elfu 28 waliathirika huku zaidi ya 11,000 wakipoteza maisha. Nchi zilizoathirika zaidi na Ebola ni pamoja na Sierra leone na Liberia. Lakini pia ziko baadhi ya nchi ambazo zilipitiwa na gonjwa hili ikiwemo Nigeria, Mali na Senegal. Inasemekana ugonjwa huu umetokana na POPO na kwa mara ya kwanza ugonjwa huu ulianzia Kongo (DRC) mnamo mwaka 1976.


14. Zika Virus Epidemic 2015 - ......
Amerika ya kusini na Amerika ya kati ndiko janga hili la virusi vya zika lilikoanzia. Ugonjwa huu huweza kuenezwa na MBU lakini pia hata ngono huweza kueneza ugonjwa huu. ingawa si hatari sana kwa watu wazima lakin unaweza kuwa hatari kwa watoto wachanga hasa walioko tumboni na kuweza kusababisha kasoro za maumbile wanapozaliwa. Mbu hawa wenye uwezo wa kubeba virusi hivi huishi katika maeneo ya unyevu na maeneo ya joto.

Asante kwa kusoma makala hii.

Imeandaliwa na Saidi Bunduki kwa msaada wa mtandao

Makala nyingine muhimu zilizopita
Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: Magonjwa 14 ya milipuko kuwahi kutokea kabla ya KORONA
Magonjwa 14 ya milipuko kuwahi kutokea kabla ya KORONA
Tuko katika janga la gonjwa la mripuko (CORONA). Lakini kumbe huko miaka ya nyuma kuna magojnwa mengi yalizuka na kuuwa watu wengi
https://1.bp.blogspot.com/--No5rT6M7yw/Xo7rrvsnDHI/AAAAAAAASCs/j2lV-M2CDV4HVhtaC1KjD-gclazsR3UKwCLcBGAsYHQ/s320/1111.webp
https://1.bp.blogspot.com/--No5rT6M7yw/Xo7rrvsnDHI/AAAAAAAASCs/j2lV-M2CDV4HVhtaC1KjD-gclazsR3UKwCLcBGAsYHQ/s72-c/1111.webp
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/04/magonjwa-14-hatari-ya-milipuko-kuwahi.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/04/magonjwa-14-hatari-ya-milipuko-kuwahi.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content