Hiki ni kilio cha mjane aliyeondokewa na Mumewe. Mungu azilaze pema roho za marehemu wote AAMIN
Wacha niimbe walaU, japo huto nisikia
Si kama napiga mbiU, niwewe nakulilia
Sijaiona nafuU, nalia bado Nalia
Umeniacha na nani?
Umekatika umeME, sasa nipo kwenye kiza
Yapasayo niyaseME, ya siri nitabakiza
Meacha watoto muME, kutwa wanakuuliza
Umeniacha na nani?
Umetoka duniaNI, Ni punde hujaugua
Ulenda kibaruaNI, wana kuwatafutia
Akakupenda ManaNI, nyumbani hukurejea
Umeniacha na nani?
Wanao wanililiA, mama yukowapi baba
Sina Cha kuwaambiA, majonzi yamenikaba
Hasa mwanao SofiA, Umemwacha wiki Saba
Umeniacha na nani?
Likikuchwa kunakuCHA, na usiku wa manane
Huficha yetu makuCHA, huridhika na ukame
Mama na mama kachaCHA, hunifariji mjane
Umeniacha na nani?
Hakika zile AmaNA, Kaka ameshazilipa
Na shemeji yako mwaNA, chochote yu ananipa
Side analia saNA, imemvimba mishipa
Umeniacha na nani?
Sina budi lea WaNA, madrasa watasoma
Wamjue MaulaNA, wakwombee dua njema
Iwe kwako AljanNA, mume wangu lala pema
Umeniacha na nani?
Umeniacha na NaNI? Swali hili Sina jibu
Jibu analo MannaNI, kwa hili linonisibu
Nahisi nipo njiaNI, kuja huko ni wajibu
U, ME, NI, A, CHA, NA, NA, NI?
Nimependa ujuzi, umwanagenzi makini wa lugha
ReplyDeleteHa ha ha haaaa eti mwanagenzi��
Deleteasante bwana Meck
Delete