SAFARI YA MASHAKA (2)

Katika maisha mwanadamu hupitia mambo mengi sana yakiwemo mazuri na mabaya. Leo nitashea nawewe stori ambayo ilinitokea mnamo mwaka 2007 nikiwa kidato cha tatu huko katika shule ya sekondari Funguni - Pangani Tanga.

Hii ilikuwa ni safari fupi yenye mateso kutoka katika Mji wa Pangani kuelekea kijijini kwetu Mkalamo, hiki kilikuwa ni kipindi cha likizo ya mwezi wa 6. Safari hii nilikuwa mwenyewe na nilikuwa natumia baiskeli katika safari. Unajua shida ilikuja wapi? Endelea.


**********************

Kwa kawaida wanafunzi wakifunga shule hurudi makwao kwa ajili ya kupumzika, kuwasalimia wazazi ndugu na jamaa lakini pia kujiandaa muhula mwingine wa masomo.

Saidi Rashidi Bunduki wakati huo nikiwa ni mwanafunzi wa kidato cha tatu, baada ya kufunga shule nikaona ni fursa adhimu kurudi kwa wazazi. 

Niliandaa baiskeli yangu siku kadhaa kabla ya safari yangu na siku  ya jumapili niliamua kuanza safari. Nikiwa peke yangu pamoja na begi langu la nguo katika kiti cha nyuma cha baiskeli yangu aina ya Phoenix kwa wakati ule zikiwa zinatamba.

Mwanzo wa safari

Nilidamka asubuhi na kujiandaa kama ilivyo ada kwa msafiri na mnamo majira ya saa 12 asubuhi nilianza rasmi safari yangu kwani sikuweza kutoka mapema zaidi ya hapo kufuatia ratiba ya kivuko chetu cha MV PANGANI kuanza kazi zake saa 12 asubuhi.

Mfukoni mwangu nilikua na akiba ya pesa kiasi cha shilingi elfu moja tu (Tsh 1,000/=) 
Kivukoni nilitumia shilingi mia tatu na kubaki na shilingi mia saba. Nilianza kupekecha baiskeli yangu mpaka katika Kijiji kinachoitwa MIKINGUNI umbali wa takriban kilomita kumi toka kuanza safari yangu. 

Hapa saa mkosi ndipo ulipoanzia πŸ”ΊπŸ”Ί

Baiskeli ilianza kwa kupata pancha tairi la mbele, nikatafuta fundi na kuziba ile pancha. Nilipomueleza fundi sehemu ambayo ninapokwenda yule fundi aliamua kunionea huruma na kunisamehe ile pesa. (Mungu ambariki yule bwana popote alipo)

Majira ya saa tatu asubuhi, nilifika katika Kijiji kinachoitwa SAKURA umbali wa takriban kilomita 30 kutoka mwanzo wa safari yangu. 

Hapa niliamua kupata kifungua kinywa (chai) na kutumia shilingi mia tano (500/=) nikabaki na shilinig mia mbili tu katika mfuko wangu wa suruali ikiwa kama akiba  yangu safarini.

Niliamini kufika salama ninakokwenda lakini mambo yalikuwa tofauti pale tu nilipoondoka katika kijiji kile. Nilitembea umbali wa takriban kilomita mbili tu na kukutana na balaa jingine. 

Sikuamini macho yangu pale ambapo nikiwa katika mteremko mkali na kusikia basta moja matata sana katika mpira wa nyuma. 

Sikuwa na jinsi zaidi ya kushuka katika baiskeli yangu na kuanza kutembea kukitafuta kijiji kifuatacho ambacho hujulikana kama "Makorora"

Kipande kile kilikuwa na mbuga na vichaka na ilikuwa ni sehemu ambayo hakukuwa na  nyumba wala shamba kwa wakati ule. Nilianza kukokota baiskeli yangu mpaka majira ya saa sita mchana nilijaaliwa kufika katika kijiji kile. Kumbuka kuwa akiba nilionayo ilikuwa ni shilingi mia mbili tu (200/-)

Kwa bahati nzuri katika kijiji kile kulikuwa na mama yangu mdogo ambaye alikuwa anaishi pale. Kitu ambacho nilishukuru ni baada ya kufikia kwake na kupata chakula cha mchana na pia alinipa shilingi mia mbili kwa ajili ya kwenda kuziba ile pancha. Nilitumia shilingi mia moja na mia nikatia mfukoni. Akiba yangu sasa ikawa ni shilingi mia tatu.

Mama alinikataza kuondoka siku ile kwa kuwa muda ulikuwa umesonga sana  na niendako bado ni mbali. Nilikubali kwa shingo upande kwa sababu nilikuwa na hamu sana na ndugu zangu.

Siku ya pili asubuhi nilianza safari majira ya saa moja asubuhi, Baada ya kukaribia katika kijiji kinachoitwa mikocheni nilipata tena pancha na kuziba kwa fundi na kutumia shilinig mia moja.

Nilichoka sana na safari ile, ilifika kipindi nilitamani nirudi nilikotoka lakini nako kulikuwa mbali. Pia changamoto ni kwamba hakukuwa na gari ya moja kwa moja kutoka Pangani Mpaka kijijini kwetu. Hali hii ilitusumbua sana.

