FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA PID

Baadhi ya maradhi ni kwa ajili ya jinsia fulani tu. Hapa tunazungumzia ugonjwa ambao huwapata wanawake pekee (PID)


Sitaki nikuchoshe;--

ILA

Huenda ukawa ndio mara yako ya kwanza kukutana na jina la ugonjwa huu. 


Kama jibu ni 'NDIO', basi wacha nikujuze;-

PID ni kirefu cha neno “Pelvic Inflammatory Disesase’ Ni ugonjwa wa maambukizi unaotokea katika via vya uzazi wa mwanamke ambapo huhusisha maambukizi katika shingo ya kizazi (CERVICITIS), nyama katika mfuko wa uzazi (ENDOMETRITIS) na mirija ya uzazi (SALPINGITIS)

Unajua kwanini nimeamua kukudokezea dondoo hii?
Kwasababu

Kundi kubwa la wanawake wamekuwa wakiteseka na tatizo hili, bila kupata msaada wa tiba huku wakibaki na madhara makubwa kama ugumba n.k.


VYANZO NA VIHATARISHI VYA KUPATA UGONJWA WA PID

Vimelea aina ya NEISSERIA GONORRHEA pamoja na CHLAMYDIA TRACHOMATIS ndio chanzo cha maambukizi ya ugonjwa wa PID ingawaje kuna aina kadhaa za vimelea vinahusishwa kusababisha ugonjwa wa PID hivyo nilivyotaja ndio vinaongoza Kwa umaarufu kusababisha ugonjwa huu.

ZIKO NJIA HATARISHI AMBAZO HUSABABISHA MAAMBUKIZI HAYA NAZO NI;-

 •   Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango
 •      Kufanya ngono isio salama (Ngono zembe)
 •   Maambukizi katika njia za uzazi baada ya kujifungua ama mimba   kuharibika.
 •     Kuambukizwa kupitia damu iliyo athirika na ugonjwa huu.
 •     Kupata maambukizi kupitia wakati wa kutoa mimba kwa njia zisizo salama.

DALILI ZAKE
Kuna dalili mbalimbali zinazoweza kuashiria ugonjwa huu wa PID miongoni mwa dalili hizo ni;-

 •     Mwanamke kupata maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
 •     Kupata maumivu wakati wa kukojoa
 •     Kupata homa na kuhisi kichefuchefu
 •     Kupata maumivu ya mgongo na kutapika
 •     Kutokwa na hedhi bila mpangilio
 •     kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
 •     Kutokwa na uchafu mweupe ukeni unaotoa harufu mbaya

NJIA ZA KUEPUKA UGONJWA WA PID
Pamoja na kuwepo kwa dawa za kutibu tatizo hili ni vyema ukajiepusha na  vihatarishi vya kupata tatizo hili kwa kuzingatia yafuatayo,

 •           Epuka kufanya ngono isiyo salama.
 •           Jiwekee tabia ya kufanya vipimo mara kwa mara hasa kizazi
 •    Usifanye mapenzi mara baada ya kujifungua au mimba kutoka mpaka utakapohakikisha shingo ya uzazi imefunga vema.
 •           Kuwahi kuonana na daktari unapoona dalili za ugonjwa
 •          Kuwa msafi na kula lishe bora

Note:
Uonapo dalili za ugonjwa huu wahi kupata matibabu kwani ugonjwa huu huweza kusababisha ugumba  ikiwa hautapata tiba vizuri.COMMENTS


Follow - ili usipitwe

Kwa mawasiliano zaidi

Name

Afya,66,Blogging,18,Burudani,29,Dini,99,Maisha,38,Mashairi,52,Sitosahau,37,Teknolojia,6,Usichokijua,14,
ltr
item
mrbunduki: FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA PID
FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA PID
Baadhi ya maradhi ni kwa ajili ya jinsia fulani tu. Hapa tunazungumzia ugonjwa ambao huwapata wanawake pekee (PID)
https://1.bp.blogspot.com/-RKrRkPOZAdc/Xs-Q1Dm_JmI/AAAAAAAATVc/R1GkTouYvvk-wgWBOMWF4FqE868Rm9oSwCLcBGAsYHQ/s320/Blausen_0732_PID-Sites.png
https://1.bp.blogspot.com/-RKrRkPOZAdc/Xs-Q1Dm_JmI/AAAAAAAATVc/R1GkTouYvvk-wgWBOMWF4FqE868Rm9oSwCLcBGAsYHQ/s72-c/Blausen_0732_PID-Sites.png
mrbunduki
https://www.mrbunduki.com/2020/05/fahamu-kuhusu-ugonjwa-wa-pid.html
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/
https://www.mrbunduki.com/2020/05/fahamu-kuhusu-ugonjwa-wa-pid.html
true
3501413861140022348
UTF-8
Loaded All Posts Hakuna chapisho lolote View All Read more Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All Recommended posts LABEL ARCHIVE Search/Tafuta ALL POSTS Bahati mbaya, Ulichotafuta hakipo Rudi nyumbani/Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content