Safari bado inaendelea

Nilipofika katika kijiji cha Mkwaja sikutembea umbali mrefu nikapata tena pancha katika tairi ya nyuma, hapa nikaamua kujitoa muhanga kutembea kwa mguu mpaka nitakapifika Mkalamo. Hapa ni sehemu ambayo sitaisahau katika maisha yangu.

Kipande hiki cha safari ndipo ilipo mbuga ya wanyama ya SAADANI NATIONAL PARK mbuga ambayo ina wanyama wengu hatari pamoja na wahalifu mbali mbali wa kibinaadamu.

Pia kibaya zaidi ni kwamba kile kilikuwa ni kipindi cha jua kali, Njaa inaniuma na hakuna mji, shamba, makazi wala huduma yoyote ya jamii.

 Mwanaume mfukoni nimebki na shilingi mia mbili tu Baiskeli ina mzigo wa begi kubwa la nguo
Na nipo peke yangu.


*************************

Nilianza kusakata rhumba lile la safari ya mashaka mpaka nilipofika sehemu na kuamua kukaa chini kusubiri kama nitapata msaada wowote. Njiani nilikuwa nakunywa maji tu katika mifereji iliyo pembezoni mwa barababara (maji machafu).


Wahenga walisema kuwa ukiwa umeharibikiwa na baiskeli kwa tatizo la pancha inawezekana kuutoa mpira wa ndani na kuweka majani.

 Sikuwa na uhakika na kauli hii lakini niliamua kujaribu lakini jitihada zangu ziligonga mwamba kwa sikuwa na kisu wala spana ya aina yoyote. Niliamua kukaa chini ya mti ka kuanza kuangua kilio.πŸ˜“πŸ˜“πŸ˜“

Baadaye nikaona kuwa kilio hakingenisaidia chochote, nikaamua kujikaza kiume na kuendelea na safari yangu ngumu.

Majira ya saa tisa jioni nilibahatika kufika katika sehemu ambayo hupatikana huduma za jamii. Sehemu ile ilikuwa na mgahawa na mafundi wa baiskeli,  (njia panda ya Mbulizaga).

Kwa bahati nzuri sehemu ile niliwakuta jamaa wawili ambao tunafahamiana walikuwa wakila nanasi,nami nikajiiunga nao kupata rizki. nguvu ziliniishia lakni nilijikaza.

Sikuwa na uwezo wa kuitengeneza baiskeli yangu kwa sababu kuu mbili

1. Sikuwa na pesa ya matengenezo
2. Haikufaa tena kutengeneza, kwa sababu mpira ulichakaa sana.

Nilipumzika pale kwa muda wa takriban saa moja na kisha kuanza kibarua cha safari yangu kuelekea kijijini. 

Wakati huo nyumbani wamepigiwa simu kuwa nimeshaondoka pangani lakini walishangaa kuona sifiki na hatimaye walianza kupata wasi wasi. Hasa ukizingatia katika safari ile njiani kuna mbuga ya wanyama ya Saadani. Walihofu huenda nimetafunwa na simba.

Kadiri safari ilivyozidi ndipo mwendo ulizidi kuwa mdogo kutokana na uchovu na maumivu ya miguu. 

Wataalamu wa mambo wanasema kuwa umbali wa kutoka pale ambapo nilianza safari kwa mguu (MKWAJA) mpaka MKALAMO ni umbali wa takriban maili 25.

 Unaweza kuona ni safari ndogo lakini kwa kijana wa miaka 17 ambaye hana uzoefu wa kutembea kwa mguu ni mtihani mzito. Ukijumlisha na milima na njia chafu ya barabara (Rough road)

Hatimaye

Kwa Uwezo wa Mwenyezimungu Nilifika salama kijijini siku ile ya pili majira ya saa moja usiku na niliwakuta wakinisubiri kwa hamu.

MAISHA NI SAFARI NDEFU SANA

MWISHO

UKUMBUSHO
Yeyote anaweza kushea mkasa wake ambao ameupitia maishani mwake kwa kututafuta katika namba zetu zilizopo hapo sehemu ya contact.

Imeandaliwa na kusimuliwa na Saidi Rashidi Bunduki

Usiikose SAFARI YA MASHAKA (3) ambayo ilitokea huko 'Mnazi mmoja' Boza Pangani. Hii bwana tulilishwa machungwa kwa lazima baada ya kukutwa shambani kwawatu 

USIKOSE MZEE MWENZANGU

Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: SAFARI YA MASHAKA (2)
SAFARI YA MASHAKA (2)
https://1.bp.blogspot.com/-QP8N6hN6u1g/Xz_GrHqNURI/AAAAAAAAXVM/Bc89ZRSgBGojaLXi3HiHhm0I0_NOMT8pACLcBGAsYHQ/w364-h183/mfano%2Bhai.png
https://1.bp.blogspot.com/-QP8N6hN6u1g/Xz_GrHqNURI/AAAAAAAAXVM/Bc89ZRSgBGojaLXi3HiHhm0I0_NOMT8pACLcBGAsYHQ/s72-w364-c-h183/mfano%2Bhai.png
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/04/safari-ya-mashaka-2.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/04/safari-ya-mashaka-2.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content